9 Next Page   
  Topic: CCM IMESHUSHA JEHANAMU TANZANIA, HOTUBA YA MCHUNGAJI KWA TAIFA < Next Oldest | Next Newest >  
Uwazi



Group: Members
Posts: 176
Joined: July 2003

Posted: Dec. 08 2003,08:06   

Mizambwa, Munishi

Hebu twendeni step by step, tusitake kukimbia wakati kusimama tu hatuanza.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano hairuhusu wagombea binafsi katika ngazi ya urais. Ndugu Munishi anasema kwamba yeye sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, that's fine.

Ninachoomba ndugu Munishi atufahamishe ni kwa vipi ataweza kugombea nafasi ya urais wakati hana chama?!

Make no mistake mimi ni mtu ninaye-support Independent candidate kwa nafasi zote i.e udiwani, ubunge hadi Urais. Lakini inavyoonekana CCM wako tayari kuruhusu independent candidate kwa nafasi za ubunge lakini sio kwa nafasi ya Urais.

Ndugu Munishi hebu tueleze utavukaje hiki kizingiti au sifa ya kuwa na chama ili uweze kugombea nafasi ya Urais?!

Katiba ya nchi inaweza kubadilishwa na 2/3 ya wabunge, CCM ina overwhelming majority ndani ya bunge. Ni kwa vipi wewe Munishi usiye na chama na tena mpinzani utaweza kuwashashi wabunge wa CCM wakubali independent candidate kwa nafasi ya urais?!

Tafadhari tufafanulie kinagaubaga, kabla ya kutuomba kura zetu, maana mpaka hapa wewe huna sifa ya kugombea urais (according to our constitution) Kwanza tatua hili tatizo la "kutokuwa na sifa" then ndiyo umwage sera zako na kutuomba kura.

Vinginevyo itakuwa ni kupoteza wakati kumjadili mtu ambaye sifa za kugombea nafasi husika hana.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 08 2003,12:36   



KATIBA SIYO MALI YA CCM

http://munishi.com/

Katiba ya Tanzania ni ya watanzania. Siyo mali ya CCM. Lazima kila mtanzania ahusike katika kuirekebisha au kuibadili. Kuna mengi yanayohitaji marekebisho na mengine yatatolewa kabisa. Najua kwamba nikiingia ikulu na katiba ya sasa itanikwamisha mengi. Tanzania ni sawa na gari iliyonoki injini. Inataka  matengenezo kamili ndani ya injini. Siwezi kuifanyia Tanzania MAREKEBISHO INAYOSTAHILI bila ya katiba mpya. Hata kama kipengele kimoja kitabadilishwa niweze kugombea bila chama cha kisiasa, hilo siyo lengo langu.

Lengo langu ni kuleta mabadiliko ambayo ndiyo kiu ya watanzania wengi wakubwa kwa wadogo. Hatuwezi kuwa na nchi yetu, bila katiba yetu. Tena katiba haiwezi kuwa yetu kama haina mchango wa mawazo yetu. Tunahimiza zoezi la kukusanya mawazo kutoka kwa watanzania wote lianze ndipo katiba irekebishwe. Bila hilo kufanyika  hakuna sababu ya kufanya uchaguzi kwani CCM watatumia mapungufu yaliyoko kwenye katiba kushinda uchaguzi kiulaini.

Tumeliona hilo. Ndiyo maana tunasema kwamba hakuna aliyehitimu kuingia katika uchaguzi na katiba ya sasa. Ina mapungufu mengi, Hatuitaki, Ni batili. Yeyote atakaeingia kwenye uchaguzi na katiba ya sasa ajue anafanya hivyo kinyume cha sheria. Ndiyo ni kinyume cha sheria kwa sababu Watanzania wengi wanataka KATIBA MPYA. Kujaribu kuwaburuza ili waingie kwenye uchaguzi bila ya kuibadili katiba ni mbaya kuliko wao kuchukua silaha na kuanza kudai haki zao kwa mtutu wa bunduki. Hatuombi hali ifikie hapo kwani itatuumiza wote. Lakini ikibidi, Hakuna jinsi.

