Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Sikiliza waongo


Ukimwi unaua: Asema Kenedy Ochieng


Gazeti INJILI
Kwenye Internet
-
http://www.munishi.com

Tel. 254-722-602445 E-mail:
munishi@munishi.com

Kiboro ametoka Nation yakarabatiwa


Gazeti la Nation kwa mara nyingine wamegeuza sura, Baada ya mkurugenzi wa zamani bwana Wilfred Kiboro kuonyeshwa mlango. Mkurugenzi mpya amekuja na mbinu mpya. Ana kibarua kizito kurudisha heshima ya Nation kama gazeti linalozingatia maadili ya taaluma ya uandishi habari.

Miaka sita iliyopita waligeuza sura bila mafanikio, na sasa wanaonekana hivi. Wanadai wataalamu wao walikaa takriban miezi tisa kubuni mpangilio wa Nation inavyoonekana sasa. Pamoja na majigambo hayo, pia NTV ilitangaza LIVE wafanyikazi wa shirika hilo wakiuza magazeti yenye sura mpya kwenye barabara za Nairobi. Kilichowashangaza wengi, ni jinsi walivyoitumia TV kuwalazimisha watu watoe maoni waliyotaka kusikia. Asubuhi saa kumi na mbili na nusu, NTV walionekana wakichukua maoni kutoka kwa watu waliowaita wasomaji, na wote walionekana wakiwamwagia sifa tele kuhusu muundo wao mpya wa gazeti pamoja na mpangilio wa makala. Wengi tulijiuliza wamesoma saa ngapi na kufikia hatua ya kusifu au kukashifu? Japo hakuwepo wa kuwakashifu. Nimroho Taabu alikuwa studio, wakati Shaaban Ndege alikuwa barabarani akiwahoji kuanzia wauzaji na wasomaji, na hata wafanyikazi wenzao ambao siku hiyo waligeuka WAMACHINGA wa kuuza magazeti. TABU alipomuuliza Shabani vipi kuhusu kurasa za gazeti hilo ambazo awali zilikuwa 30 na sasa ni 72, Jibu lilikuwa watu wamezifurahia sana na ndiyo maana wamesoma haraka na kumaliza na saa moja kamili wanatoa maoni yao jinsi sura mpya ya Nation ilivyowavutia. Iliwabidi NTV wafanye kile ambacho hawafanyi yaani kuwa na kipindi cha leo magazetini. Tofauti na KBC pamoja na CITIZEN, Leo magazetini ya Nation ilikuwa na gazeti moja tu, nalo ni Nation Mpya iliyokuwa inajiuza na siyo kujitembeza.

Lakini wengi waliiona hatua ya NTV kujipigia debe asubuhi kama kibaya kinachojitembeza. Japo mimi siku hizi sinunui magazeti, lakini siku hiyo ilinibidi ninunue nione jipya ndani ya Nation mpya. Sinunui magazeti kwani kila asubuhi KBC hunisomea magazeti yote kwenye kipindi chao cha DAMKA na KBC channel one.Lakini tofauti na siku nyingine, siku hiyo walionyesha kichwa cha habari katika Nation, lakini siyo nembo yao. Kwamba wanatumia magazeti yao kila asubuhi kuwafanya watazamaji watizame kipindi chao cha leo magazetini, na leo gazeti mojawapo limegeuza sura yake na KBC wakatae kuonyesha, hilo kidogo lilinikera. Ikiwa vyombo vya habari vinaogopana kiasi hicho, kwa nini KBC wayatumie magazeti kutayarisha kipindi huku wakiwanyima wenzao haki ya kuonekana kwenye TV yao wakati wanapogeuza sura ya gazeti lao? Hayo tuwaachie wenyewe, wanajuana kwa vilemba. Nilipolinunua gazeti la siku hiyo kweli kulikuwa na mabadiliko. Pengine siyo kama wenyewe walivyotia chumvi nyingi, lakini binafsi niliona kuna mtizamo mpya wa masuala hasa ya siasa na kidini.

Japo walijigamba kwamba iliwachukua miezi tisa kuunda mpangilio wa herufi na sehemu za kuweka picha pamoja na LAYOUT nzima ya gazeti, mimi niliona kwamba kazi hiyo ukimpa mpiga chapa anayejua kutumia PAGE MAKER, itamchukua muda usiozidi masaa mawili kuja na mpangilio mzuri kuliko huo wa Nation inayoitwa mpya.

Lakini kwenye maoni ya mhariri walionyesha kwa mara ya kwanza kuipinga Serikali ya Kibaki kwa kile walichokiita mwingilio wa serikali kuusambaratisha upinzani kama CCM inavyofanya huko Tanzania. Pia walifanya kile ambacho wengi hawakukitarajia kwani kwa miaka ya hivi karibuni Nation ilionekana kulegeza kamba na kuinamia upande wa serikali. Kwenye toleo lao jipya walimwambia Kibaki usoni kwamba kama mbinu anazotumia zinalenga kumrudisha madarakani kwa gharama yeyote, basi mambo yatamwendea kinyume. Walienda hatua zaidi na kuchora katuni ya Kibaki akiletewa barua isemayo ODM wamemngatua madarakani. Kwangu hiyo ni hatua nzuri kuelekea pazuri. Serikali hazipaswi kuumaliza upinzani ndipo zijigambe kwamba zimerekebisha uchumi.Serikali nzuri ni ile inayoruhusu upinzani wenye nguvu, na wakabiliane nao bila kutumia hila, wala nguvu ya dola kuunyamazisha upinzani.

