Ukurasa wa mbele
Gazeti la NYAKATI
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

Gazeti la INJILI
Kwenye Internet

http://www.munishi.com

Tel. 254722602445 E-mail:fmunishi@hotmail.com Or
munishifaustin@yahoo.com

Mchungaji Mwangi awasili USA

Rev. Moses Mwangi

Mchungaji Moses Mwangi amewasili Marekani akitokea Kenya kwa ziara ya miezi mitatu. Gazeti la Injili lilipomtafuta kwa simu nyumbani kwake Nakuru, Tulipewa habari za kuondoka kwake na kuwasili kwake USA.

Aliporudi Ajali Yakatiza Maisha yake
Zilibaki
kilomita tatu aingie nyumbani kwake. Yaliyotokea hayaelezeki, na hata yakisimuliwa inakuwa vigumu kuingia akilini. Baada ya safari ndefu ya maelfu ya kilomita kutoka marekani, ndege iliyombeba mwangi ilitua salama katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi. Mkewe ambaye alikuwa amekuja kumlaki alikuwepo uwanjani tayari kumkaribisha mumewe nyumbani. Ilikuwa furaha isiyo kifani kwa wapenzi hawa wawili kuungana tena baada ya kitambo kidogo.

Walikuwa na mengi ya kusema, lakini wakaona wayafupishe ili waanze safari ya kuelekea Nakuru. Barabara kutoka Nairobi hadi Nakuru siyo nzuri sana, lakini hata hivyo walikuwa wamepita sehemu zote mbaya. Kona kali, mashimo njiani karibu yote walikuwa wameyapita. Walipofika STEM HOTEL kilomita tatu kutoka Nakuru mjini, Ndipo mapepo ya kifo yalipojitokeza na kusababisha ajali iliyokatiza maisha ya Mchungaji Mwangi na mkewe. Kila mtu amesema lake kuhusiana na ajali hiyo, Lakini dereva ambaye mpaka sasa yuko mahututi ICU Hospitalini, ndiye anayeweza kutueleza nini hasa kilitokea siku hiyo.

Wengine wanasema kwamba gari nyingine iliingia barabara kuu kwa ghafla na kusababisha ajali hiyo mbaya. Iwe ilivyokuwa, Lakini Mchungaji Mwangi na mkewe sasa ni marehemu. Hapo ndipo kuna mtihani mgumu wa mawazo yangu kukubali hilo. Pengine ni kwa sababu wakati wa mazishi sikuweza kuhudhuria, ndiyo maana kwangu Mwangi bado yuko safarini na siku moja atarudi tuonane. Kidogo nafarijika nikiamini hivyo. Sijui mambo yakoje kwa wale waliutizama mwili wa mchungaji Mwangi pamoja na Mkewe kwa mara ya mwisho, na kuwaona wakiwekwa kaburini. Najua kwao majonzi ni mengi. Ndiyo maana nawapa pole jamaa na marafiki, na hasa watoto wa mchungaji. POLENI SANA.

Tumempoteza SHUJAA katika vita vya kupambana na shetani duniani. Najua kwamba Mwangi na mkewe watafufuliwa siku ya mwisho ili tumlaki Yesu mawinguni, Lakini nahuzunika kwa sababu KAZI duniani ni nyingi, na Mwangi bado tulimhitaji sana. Niyasemayo, washirika wa kanisa la DC Nakuru wanatakubaliana nami. Pamoja na kwamba Mark Kariuki ndiye aliyekuwa mchungaji wa kanisa hilo, Kazi nyingi kanisdani hapo zilifanywa na mchungaji Mwangi na mkewe. Kwamba cheo chake kilikuwa mchungaji msaidizi, hii haikumzuia Mwangi kuwa mchungaji MTEGEMEWA. Kadiri alivyozuiwa kuonekana kwenye kipindi cha TV cha kanisa hilo, ndivyo alivyosikika zaidi kanisani hapo.

Mwangi alikuwa mtu mmoja ambaye ukichimba shimo kubwa na kumfukia huko asionekane wala kusikika, uwepo wake shimoni ungesababisha ngurumo na tetemeko ambalo litawafanya mjue Mwangi yuko karibu. Sasa amezikwa kweli kaburini, na Nakuru ndio kwanza inaanza kuusikia uwepo wake. Umati uliomiminika kwenye mazishi yake, ni ishara kubwa kwamba Mwangi alikuwa na mguso tofauti katika maisha ya watu.



Pastor Mark Kariuki na Mchungaji Mwangi wa Maina ambaye sasa ni marehenu


Siyo nia yangu kuonyesha nani zaidi, Lakini Mark Kariuki pamoja na kuonekana kwenye TV kila kukicha, bado hataweza kufikia pale Mwangi alipokuwa japo kwenye TV alionekana tu alipokuwa akiunga mkono yaliyosema na Mark Kariuki. Mtu ambaye alikuwa na uwezo wa kuongoza kuliko BOSS wake, aligeuzwa kama shabiki aliyeonyeshwa tu pale anaposhangilia. SAWA. Sasa mwangi shabiki hayuko. Na kazi mliyomkataza kuifanya amewaachia muifanye bila woga kwamba Mwangi angewapindua.

Na kama watu waliohukumiwa na dhamira zao, Walijikomba kuonyesha ibada ya mazishi ya Mwangi kwenye TV badala ya kipindi cha siku hiyo. Mwangi ambaye hakuwahi kuonekana akihubiri kwenye kipindi hicho japo alikuwa mchungaji msaidizi wa Mark Kariuki, Alionekana akiwa marehemu mwili wake ukiwekwa kaburini. Aibu kubwa kwa Mark Kariuki na tena ilionyesha UNAFIKI WA HAL:I YA JUU.

Lakini machoni pa Mungu Mwangi ni SHUJAA aliyefanya kazi yake kwa uaminifu hata kama nafasi alikuwa akinyimwa. Nzuri zaidi ni kwamba watu pia waliliona hilo. Uwepo na sauti ya mwangi inasikika zaidi sasa kuliko alivyokuwa hai. Hilo ni fundisho kwa wale walio na wivu wa kuona kwamba mwenzao akionekana kwenye kipindi cha TV atangara kuliko wao. Kama Mungu amekupa huduma, huna sababu ya kuogopa huduma za wengine kwamba zitakuzima, labda iwe huduma yako ni bandia.

Mwangi na Mrs. laleni salama. Kazi yenu mmeimaliza, na sasa subirini TAJI. Wengine watasema kwamba wao ndio walioonekana zaidi kwenye TV, Lakini Bwana atawaambia ondokeni kwangu enyi watenda maovu msiopenda wengine wainuke kihuduma, na katika kujaribu kuwazuia wengine hata huduma zenu mnaziharibu.

Imeandikwa Na Faustin Munishi.

Bonyeza hapa kwa habari zaidi

 
| http://munishi.netfirms.com |