Kuhusu baraza la mawaziri, nilisema wazi kwamba mimi sitakuwa na uwezo wa kuunda baraza la mawaziri. Katiba ya sasa inamruhusu rais kuunda baraza lake la mawaziri. Katiba mpya italiruhusu bunge kuunda baraza letu la mawaziri. Sifa za watakaogombea nafasi za uwaziri lazima ziambatane na taaluma zao katika wizara husika. Wakati wa kuchaguliwa waziri kwa sababu za kikabila, kiundugu na kirafiki, UMEKWISHA. Hata hapa kuna wengi tayari nimeona wataifaa Tanzania katika baraza la mawaziri. Mtu kama Augostino Moshi ukisoma posti zake utaona uanasheria ndani yake.

Hawa ndio tunaotaka kuwahimiza wagombee nafasi za waziri wa sheria na katiba. Wabunge wakiridhishwa na kuhitimu kwao katika fani husika watawachagua.
Nimemtaja Moshi siyo kwa sababu ni mchagga, bali nipate nafasi ya kujibu swali lake. Aliniuliza kama nakimudu kiingereza. Ukweli ni kwamba kiingereza nakimudu vizuri.

Lakini nilijifunza kwa njia ngumu zaidi. Nikija Nairobi mwaka 1984 nilikuwa siwezi kabisa kuwasiliana kwa kiingereza. Jambo hilo lilinikera sana. Niakaamua kuanzia mahali. Biblia ndicho kitabu kilichokuwa hakibanduki mikononi mwangu. Nilikuwa nimemaliza kuisoma na kuirudia mara tatu. Nikanunua madaftari makubwa ya kuandikia kama matano, halafu nikanunua Biblia ya kiingereza. Nilianza kuandika neno hadi neno, nikamaliza kuandika agano jipya. Mengi nilielewa maana kutokana na ukweli kwamba nilikuwa nimeyasoma katika Biblia ya kiswahili. Yaliyonishinda matamshi ilinibidi ninunue biblia katika kaseti. Yale ambayo sikuelewa kuyatamka, Biblia ya kaseti ilinisaidia kujua yanatamkwa vipi.

Hata kabla ya kumaliza agano la kale tayari nilikuwa na kiingereza kingi sana akilini mwangu. Tayari niliweza kuwasiliana kwa kiingereza kuliko.  Nasita kusema kuliko wasomi wengi Tanzania, lakini ukweli unabaki hivyo. Sasa hivi ndipo kasi ya kujifunza kiingereza imeongezeka Tanzania. Wakenya na Waganda wamefungua shule uchwara na wanaziita za kimataifa kwa sababu tu wanazingatia somo la kiingereza. Ningekuwa najua kutumia kompyuta wakati huo, nisingepitia njia ngumu hivyo kukijua kiingereza.

Lakini sijuti kwani maneno mazito ndani ya Bibilia yamekiongezea uzito kiingereza ninachotumia kuzungumza na hata kuandika. Sitaki nijisifu kwamba Kiingereza changu ni sawa na kile cha malkia wa UINGEREZA, lakini nitakuwa mpumbavu gani nishindwe kujieleza kwa lugha rahisi kuliko zote duniani? Kiingereza kwa sasa ndiyo lugha rahisi kuitumia kuliko hata kiswahili. Haya niliyoyaandika hapa hakuna mahali  katika kompyuta naweza kufanya "SPELL CHECKING", sababu ni kiswahili.  Lakini ingekuwa kiingereza, bila kujali natumia programu gani nitapata mahali pa kuisahihisha kazi yangu kiulaini.

Ni urahisi huo ndio unaonipa mashaka kwamba wengi hawajui kiingereza. Kuna rafiki yangu simtaji. Ni mwandishi wa habari katika gazeti la NATION lichapishwalo kwa kiingereza kila siku nchini Kenya. Ukisoma makala zake, utapenda. Mpangilio wa lugha, usahihi wa maneno, NK. Lakini wacha akuandikie barua ya mkono, Au akutumie ujumbe mfupi kwa simu za kipepesi. Utashangaa mbona kiingereza chake kibovu?
Kumbe amelemazwa na kompyuta ambayo inamfanyia kila kitu kuanzia "SPELL CHEKING" mpaka na mtiririko wa lugha. Je ni kitu cha kujivunia kujua kiingereza? Hapana. Hata wanaokiongea au kukiandika vibaya siyo makosa yao. Siyo lugha yao ya kwanza maishani.