Kwa nini Rais wa Tanzania hasikiki duniani kwa lolote? Kila mtu anajua kwamba serikali ya nchi hiyo hutumia vyombo vya dola kuwanyamazisha wapinzani. Hata kama wangeenda mwezini kwa miguu, bado dunia itawadharau serikali ya Tanzania kwani wanajua mbinu wanazotumia kubaki madarakani. Katika hilo la kumuonya Kibaki asiufuate mkondo wa watu kama kina Kikwete tunawapongeza Nation. Pia walimchokonoa Paul Kagame wa Rwanda na kumuusisha moja kwa moja na mauaji ya halaiki ya Rwanda.Pamoja naye pia walimlaumu Yoweri Museveni wa Uganda kwamba alihusika kwa njia moja ua nyingine katika kumsaidia Kagame aiangushe ndege iliyokuwa imembeba rais wa Rwanda wakati huo, na kusababisha mauaji ya halaiki. Katika hilo pia Nation mpya wana pongezi zetu. Isitoshe katika toleo hilo, walimsakama baba mtakatifu na kanisa Katoliki kwa kuwanyima uhuru makasisi waliolemewa na tamaa ya wanawake waoe na waendelee kuwa makasisi wa kanisa hilo. Walimnukuu askofu Emmanuel Milingo akisema kwamba atawatawaza makasisi waliooa wawe wahudumu katika kanisa hilo la kikatoliki ambalo makasisi wake hujifanya hawaoi, huku wakiongoza katika ufuksa, hususan wa kufanya mapenzi kwa watu wa jinsia moja. Kama hayo ndiyo mabadiliko waliyomaanisha Nation, basi tunawapa mkono wa kheri na kuwaombea wasibadili msimamo huo. Lakini wana kazi kubwa kutuhakikishia kwamba wamejikomboa kutoka mikono michafu ya serikali iliyotaka kuwageuza kama wapiga debe wa serikali.



Nation ilianzishwa mwaka 1954 na tajiri wa kihindi Bwana AGHA KAN. Magazeti hayachaguliwi kama wabunga na Rais, kwa hiyo ni vigumu kujua lini Nation watangatuka madarakani wayaachie magazeti mapya yaje na mitizamo mipya. Kanu iliikuta Nation na imetolewa, na bado hawa jamaa wanaendelea kujibadilisha ngozi kama nyoka. Kama ilivyo kwa wanasiasa, Gazeti likilewa madaraka hufikia hatua ya kuamua nani awe nini na kwa muda gani.Tunaomba Mungu Nation isiwe inaelekea hapo. Lakini wenyewe wanajiona hapo. Ndio maana utawasikia wakisema wanatafuta wasanii wapya, wanasiasa wapya, lakini siyo magazeti mapya. Wakati sasa umefika wa sheria kuundwa ili kipindi cha magazeti kisizidi miaka 10 na tena yale yanayochapisha yawe yamechaguliwa na wananchi. Yaani uchuguzi mkuu pia uvihusishe vyombo vya habari. Unafikiri kama siyo kura, lini kina BBC na CNN, na sasa NATION watatoka madarakani? Vyombo kama GTV haturuhusiwi kukua nasi tutoe maoni tofauti na hawa wanaojiona wanahabari wa maisha. Nation wana TV yao ambayo wimbo ambao hawakuurekodi wao lakini una alama ya GTV hawauonyeshi. Kisa hawatambui chombo kingine cha habari.Tunapoimba kuhusu demokrasia, lazima tuelekeze macho yetu kwa vyombo vya habari ambavyo vimetawala kwa muda mrefu wa kutosha. Vitoke viwaachie nafasi wanamapinduzi wenye mawazo mapya. Magazeti kama UHURU na MZALENDO ya Tanzania, hayapaswi kuwepo kwenye ulimwengu wa sasa. Lakini kwa sababu yanamilikiwa na Serikali mbovu ya CCM, basi yanaendelea kuudanganya umma wa Tanzania kwa propaganda zinazoitwa habari. Serikali yenye siasa mbaya ya ujamaa na kujitegemea inapomiliki vyombo vya habari Tanzania, utatarajia siku moja kusikia kutoka vyombo hivyo kwamba siasa hiyo ya kujitegemea kiumasikini ilishindwa? Ndio maana kuna haja ya kuvipigia kura vyombo vya habari. Na hapo ni kama havitatumia mbinu chafu wanazotumia CCM kubaki madarakani hata leo. Lakini nafasi itakuwa imetolewa kwa vyombo vipya vya habari kuingia uwanjani. Kama kuna uwanja mgumu kuingia na kucheza duniani, ni uwanja wa vyombo vya habari. Lakini tunashukuru teknolojia kwani hata haya ninayoyaandika usingeweza kuyasoma kama siyo mtandao wa Internet. na huku pia kuna majabali kama kina GOOGLE na YAHOO ambao nao wanajiita wababe wa mtandao.Uzuri wao hawa wa hapa wanaruhusu wengine waonekane hata kwenye sachi injini zao. Nina maana ukichapisha www.gospelgtv.com na uwaambie GOOGLE au Yahoo wakutafutie iko wapi, watakuletea bila wivu.Nation hawawezi fanya hivyo. Wanajifikiria wenyewe kwanza kabla ya wengine. Wanataka kila mtu angatuke au kustaafu, lakini siyo wao.

