![]() |
![]() |
|
|
|
||
|
Gazeti
INJILI
Kwenye Internet
http://munishi.netfirms.com Tel. 254722602445 E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com MUGABE NA ZIMBABWE TUNAJIFUNZA NINI?
Mr. Mugabe na sera za Mashamba ZANU PF Chama kinachotawala Zimbabwe hakina tofauti na CCM inayotawala
Tanzania. Kwamba Mkapa amekuwa wa kwanza kumuunga mkono MUGABE hiyo
ilitarajiwa. Sera za ardhi alizotumia Mugabe siyo kwa manufaa ya wananchi
wa zimbabwe bali ni kwa ajili ya kulinda maslahi yake kisiasa. Inasemekana kuwa Mugabe ameshinda uchaguzi, lakini mimi nasema Afrika hakuna chaguzi zinazofanywa. Kama hazitaingiliwa na mataifa ya magharibi, basi vyama vinavyodai kupigania uhuru vitauza sera za kuwaadaa wananchi kwa malengo yao ya kuendelea kuwatawala.
Kiongozi wa UPINZANI Zimbabwe pia simuungi mkono kwani alionekana kama kibaraka wa kulinda maslahi ya mataifa ya mahgaribi na UINGEREZA ilikuwa ikiongoza katika hilo. Ni ukweli usiopingika kwamba Zimbabwe inahitaji mageuzi ya kweli, lakini watu wa kuleta mageuzi hayo ndiyo waliokosekana. Sambamba na Tanzania ambayo kama Zimbabwe inahitaji mageuzi ya kweli lakini watu wa kuyaleta mageuzi hayo ndiyo ambao walikuwa hawajapatikana.
Tunamshukuru Mungu kwamba ametukumbuka na kutupa kijana Faustin Munishi ambaye ataleta mageuzi ya kweli Tanzania na Afrika kwa ujumla. Sera za Munishi kukataa kuwa kibaraka wa nchi za magharibi ili asaidiwe kuingoa CCM madarakani ndizo zinazothibitisha kuwa huyu ni mwanamageuzi ya kweli. Kila mara Munishi hutufundisha kwamba huwezi kuwa mtumwa ili uwatoe watu utumwani. Ukifanya hivyo utakuwa umebadili watawala tu na siyo kwamba umeleta mageuzi .
Mwinjilisti Munishi: Nimepewa jukumu kuiongoza Tanzania Upinzani ungeshinda Zimbabwe bado wananchi wa Zimbabwe wasingeona mabadiliko katika maisha yao kwani wangetoka katika makucha ya chama tawala na MUGABE na kuingia kwenye makucha mengine ya ukoloni wa wazungu ambao ndio mbaya zaidi. Lakini je sasa wameepuka ukoloni wa nchi za magharibi Hasha hawajaepuka nasikitika kusema kwamba mambo sasa ni mabaya kuliko awali. Wanasiasa wamewadanganya wananchi kwamba wanafanya kitu kinachoitwa uchaguzi ili maisha yao yawe mazuri zaidi. Ni waongo. Wamepoteza muda wa WAZIMBABWE na kilichopatikana ni chuki zaidi kati ya wazungu na waafrika, chuki kati ya wanachama tofauti wa vyama vya kisiasa, na mbaya zaidi uchumi wa nchi yao umeharibiwa zaidi. Wazungu waliokuwa wakiunga mkono upinzani kwa kisingizio cha kutaka kuwasaidia wananchi wa Zimbabwe ndio watakaokuwa wa kwanza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi hiyo ili wananchi waendelee kuteseka.
Mugabe aliyewaahidi wananchi kwamba atawapa mashamba ya wazungu, sasa atajitahidi sana kurekebisha sera ili aondolewe vikwazo vya kusafiri alivyowekewa kwani utawala bila kwenda ulaya kuponda raha na kununua nguo za bei mbaya huo siyo utawala tena kulingana na mawazo finyu ya viongozi wengi wa kiafrika. Wananchi wataachwa na shida zao, na Mugabe na wazungu wake watarudiana kama mwanzo. Sitoshangaa kusikia wazungu walionyanganywa mashamba wakirudishiwa na kuruhusiwa kuwanyanganya wananchi wa Zimbabwe mashamba zaidi. Hiyo ndiyo siasa. Ndiyo maana mimi Munishi siwezi kuwa mwanasiasa. Nitawakomboa Watanzania bila siasa. Kwa Mungu yote yawezekana. Sitokubali kutumiwa na nchi za magharibi ili niwalindie maslahi yao Tanzania kama anavyofanya Mkapa. Angalia kila kitu Tanzania kimeuzwa. Hata wananchi wenyewe sasa wameuzwa. Yote hayo ni matunda ya msingi mbovu alioujenga Nyerere ambao nawaomba mnisaidie ili tuubomoe. WANANCHI nisaidieni kwa hili.
Munishi Akienda zake Nyumbani
|
||
|
Faustin
Munishi Tell. 25472602445 Nairobi Kenya East Africa
E-mail: fmunishi@hotmail.com | munishifaustin@yahoo.com You are Visitor Number since 14th February 2001 |
||