Pamoja na umuhimu wa kiingereza duniani leo, Siungi mkono kasi watanzania waliyo nayo katika kukikimbilia kiingereza. Wengi wanalipa pesa za kutisha kwenye shule ambazo zinatilia mkazo kiingereza, Wengine wanawapeleka watoto wao nje Kenya Uganda, Na hapo nimetaja sehemu chache sana. Yote ni watoto wajue kiingereza. Kuna tofauti kati ya kuelimika na  kujua lugha. Lakini kwa watanzania wengi hilo hawalijui. Wanafikiri kuelimika ni kujua Lugha. Kuna uwezekano wa kuzijua lugha tofauti bila kuwa na elimu. Lakini kiingereza tu, sioni ulazima wa wazazi Tanzania kwenda kasi wanayokwenda kukifukuzia kiingereza. Kuna njia nyingi za kuweza kuijua lugha yeyote bila kuingia gharama kubwa wanazoingia watanzania.Nimalize kwa kusema kuna njia nyingi za kumuua panya. Ukiweka mtego utamnasa atakufa. Ukiweka dawa ya sumu jikoni, panya atakula na atakufa. Lakini ole wako mtoto wako akidhani hiyo uliyoweka jikoni ni peremende. Uliyotarajia yampate panya yatampata mtoto wako.

Watanzania wengi wameamua kumuua panya wa kiingereza wakitumia sumu jikoni. Tayari nimeiona hatari mbele yao. Nani awaambie njia nyingine rahisi ambayo ni kumchagua Munishi awe rais wa Tanzania chini ya katiba mpya nitainua kiwango cha elimu. Kiwango cha elimu kikiinuka Lugha zozote hazitakuwa ngumu watanzania kuzitumia. Naujua ugumu nilioupata kujua niyajuwayo, sitopenda mtoto wa kitanzania apitie niliyoyapitia kupata elimu.

Bwana Moshi nafikiri nimekujibu. Nashukuru kuniuliza hilo, kwani CCM wamekuwa wakimtesa sana Mrema kwa hilo. Najua hata mimi wataanza kutumia hilo kama mtaji wa kunipinga nisiwe rais. Lakini hata Mkapa kiingereza chake ni cha kubabaisha pamoja na kwamba alisomea lugha ya kiingereza kama somo ili aweze kuwa mhariri wa DAILY NEWS. Kwa mtaji wa lugha tena ya kiingereza hapa wamefika. Watafute jingine. Ikulu nitaingia tu. Nia na sababu ninazo. Kama walifikiria kwamba uwezo ni kiingereza, basi hata uwezo ninao.  

Kuhusu swali la uraia, maoni yangu ni kwamba Mtanzania anayetaka kurudi kuuchukua uraia wake, itabidi aukane uraia aliouchukua ugenini. Ni maoni yangu binafsi. Lakini kwa sababu tutabadili katiba, sijui maoni ya watanzania yatakuwaje kuhusu hilo. Kulingana na katiba ya sasa, Rais anakuwa kila kitu. Ndiyo maana maswali kama utafanyaje kuhusu hili na lile yanajitokeza kwa wingi. Lakini KATIBA MPYA mambo hayatakuwa hivyo. Kila jambo litashughulikiwa na wizara husika na wanataaluma husika.

Swali la uraia litashughulikiwa idara ya uhamiaji. Katiba mpya itawatengenezea mazingara mazuri ya kufanya kazi yao bila kuingiliwa kisiasa. Kwanza kutakuwa hakuna chama cha kisiasa madarakani.