Nation Lageuka kuwa Gazeti la chama na serikali
Hatutegemei kazi ya gazeti iwe ni kuipinga serikali tu, Sambamba na hilo hatutegemei gazeti liwe linaimba sifa za serikali hata pale serikali inapokosea. Nation wanafanya hivyo bila haya. Tangu serikali mpya waingie madarakani gazeti la Nation limekuwa likiyafumbia macho makosa yao, huku wenzao Standard wakiwa mstari wa mbele kuyakemea. Baada ya Nation kuisoma "Stori" hii, Kiranja wao Wilfred Kiboro alikasirishwa sana. Haraka aliamuru sera za gazeti hilo zibadilishwe na kuanza kuikemea serikali. Sasa kama hawaikemei serikali kwa sera mbovu za usafiri, Kiboro mwenyewe anakuwa habari, kama siyo habari kuwa Kiboro. Walianza na Kibaki mwenyewe pale waliporipoti kwamba aliporomoka kwenye ngazi za Ikulu na kutonesha majeraha ambayo tayari alikuwa nayo. Serikali iliwapuuza kwani ilikuwa na kazi ya kuwanyamazisha Standard waliokuwa wamezidi na kelele zao. Ni ukweli usiopingika kwamba Nation ya Kiboro inaboronga na inaporomoka, huku Standard wakijigamba kwamba wameshika usukani. Sijui kama wasomaji watarudisha imani yao kwa Nation tena. Tunasubiri tuone. Serikali ni kama inafanikiwa. Kwani Standard nao wanaonekana kwamba mdomo waliokuwa wakiupanua sana kupiga kelele, umewekwa kitu, na sasa sauti haitoki sawasawa. Kwamba wanaopinga ndio wanaozawadiwa, inaonekana kuwaumiza Nation na CITIZEN. Sasa wameanza kupinga. Lakini wakiwa wamechelewa. Nani aliwadanganya wanasiasa watakumbuka fadhila? Wanajidai kuwasaidia Kana kwamba wanajitetea, Nation waliandika kuhusu mhariri wa gazeti hili na kujaribu kuichambua web site hii. Lengo ni kuonyesha kwamba mkuki kwa Nguruwe ni sawa, lakini kwao ni wa uchungu. Habari zaidi

Rev.Wachira asema magazeti yanapaswa kuikosoa serikali, kwani hata kama serikali ingeundwa na malaika, bado inahitaji chombo cha kuikosoa isiende mrama. Ni makosa kufikiri kwamba serikali mpya haijafanya makosa. Kwangu tayari wamefanya makosa mengi kwa mwaka mmoja madarakani. Mwaka wa pili utakuwa kuvunja rekodi ya makosa yaliyofanywa na serikali za awali.Tusubiri hadi wavunje rekodi ndipo tuikosoe?




Mfano gazeti la Nation, Limeacha sera zake za karibuni za kuisifu serikali ya Kibaki, na sasa wameanza kumshambulia Munishi.


How politics derailed
the Munishi gospel crusade

By DAN TENG’O
He came, he saw and conquered the local gospel music scene. But not any more. The lustre that Faustin Munishi had in the 80s when he took the local gospel music scene by storm seems to have faded out.

The once-famous artiste, who popularised solo gospel music in the early 1980s when the genre was dominated by choirs, is no longer enthralling fans with hypnotic vocals and idiomatic Kiswahili rich in imagery and symbolism as he used to.

Since 2000, when the Tanzanian Government banned the evangelist’s seventh gospel cassette titled, Mpende Adui (Love the Enemy) owing to its political views, nothing has been heard of him, at least musically speaking.  

Instead, the Arusha-born Munishi has remained steeped in political activism for the past few years and has now decided to fight for his cause via his website.

Munishi, who is credited for rocking the local gospel music scene with seven delightful music albums, has vowed to censure Tanzania’s ruling party, Chama cha Mapinduzi (CCM), until its downfall, of which he seems sure.

On his website, which is full of his family pictures, Munishi claims that he has been "anointed by God" to free Tanzanians from the country’s ruling party. To hammer the point home, Munishi attacks the party with acid lyrics of the opening track for the album Mpende Adui.

In true vitriolic fashion, Munishi’s website has a link entitled "Wasikilize waongo!" (Listen to the liars! which, upon clicking, directs one into the Tanzanian National Website.

He takes a swipe at President Benjamin Mkapa’s government, accusing it not only of misruling Tanzania, but also of human rights abuses. He cites himself as an example of a gagged citizen, saying copies of Mpende Adui were confiscated by police for allegedly disparaging the Mkapa government.

"Tanzania is for all its citizens and not Mkapa’s or CCM’s as it seems to be," he trumpets in his website, adding that Mkapa claims to know everything that is good for Tanzania yet the opposite is true.

On the website, he hits at the US virulently, much as he did in the song titled Msiabudu America (Don’t worship the US), featured in his controversial seventh album. In the song, he accuses the US of denying people visas unnecessarily.

Also on the receiving end of Munishi’s attacks are journalists and local media houses with the exception of KBC (Kenya Broadcasting Corporation), which helped to boost his musical career back in the mid-eighties and BBC which granted him a full interview during his tug-of-war with the Government of Tanzania, which he confesses to hate.

He rails at radio stations for being overly commercial. "Their aim is not to inform or entertain. They are out to broadcast commercials. They use commercial means to target believers, thus injuring their faiths. Their programmes gloss over matters to do with faith," he says.  

Before finding a vocation in music, Munishi, 44, worked as a painter in Arusha. In 1980, he acquired an accordion and started to sing old Sunday school themes such as Niko Chini ya Mwamba which became a number one single in Kenya.

Munishi became a born-again Christian that year and joined Tanzania’s Bishop Mosses Kulola’s entourage as a singer before ditching the old preacher for a solo music career in Nairobi.

His debut album registered mild success. The second, Niko Chini ya Mwamba, however, put the singer into big business. In 1989, he went back to Arusha and married Ms Prisca, with whom they sang a duet in the opening track for the third album "Yesu na Wewe" (Jesus and you).

From then, the wife never sang in public again, thus causing the wide speculation that she had actually ditched the singer.

In 1993, Munishi made another trip to Arusha (in a sleek white Mercedes Benz) to refute the allegations and did it at an open-air crusade, where the alleged estranged wife accompanied him in a musical number, just to prove that she was still around.

Munishi is blessed with three children, the oldest being Mojashi, who immediately after being born, joined the father's singing group in Nairobi by the name "Mojashi Choir".

The choir collapsed later and so did Munishi’s own newspaper, Injili, whose first and only copy came out in 1996.

Most of the newspaper material has been repackaged in his website which, like the print version, is full of Munishi’s various profiles in the positive and his "enemies" in the negative.


Munishi Bado nahubiri Injili

Nashukuru kwamba wengi wameanza kunielewa. Lakini kuna wale ambao bado kwa makusudi hawataki kuelewa kwamba Munishi mimi sijaacha kuihubiri injili. Ila wanakataa ukweli kwamba Injili ni maisha na sijui wapi utajenga ukuta useme injili inaishia hapa na siasa inaanzia hapa. Katika hilo tukubaliane kutokukubaliana.

Kwangu kuikemea CCM na serikali mbovu ya Mkapa, ndiyo Injili yenyewe hiyo. Injili inakataa maovu ya kila aina. CCM aliyoanzisha Nyerere ni baba wa maovu Tanzania. Ndiyo maana kwangu ni sawa na JEHANAMU Tanzania.

Sasa magazeti yameanza kunishambulia eti nimejaribu kusema nitakuwa Rais wa nne Tanzania. Kuna ajabu gani mimi kuwa Rais? Nina kila kinachohitajika kuwa Rais wa Tanzania.

Vyombo vya habari vijue hivyo na viache kunisakama.


Vs

NTV Wavuta viatu badala ya Soksi

By Pastor Munishi


Je Kenya wata "Swich Off" NTV au Itawa "Turn On"?
Kuboresha NTV Haimaanishi kupora watangazaji kutoka KTN. Badala yake inaonyesha uvivu wa kutengeneza watangazaji wenu, au kuwatafuta wapya.
Baada ya kurupushani na Lucy, sasa Nation wanaonekana kushika adabu. TV yao wanasema itatuwasha badala ya sisi kuiwasha.Wengi wametafsiri hiyo kama ongezeko la vipindi vinavyohusiana na "ngono" Tayari wameanza kuonyesha nyimbo ambazo waimbaji na wachezaji wako nusu uchi kama siyo uchi kabisa. Ikiwa walimaanisha kuiwasha jamii kwa jinsi hiyo, basi wamekosea. Tunatakiwa kulaani vipindi vya ngono kwenye TV. Na Nation wajue hivyo.


Kila la Kheri NTV
Tunapokaribisha mabadiliko NTV, matarajio ya wengi yalikuwa kuona ubora wa vipindi NTV wanavyoweza kutayarisha, na siyo kuvua watangazaji kutoka stesheni nyingine wakitumia ndoano ya pesa. Ubunifu na kuandaa vipindi vingi kwangu huo ndio ubora wa stesheni. Pesa siyo kila kitu. Ni kweli NATION wana kila kifaa ambacho pesa zinaweza kununua. Lakini vifaa bila watu wabunifu ni bure. Wasishangae mtu mbunifu mwenye KAMERA moja akafanya vitu vikawastaajabisha. Haijalishi kipindi kimeandaliwa na watu wangapi, au na vyombo vya bei gani, kama kipindi ni kibaya ni kibaya. Kuandaliwa NTV kwenye vyombo vya bei mbaya hakukifanyi kipindi kuwa bora kama hakuna ubunifu wa kutosha
.
"LOGO"ya NTV Inatia kichefuchefu

Baada ya kuwaza na kuwazua, Nation waliona waje "LOGO" Mpya.
Nation TV walichofanya ni kubadili "LOGO" lakini mtindo na mbinu bado ni ule ule. Tena wengi wanasema sasa ndio wameharibu zaidi. Kama ulikuwa umezoea kupika maharage kwenye chungu cha kawaida yakaiva na kuliwa, Ukinunua sufuria ya bei ya juu na bado upike maharage, walaji hatutaona tofauti. Ndivyo NTV walivyofanya. Kwanza aliyebuni hiyo "LOGO" hakutumia usanii hata kidogo.Alichofanya ni kuiangalia "LOGO" ya CNN na kujaribu kuiiga. Matokeo, alitengeneza kitu ambacho macho yetu yalishakiona CNN. Ndiyo maana macho yanakataa kuamini kwamba NTV wana "LOGO"Mpya. Fanyeni kiungwana. Rudini tena mezani, mchore upya. Huwezi kuja na kitu kipya ambacho kimeshindwa ubora na kile cha zamani.

Wafanyikazi NTV wamekosa motisha.
Mtindo wa NTV kuwanunua wafanyikazi kutoka stesheni nyingine hasa KTN, unawafanya wale walioanza NTV kujiona hawafai kitu. Akija Emmanuel Juma kutoka alikotoka, anapandishwa cheo huku wakongwe wa NTV wanabaki midomo wazi kwa mshangao. Akija Nimro Taabu kutoka taabuni, naye mara moja anawekwa kusoma habari huku kina Shabani Ndege wakinyimwa nafasi ya kujiendeleza.

Kosa kubwa walilolifanya ni kumpa huyu Mwarabu toka KTN nafasi ya kusoma habari badala ya Mukami ambaye anatawala "SCREEN" vilivyo. Mukami sijui nimwite dada Mukami au Bi Mukami. Lakini tayari alikuwa ameshapanda chati na kuwa kati ya watangazaji wazuri Kenya. Mwenyewe akisoma Habari utadhani Natio TV ni mali yake.