Maswali mengi niliyatarajia, na bado nayatarajia. Wengi wamezoea sana utawala wa CCM wala hawajui itakuwaje bila CCM. Mimi naiona Tanzania mpya bila CCM. Picha hiyo iko akilini mwangu. Niko tayari kuendelea kuwafafanulia zaidi picha ya Tanzania mpya. Naiona iko nami. Mungu ameiweka maishani mwangu. Hakuna kitakachonitenga na Tanzania mpya iliyo maishani mwangu, labda maisha yenyewe ndiyo yanaweza kunitenga na Tanzania mpya na katiba mpya, halafu MAISHA MAPYA YA WATANZANIA.
Mungu bariki watanzania. Waonyeshe Tanzania mpya bila CCM.

   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Dec. 08 2003,12:55   

Quote (Munishi @ Dec. 08 2003,12:36)
Kuhusu baraza la mawaziri, nilisema wazi kwamba mimi sitakuwa na uwezo wa kuunda baraza la mawaziri. Katiba ya sasa inamruhusu rais kuunda baraza lake la mawaziri. Katiba mpya italiruhusu bunge kuunda baraza letu la mawaziri. Sifa za watakaogombea nafasi za uwaziri lazima ziambatane na taaluma zao katika wizara husika. Wakati wa kuchaguliwa waziri kwa sababu za kikabila, kiundugu na kirafiki, UMEKWISHA. Hata hapa kuna wengi tayari nimeona wataifaa Tanzania katika baraza la mawaziri. Mtu kama Augostino Moshi ukisoma posti zake utaona uanasheria ndani. Hawa ndio tunaotaka kuwahimiza wagombee nafasi za waziri wa sheria na katiba. Wabunge wakiridhishwa na kuhitimu kwao katika fani husika watawachagua.
]

ahahahhhahahahhahahahahahhhahah!!!!!!!!!!!!!1111 :D  :D  :D  :D  :D  :D  :D  :D  :D

Mbabaishaji mkubwa wewe :D  :D  :D  :D

Huwezi kuliachia bunge liteue Baraza lako la Mawaziri. Wewe ni mgombea binafsi inamaana huna hata Mbunge. Je, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri katika Office ya Rais n.k. watoke katika CCm. Hivi unataka kutuambia kweli hapo umebadilisha uongozi / Chama au tumebadilisha Rais.  Na kama ni kubadilisha Rais hata mwaka 2005 tunafanya hivyo kwani Mkapa hagombei tena, yaani hata ikishinda CCM Rais atakuwa mwingine.

Kama bunge litachagua baraza la Mawaziri kuna uwezekano mkubwa kwa Mawaziri wengi kutoka katika Chama kimoja. Mfano kama CCM ikiwa na Wabunge wengi na Mawaziri wote wakitoka CCM, kwa sababu watachaguana kwa kukujuana na Uchama utakuwa ndani yake.

Huoni kama hiki ni kichekesho!!!!!!!!!!!!

tafadhari Ndugu Munishi tueleze vizuri usituletee "kiini macho" hapa.

INANIUMA SANA!!!!!
Jina Kubwa

   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Dec. 08 2003,12:58   

Quote (Uwazi @ Dec. 08 2003,08:06)
Mizambwa, Munishi

Hebu twendeni step by step, tusitake kukimbia wakati kusimama tu hatuanza.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano hairuhusu wagombea binafsi katika ngazi ya urais. Ndugu Munishi anasema kwamba yeye sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, that's fine.

Ninachoomba ndugu Munishi atufahamishe ni kwa vipi ataweza kugombea nafasi ya urais wakati hana chama?!

Vinginevyo itakuwa ni kupoteza wakati kumjadili mtu ambaye sifa za kugombea nafasi husika hana.

Ndugu Uwazi huyu ni mbabaishaji tu hana sera wala Nyimbo. Amekosa la kusema. Muangalie anavyo taka kuudanganya Umma wote hapa.

INANIUMA SANA!!!!!
Jina Kubwa

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 08 2003,13:40   



http://munishi.com/

KUKU ALIYEZOEA KAMBA MGUUNI....

Watu wengine!!! Sasa huyu nae vipi? CCM imemkalia kooni mpaka haoni kingine baada ya CCM. Kuku aliyezoea kamba mguuni ukimfungua bado anafikiri amefungwa. Wengine itabidi twende nao hivyo hivyo. Siyo makosa yao. Kamba za CCM zimekaa mguuni kwa muda mrefu.