Hesabu NTV zinawachanganya pale walipomtoa Jamilla Mbogua na badala yake wakamweka Bi Mohammed. Sina tatizo la udini, na pia sikubaliani na Jamilla pale alipokuwa ameanza kuzidisha mapambo. Lakini ilikuwa ni kiasi cha kuambiwa apunguze kujiremba kupita kiasi. Lakini kwa usanii wa kusoma habari pamoja na kuweka madoido, hakuna mwenzake. Akikalia kiti na aangalie camera, halafu aanze kuzungumza, Utadhani Nation TV ni ya Mbugua baba yake. Hata kama angetoka nyumbani bila kunawa uso na asome habari bado watu watamsikia. Jamilla ujue hivyo. Naye Sophy Ikenye anakosa nafasi uwanjani kwani wachezaji wa kulipwa ndio wanaopangwa uwanjani hata kama chenga zinawashinda. Wafanyikazi wengi wanasema hiyo siyo sawa. Huwezi kuja utukute, halafu uwe Boss wetu. Sisi ndio tunaotakiwa tukuonyesha mambo hapa hufanywa vipi. Ila NTV wanafanya kinyume chake.


NTV ni Walafi
Kifupi niseme NTV wamevimbiwa. Ulafi wa watangazaji umewafanya wale kupita kiasi na sasa WAMEVIMBIWA. Matokeo wengi watakuwa "WASTE". Sio ajabu, kwani sera za Nation ni kununua kila mtangazaji KTN wakifikiri kufanya hivyo kutaiporomosha KTN. Walidanganyika. Sasa wameonyesha kila mtu kwamba KTN ilikuwa inawakosesha usingizi. Wengi wanasema kama mmewachukua, basi wafanyeni bora kuliko walivyokuwa. Kinyume cha hayo NTV itaonekana kana kwamba nia yao ni kuharibu vipawa vya watangazaji wanaonunuliwa. Unaulizwa wewe ni bei gani, ukisema, unanunuliwa ili uharibiwe uwe "WESTE" Hata watangazaji wanaohama kila kukicha, na wenyewe wana kasoro ya Tamaa. Wanataka huku na huku, mwisho watakosa kote.


Maringo NTV Hayatawasaidia

Bennie Mack Ambaye TV nyingi Afrika hununua maonyesho yake kwa mamilioni ya dola.
Nani alisema kwamba vipindi vizuri lazima vitoke Marekani? Kwamba Nairobi wameanza kutengeneza mikanda ya video hizo ni habari njema. Inashangaza kuona kwamba TV Stesheni nyingi hazijapokea habari hizo kwa furaha inayozistahili. Hakuna hata stesheni moja iliyoanza kununua video hizo na kuanza kuzionyesha. Kwao, kwenda Marekani kununua maigizo ambayo hayaendi sambamba na tamaduni zetu ni rahisi, kuliko kuteremka River Road na kununua maigizo ambayo wengi tunaweza kujihusisha nayo. Wanadai ubora wa picha ni duni. Kila kitu lazima kianzie mahali.Ikiwa wale wanaojiita waandishi wa habari hawajaweza kuzalisha igizo lolote, siyo ajabu soko la video za nyimbo za Injili likaanzia River Road. Majumba ya TV yameze kiburi na wafanye kile ambacho kila mtu alikusudia wafanye. Debe tunalolisikia Nation lilenge kununua kazi za wasanii humu nchini na kuzionyesha. NTV waache maringo na waanze kuonyesha maigizo na nyimbo zinazotengenezwa na wasanii humu nchini. Kiwango cha ubora kisiwasumbue bali waangalie sanaa iliyotumika. Hata HOLLYHOOD haikuanza na ubora walio nao. Lini waafrika watajifunza kujivunia chao? Leo hii ukipeleka nyimbo yako NTV na wajue ilitengenezewa River Road wanaidharau na kuitupa kapuni. Lazima muwape moyo wasanii wa humu nchini ili kazi zao ziweze kufikia ubora wa kina OPRAH. Haiingii akilini kuona stesheni inatumia mabilioni ya shilingi kuagiza vipindi kutoka nje wakati wasanii wa humu nchini wanawapelekea kazi zao wazionyeshe bure bila malipo lakini wanawapuuza. Badala yake waliopaswa kulipwa ndio wanaolipa ili kazi zao zionyeshwe kwenye NTV.

Ikiwa mabadiliko yalimaanisha ongezeko la vipindi vya ngono kutoka Marekani basi NTV wamepotea lengo.

Hiyo ni AIBU kubwa. Ni matumaini yetu kwamba mabadiliko NTV yatalenga kuinua wasanii wetu. Kinyume chake ni kuendeleza utumwa wa kimawazo ambao vyombo vya habari Afrika vimekuwa vikiukumbatia kwa muda mrefu. Mtasemaje kuhusu vyombo vya habari Afrika kujaza kazi za wasanii wa nchi za magharibi? Huo ni Utumwa wa kimawazo. NTV Onyesheni mnamaanisha mnaposema mna mipango ya kuboresha stesheni yenu.

NTV wavuta Viatu badala ya Soksi

Anaitwa Sophy Ikenye
Je Kenya wata "Swich Off" NTV au Itawa "Turn On"?
Kama kuna jambo linalowakera wakuu wa NTV, ni pale wanapomweka mtu kusoma habari na mtu huyo anajulikana kuliko wao. Nasikia hilo ndilo linalowafanya wabadilishwe kila kukicha. Wengi tunaliona hilo kama usumbufu. Kama wanataka, na wao waingie uwanjani. Tunasubiri NTV Jioni itakayoletwa na Bwana Kiboro.
Nation Kenya ni Kiboro japo mmiliki ni Agha Khan