Katiba mpya siyo lazima kuwa mbunge ndipo uupate uwaziri. Kigezo kwamba lazima mawaziri wawe wanataaluma ndicho kitakachowapukutisha CCM pamoja na wingi wao bungeni.

Hata kama mtu atachaguliwa kwa kura za wabunge wote na awe siyo mwanataaluma katika wizara husika, hawezi kupitishwa. Tatizo la wingi wa wabunge wa CCM huwezi kulirekebisha kwa kumpa rais uwezo wa kuwachagua marafiki zake katika baraza la mawaziri. Bora tuwapate wanataaluma mawaziri kutoka CCM, {kama wapo} Kuliko kuwa na rundo la mawaziri wasio na taaluma za wizara wanazoziongoza.\

CCM ikiwekwa BENCH Tosha. Kama kuna watanzania waliokuwa CCM na ni wanataaluma, na wawe wametubu makosa ya kujiunga na chama cha majambazi, tutawatumia. Wengi wameanza kuliona hilo na wameanza kulihama jahazi linalozama. Ushauri wangu kwao, ni wafanye hivyo mapema. Wakichelewa mlango utafungwa. WATAZAMA pamoja na CCM.

   
Pillar



Group: Members
Posts: 319
Joined: July 2003

Posted: Dec. 08 2003,16:36   

Munishi

Nilikuvumilia sana na vile vile kusoma habari za maisha yako. Kwa papara zangu nilianza kukuuliza maswali lakini majibu yakawa ya mkato na ndugu Augustine Moshi akaomba upewe nafasi ya kujieleza zaidi.

Jana Mr. Augustine Moshi amekuuliza swali lakini sijaona jibu lake. Naomba utujibu maswali. Na unapojibu maswali yaweke vizuri hili yaonekane. Ukichanganya majibu ya maswali yetu na historia yako ya maisha tutakuwa tunachanganyikiwa.

Kama huwezi kujibu maswali yetu basi hakuna sababu ya kuelewa historia ya maisha yako zaidi ya yale tuliyosoma. Kwa kweli sasa naanza kupata wasiwasi.

   
aawakil



Group: Members
Posts: 22
Joined: July 2003

Posted: Dec. 08 2003,16:47   

Ndugu Munishi,

Kweli umenishangaza kwa kauli yako kuhusu uraia. Inaelekea bado mawazo yako ni za zamani na wa ukoloni hapo unaposema kuhusu suala la uraia mtanzania akitaka kurudi Tanzania lazima a ukane uraia hiyo nyingine. Hebu tumia akili yako nani ata kubali kuukana uraia wamarekani au nchi nyingine iliachukue uraia wa Tanzania. Samahani lakini hilo ni ndoto na mawazo yako binafsi. Katika hiyo global village na utandawazi wakati nchi nyingi duniani zina kubali uraia mbili wewe bado unamawazo wa zamani. Hiyo ina maana kuwa ujali watanzania na uko tayari kuwapoteza kwa kuwavulia uraia wao. Nchi nyingi za africa pia zina kubali uraia mbili nazo ni Ghana,Nigeria,South Africa,Rwanda, na kenya na uganda pia katika katiba yao mpya inaruhusu wananchi wake kuwa na uraia mbili.
Vipi Munishi mbona nilifikir kuwa una mawazo wa kisasa lakini bado mawazo yako ni ile ile na inaonekana kuwa hujali watanzania waliyo nje. Inasikitisha sana.

   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Dec. 08 2003,17:24   

Quote (Munishi @ Dec. 08 2003,13:40)
Katiba mpya siyo lazima kuwa mbunge ndipo uupate uwaziri. Kigezo kwamba lazima mawaziri wawe wanataaluma ndicho kitakachowapukutisha CCM pamoja na wingi wao bungeni.