Bwana Wilfred Kiboro akiwa na Agha Khan Mmiliki wa Nation Media.
Nation ilianzishwa mwaka 1960 na Shehe wa dini ya Kiislam Bwana Agha Khan. Kinyume na KTN iliyoanzishwa mwaka 1989 na wafanyibiashara Wakenya. Kinachowashangaza wengi ni Nation kununua watangazaji kutoka KTN badala ya kinyume chake. Hatujali nani ananunua nani, Lakini kufanya hiivyo kuzuia upinzani ni kosa. Haki ya Nation kuboresha NTV siyo lazima izime zile TV nyingine. Ubora wa NTV utapimwa na KTN yenye nguvu. Kutumia pesa kuwamaliza wapinzani kama GTV hakutaifanya NTV bora. Badala yake NTV itakuwa dikteta wa habari. Uhuru wa vyombo vya habari utatoka wapi wakati vyenyewe vinanyimana uhuru? NTV inapodai uhuru wao kuhabarisha, huku ikiwanunua wanahabari kutoka KTN na zile stesheni nyingine (Lakini siyo GTV), Huo ni unafiki unaotakiwa kukemewa kwa nguvu zote. NTV wanatakiwa wajue kwamba pesa siyo kila kitu. Kiboro anaweza kucheka mpaka jino la mwisho leo, Lakini kama siyo AGHA KHAN Nguzo kuu ya Nation Mwenyewe angeanzisha "KIBORO TIMES" ingefika wapi?

Bwana Joseph Muliro Akijibu hoja kwa niaba ya NTV, Alisema:
"
Hellow sir Well thanks for your comment but I would beg to disagree with you, both Nation TV and radio started in 1998, while KTN atrted in 1991, The Nation News paper started in 1968, while standard news paper started in 1902. secondly NTV is the only station that shows african movies like wingu la moto, another one is UHONDO, while KTN doent have even a single African movies, thirdly when it comes to christin music, Nation TV is the leading station when it comes at playing gospel songs and we have a programme called the storm every saterday.coming to the issue of presenters, Nation has never approached any KTN presenter in the name of giving him/her more money, we normally run those job vacancies in the news paper, and any body is free to apply, on the contrary KTN took most of our presenters, watch Nation and watch KTN and you will come to right conclution, good day sir."

Ni maoni yake kama alivyoandika mwenyewe. Gazeti la Injili hatukuhariri chochote.
Je! Una maoni Gani? Tuandikie kwenye fomu mwisho wa ukurasa huu.

MAURICE MUNENE MUGAMBI. mrcmunene@hotmail.com Asema:
UKWELI MTUPU KUHUSU NTV.
Naunga mkono maoni yako, kuhusu hulka mbaya ya mabwanyenye wa Nation,kuwawinda wasomaji habari kutaka KTN.Hatuijaona 'any added value'baada ya wao kuwachukua. I also ask,who says Munish cant rule Tanzania?These prophets of doom will be proven wrong soon for God is surely lifting you from one level of glory to another.God gives mandate. Unlike many Kenyan polictian rebels,without a cause,you surely stand out as visionary leader for your country. However;i believe your true patriosm can be demonstrated better if you opted to fight from within and not without.Am afraid History may judge you rather hashly because you aren't alone in this battle-Your brothers from within,Tanzania,are taking the bull by the its horns through an organised political vehicle.Though they are various of them ,i strongly believe you should board one and further the common cause in an unified voice.What's your take on this ndugu Munishi? Otherwise you are a true son of Africa.You should fire from all angles and don't spare your host Kenya too.We need to hear your thoughts about the powers that be in Kenya.You are hero at home and heros are saluted everywhere not because they are always right but because they are always principled. I would love to hear from you.

Nation TV Wakosa Mwelekeo

 

Waliingia kwenye uwanja wa TV Nairobi kwa vishindo. Na matangazo mengi kwenye gazeti lao "DALY NATION" yaliwafanya wapinzani wao wakubwa KTN kuonekana kama simba aliyenyeshewa. Wananchi walisubiri kwa hamu kuona uwanja wa TV Kenya ukibadilishwa na magwiji wa habari Afrika Mashariki na kati. Baada ya kuanza na kasoro nyingi, wananchi waliendelea kusubiri kwani wengi walisema mwanzo wa kila kitu ni mgumu. Roho za watu wengi zilipoa kidogo wakati NATION TV walipoanzisha kipindi kilichowaonyesha viongozi wa Kenya kuwa ni kichekesho kitupu. Kipindi hicho kilijulikana kama REYDICULAS "Mnisamehe kama sikuandika vizuri jina hilo." Hii ni kwa sababu binafsi sikuwahi kukiona kipindi hicho japo watu wengi walionekana kukisifu na kukipenda sana. Pengine hamu ya kuona watu weusi kwenye TV zetu ilichangia kuwafanya watu washabikie kipindi hicho.

Matumaini hayo yaliendelea kufifia kila kila siku baada ya NATION TV kufuata mkondo ule ule ambao TV za awali ziliufuata. Vipindi vingi vilikuwa vya nchi za magharibi, Habari pamoja na usomaji wake haukuwasisimua wengi, kwani badala ya NATION TV kuwatumia wakongwe wake wa habari katika magazeti yao, waliaza na watu wapya jambo ambalo mpaka sasa sijui nani aliyefanya maamuzi hayo yasiyo ya busara hata kidogo.

Kila tunachokiona kwenye TV ni kazi ya uandishi halafu ikapatiwa sauti na picha. Kwa NATION hawakuhitaji waandishi wapya wa TV, bali walihitaji wasomaji wa yale ambayo tayari yameandikwa na waandishi wao waliobobea katika fani hiyo. Kwa maneno mengine walihitaji KAMERA nzuri na studio ya kisasa kuweza kuwa na vipindi vya kutosha masaa 24 kila siku kwa muda wa miaka ishirini. Cha ajabu ni kwamba pamoja na kuwa na studio ya kisasa kama hii inayoonekana hapa, bado NATION TV haina vipindi vya kutosha masaa sita kwa siku.



Studio ya kisasa NATION TV, Ila vipindi ni kiwango cha chini sana.

Akiongea na Gazeti la Injili, aliyekuwa mhariri wa gazeti la NATION Bwana Ogova Ondego ambaye sasa analifanyia shirika la habari la Kenya KBC alisema alijiondoa NATION baada ya kuona kuwa hawataki kuitumia taaluma yake vizuri. "Niliwaambia nianzishe kipindi cha TV ambacho kitatumia makala zangu ninazoliandikia gazeti la NATION lakini wakubwa walikataa." "Walisema siwezi kulipwa na gazeti halafu tena nilipwe na TV." Alimaliza Ogova ambaye mbali na kuifanyia KBC, ameanzisha WebSite yake inayohusiana na mambo ya sanaa na inapatikana katika http://artmatters.netfirms.com

Inawezekana kuwa uongozi wa NATION ulikuwa sawa kumzuia Ogova kupata mishahara miwili, lakini ikiwa hakuna mtu mwenye uzoevu kama wa Ogova kuandika makala za TV sioni kwa nini wamkataze. Lakini kuna minongono NATION kuwa Mkurugenzi wa shirika hilo la habari Bwana Kiboro anataka mwenyewe awe ndiyo habari. Tena wako wanaosema kuwa hata wale wanaoajiriwa kushika nyathifa mbali-mbali katika shirika hilo, huchaguliwa kwa misingi ya undugu au ukabila na siyo uwezo wa mtu kitaaluma. Katika enzi hizi za mtandao wa Internet itakuwa vigumu kwa NATION kuwazuia waandishi wake kupata zaidi ya mishahara miwili kwani kila mwandishi anaweza akawa na WebSite yake na kuandika "story" zake hapo na kuziuza kwenye chombo chochote cha habari ulimwenguni.

Ogova amefungua mlango kwa waandishi kuwa huru, sijui wengine wanasemaje. Waandishi wengi huwa msitari wa mbele kutetea wanaoonewa katika jamii, lakini hakuna wa kuwatetea wakati vyombo vya habari vinapowaonea na kuwanyanyasa waandishi. Kwa mwandishi yeyote anayetaka kuanzisha WebSite, niko tayari kusaidia.

Ameandika Munishi Faustin

 


Huyu ni Bwana Lui Otieno KTN. Anasema yeyote anayetaka kuujua ubaya wa NTV awasiliane naye kwa simu. Alikuwa huko yakamfika shingoni akatoka. Anawajua NMG ndani na nje. Kwa sababu NTV wamesema, yeye atasema akiulizwa kufanya hivyo. Nanyi waomaji wa GTV On line, Msiandikie mate wakati wino uko. Nambari ya simu hiyo hapo. Kwa wale walio nje ya Kenya itawabidi watangulize nambari ya kimataifa +254 kisha ufuatishe nambari zinazofuata. Wasomaji, Lui Otieno huyu hapa. Muulizeni yanayowakera moyoni. Wengine wamekuwa wakiuliza kama ameoa au la. GTV hatuna majibu, Lakini Lui mwenyewe atawajibu.

KBC wasema wao ni "JUNGU KUU HALIKOSI UKOKO"

KBC walipowaona NTV wanavuta viatu na havivutiki, wao waliamua kuvuta soksi zao. Walikuja na mbinu mpya ya "Jungu kuu halikosi ukoko." Walienda kwenye Maktaba yao na kuchukua maigizo na filamu za zamani na kuziita zilizopendwa. Sasa watazamaji wanaonyeshwa zilizopendwa. Hiyo tu imewapa NTV kibarua kigumu. Sasa watazamaji waliokuwa wawekwe sawa na NTV, wanazunguka kila mahali mradi wapate kipindi kizuri. Mawazo ya NTV kwamba watazamaji wangeikodolea macho NTV pekee, yamegonga mawe. Labda warudi tena mezani kuchora upya. Kijisanduku kwa jina TV kimepata sura mpya baada ya utitiri wa vituo vinavyoitwa vya TV kuanza kurusha matangazo bandia. Sasa mtazamaji ana uhuru wa wa kutotizama zote, na kujitengenezea utaratibu wake wa nini aone na kwa wakati gani. Shukrani kwa vifaa vya kuchezea VCD. Wengi siku hizi wanajinunulia VCD zenye nyimbo za Injili kutoka wasanii tofauti na kuanza kujipangia utaratibu wa vipindi vya kuona kinyume na ilivyokuwa mwanzo, Eti wangoje kuwekewa vipindi na NTV wakati wao wenyewe ni TV stesheni. Wamegundua kwamba NTV na zile nyingine wanachofanya ni kuweka mikanda ya nyimbo na filamu kwenye chombo kama VCD Player au Video Player. Tofauti ni kwamba mitambo ya kurushia matangazo hupeperusha hewani kilichowekwa na kukiingiza kwenye nyumba za watu kupitia erial zilizotundikwa juu ya mapaa ya nyumba. Wengi wanasema indapo TV hazitabadili mtindo, basi itawalazimu kuondoa vifaa hivyo juu ya nyumba na kutegemea vipindi wanavyojipangia wenyewe nyumbani mwao.

CITIZEN nao sasa wameamka. Wameboresha mitambo ya kurushia matangazo.