Hata kama mtu atachaguliwa kwa kura za wabunge wote na awe siyo mwanataaluma katika wizara husika, hawezi kupitishwa. Tatizo la wingi wa wabunge wa CCM huwezi kulirekebisha kwa kumpa rais uwezo wa kuwachagua marafiki zake katika baraza la mawaziri. Bora tuwapate wanataaluma mawaziri kutoka CCM, {kama wapo} Kuliko kuwa na rundo la mawaziri wasio na taaluma za wizara wanazoziongoza.\

Bado hujaeleweka na hiyo Katiba Mpya jinsi itakavyokuwa. Endapo kama Waziri si lazima awe mbunge, na jinsi tunavyoelewa Wabunge ni wawakilishi wa Wananchi, huoni kuwa hapo utawaweka Mawaziri mliosoma wote, au hata kule Bungeni watapigiwa Kura watu wengine kushika Uwaziri hata kama hawakubaliki na Wananchi kigezo kitakuwa ni elimu yake na ana Marafiki Bungeni watakaompigia debe.

Hapo bado hujatueleza vizuri kuhusu suala hili la Katiba ambalo ni muhimu sana katika Uchaguzi ujao.

JARIBU KUFIKIRI TENA TUNASUBIRI UFAFANUZI WAKO.

INANIUMA SANA!!!!!!
Jina Kubwa

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 08 2003,19:18   



http://munishi.com/

SWALI LA MOSHI LIMEJIBIWA

"Nimemtaja Moshi siyo kwa sababu ni mchagga, bali nipate nafasi ya kujibu swali lake. Aliniuliza kama nakimudu kiingereza. Ukweli ni kwamba kiingereza nakimudu vizuri."

Swali la uraia pia nimelijibu. Idara ya uhamiaji ndiyo itakayohusika na swala la uhamiaji. Katiba ikirekebishwa, na hilo la kuwa na uraia wa nchi tatu au zaidi nalo mliweke. Likipitishwa liwe sheria, itakuwa hivyo.

Tatizo la wengi ni kwamba mnawaza kulingana na katiba ya sasa ambayo ni batili. Mimi mtazamo wangu ni katiba mpya. Katika hilo tutatofautiana. Na hiyo ndiyo maana nzima ya kujadili. Siyo lazima nikubaliane na kila mtu ndipo mjadala uendelee, Pia siyo lazima nipingane na kila mtu.

Muhimu lazima mjue katiba mpya haiandikwi na Munishi
akitumia mawazo yake. Katiba itajumuisha mawazo ya watanzania wote. Suala hapa ni wote tuone umuhimu wa kuwa na katiba mpya. Halafu itafuatiwa nini kirekebishwe na nini kitolewe kwenye katiba ya zamani. Yote hayo yatafanywa na kila mwananchi. Ni kweli kutakuwepo na wataalamu wa kuandika katiba lakini hata wao hawapaswi kuandika mawazo yao. Ni katiba yetu. Tuchange mawazo iwe yetu.

Tatizo la watawaliwa kujitawala kuna kazi. Mimi sitaki kuwatawala watanzania. Nataka kuwaongoza jinsi ya kujiongoza. Toeni mawazo yenu jinsi mnavyotaka muongozwe, na siyo kuuliza mtaongozwa vipi.

Rais ni mtu mmoja. Watanzania ni zaidi ya milioni arobaini. mawazo ya  mtu mmoja hayawezi kuwa ndiyo mwisho. Ilikuwa hivyo wakati wa Nyerere ambao bado tunao kwa kivuli cha Mkapa, Haitakuwa hivyo baada ya mimi kuingia ikulu na katiba mpya.

Nakubali kwamba wengine tutakubaliana na wengine tutakosa kukubaliana. Pia kuna wengine tutakaokubaliana kutokubaliana. Na kuna wale tutakaokubaliana kukubaliana. NA MJADALA UENDELEE. Tukikosa kukubaliana katika hili, tunaweza kukubaliana katika lile.

   
aawakil



Group: Members
Posts: 22
Joined: July 2003

Posted: Dec. 08 2003,19:33   

Ndugu Munishi,

Ahsante sana na nimekuelewa vizuri. Hii inaonyesha kwamba kweli unawafikiria watanzania walio nje na hicho ni kitu muhimu sana. Mtanzania ni Mtanzania awe mahala popote duniani. Kura yangu umepata.

9 Next Page