CITIZEN nao sasa wameamka. Wameboresha mitambo ya kurushia matangazo. Wanapatikana kiurahisi hata kama eria imeelekezwa popote. Wamegundua kwamba walio wengi hawasumbuki kurekebisha erio zao. Ile TV inayopatikana ndiyo inayoangaliwa. Ukiangalia juu ya mapaa ya nyumba za watu Afrika, utagundua kwamba chombo kinachopaswa kunasa matangazo ya TV kimewekwa kiholela sana kiasi kwamba kama huna mitambo ya nguvu na iwe kila mahali ni vigumu TV yako kuonekana. Watu wengi hawako tayari kuwalipa wanataaluma wawawekee erio kiutaalamu. Ndio maana utaziona zimeelekezwa popote na mara nyingi huwa hazilengi mitambo yeyote. Siyo ajabu kukuta mtu yuko karibu sana na mitambo ya kurushia matangazo ya TV na bado TV yake inaona mchele badala ya picha. CITICEN wamegundua hilo, lakini bado wanahitaji kuvuta soksi zaidi. Wanadai wanasikika na kuonekana Arusha na Uganda. Lakini GTV ilipowasiliana na Arusha walisema hawajaiona CITIZEN huko. Ila katika kuifanya TV yao kuonekana ya Afrika tena Kenya, CITIZEN wanaongoza kwa hilo.

Je TV zinazojiita za Injili ni bora kuliko zile nyingine?
Nazo TV zinazojiita za Injili hazitofautiani sana na zile za kidunia. Gharama za kutangaza mikutano ya Injili ni juu kuliko kawaida. Zimejibandika majina kama Family Media lakini ni TBN. Ukidanganyika ufikiri ni TV ya humu nchini inayojali maslahi ya wahubiri wa humu nchini, Hutayaamini masikio yako pale utakapoambiwa ulipe kwa DOLARI za Kimarekani ndipo uweze kuonekana hapo. Cha ajabu bado wanachangisha pesa kuwawezesha kurusha matangazo yao nchi nzima. Kwao Waafrika ni watu wa kuhubiriwa tu na wahubiri kutoka Marekani. Kwamba TBN wanadhamini Family Media na vipindi vyao ndivyo vinavyopewa kipau mbele, huo ni ukweli usiopingika. Lakini kutulipisha pesa wahubiri Waafrika ndipo tuweze kuonekana hapo, na kisha kutuchangisha ili kuisaidia TV iliyokwisha changiwa kutoka Marekani, ni sawa na kutuibia mchana. Wahubiri imewabidi wawe matapeli kuweza kupata pesa za kulipia TV zinazojiita za Injili. Wengine imewabidi kutengeneza miujiza ya uongo ili watazamaji washawishike kuwapa pesa ambazo nao huzipeleka mifukoni mwa Family Media TBN. Tunapowalaumu wahubiri matapeli, tutakosea sana kutozilaumu TV zinazowafikisha katika hatua hiyo. Ziwe ni zile za kidunia, au zinazojiita za Injili, haziwezi kwepa lawama. Ni haki ya watazamaji kuhabarishwa na kuelimishwa, lakini vyombo vya habari vinapodhamini pesa kuliko watazamaji na wasikizaji wake, Hatari iko hapo. Pesa mbele Injili nyuma, ndilo changamoto yao. Wakristo walifarijika wakati TV nyingine ya kidini ilipoanza kurusha matangazo yake Nairobi. GODS TV chini ya kivuli cha SAYARE TV kutoka kule Eldoret, imeanza kufanya kile watazamaji walichokizoea kutoka Family. Yaani mahubiri kutoka kwa wahubiri wa Marekani. Wanadai kwamba minara ya kurushia matangazo imegharimiwa na GODS TV, na masharti ni lazima masaa kumi yawe ni yao GODS TV. Ni Masharti kama hayo ndiyo yanayotufikisha kusema kwamba inaonekana Waafrika hawajafikia wakati wa kuanzisha TV zao za Injili. Kama wamefikia basi waanzishe TV zile ambazo haziwekewi masharti yeyote na TV za Kimarekani. Tunausubiri wakati huo kwa hamu. Lakini kwa sasa lazima tuvumilie Family TV ikiwajenga kina TD JAKES na wengine kutoka Marekani, Ili siku watakapozuru Kenya wapokelewe kuliko Rais. Wakiondoka watuache tukigombania Dala kidogo walizotuachia. Tena sasa lazima tuikaribishe TV nyingine kutoka huko huko Marekani kwa jina la SAYARE. Nao watafanya kile kile Family na CITICEN wanachofanya. Kuwapatia masaa wakubwa waseme kwani wamesaidia kuweka mitambo ya kurushia matangazo. CITIZEN ukiwasikia wakitamba kwamba wao ni pale roho ya nchi inapodundia, Wanakingiwa kifua na VoA ya Marekani. Ukoloni huu wa kutawaliwa kwa kutumia vyombo vya habari utaisha lini? Nani atukomboe? Mungu atusaidie.

Bonyeza hapa usome zaidi



Nyerere Msingi aloujenga Tanzania haufai, Tuubomoe.
Ujamaa ulishindwa, kwani CCM alioanzisha Nyerere sasa imezeeka. Sera zake zimeiharibu nchi yetu Tanzania. Tunataka mapinduzi tuitoe CCM madarakani ili tusinyanyaswe tena. Tumeonewa vya kutosha. sasa basi. CCM hatuitaki, imetufika shingoni. Tutaitapika.Mungu bariki Watanzania, wape hekima ya kutosha kuiweka CCM kapuni. Chukua usukani sasa kuiongoza Tanzania kwani kwa kipindi kirefu nchi yetu iliwekwa wakfu kwa shetani mpinzani wako. Tunamkataa shetani na CCM chama anachotumia kuwatesa watanzania, na tunaiweka nchi yetu mikononi mwako. Tumeomba machache hayo katika jina la Yesu Mwokozi wetu. Amen HABARI ZAIDI

Contact us/ Tuandikie

Full Name
E-mail
Subject
Message
   
   
 
biashara| http://munishi.com |