7 Next Page   
  Topic: CCM IMESHUSHA JEHANAMU TANZANIA, HOTUBA YA MCHUNGAJI KWA TAIFA < Next Oldest | Next Newest >  
Augustine Moshi



Group: Members
Posts: 318
Joined: May 2003

Posted: Dec. 01 2003,02:56   

Mimi naendelea kusubiri Mchungaji Munishi amalize kutuelimisha kuhusu historia ya maisha yake. Kwa vile jana ilikuwa Jumapili, bila shaka Mchungaji alikosa nafasi ya kuendelea na simulizi lake.

Nataka kumuuliza Mkunda hivi: kama ingekuwa kweli kwamba Munishi aliwahi  kuchomwa visu hilo ni kosa lake? Haiwezekani kwamba majambazi walimvamia na kumchoma visu? Nadhani tumpe fursa Mchungaji Munishi amalize kutueleza historia yake. Hata kama amewahi kupata ajali ya kchomwa visu huenda akatufahamisha ilivyotokea. Na wengi tungeweka picha zetu hapa huenda yangeoekana makovu mengi tu.

Mimi sio mwana saikolojia, lakini kama Munishi atakuwa na moyo wa kuendelea na simulizi lake kwa uwazi kama alivyofanya kwenye awamu ya kwanza, basi nitamuelewa once and for all. Nitaelewa hata ni kwa nini anataka awe Rais.

Augustine Moshi

   
Binti Lishe



Group: Members
Posts: 68
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 01 2003,16:04   

Hee!

Hii demokrasia itatupeleka 'jehenum'.  Siku moja nilisikia watu wakiongelea habari za picha ya George Bush kwamba kwa kuangalia picha yake tu unaweza kuelewa kwamba mtu huyu kichwani nati fulani zimelegea.

Asante Munishi kwa kutuwekea picha yako.  Wengine tumekuwa tukijiuliza huyu Munishi mwenye kuandika maelezo marefu marefu ni nani na yukoje?  Lakini, bahati nzuri umetuwekea picha na kutokana na picha wengine tumeweza kuelewa wewe ni mtu wa namna gani.  Macho yako yanadhihirisha mengi.  

Ole wetu Watanzania tukifikia mahali tukadanganyika na kuwasiikiliza na kuwapa uongozi wa nchi yetu watu waliokwisha kuchanganyikiwa.

Ni

Binti Lishe

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Dec. 02 2003,12:28   

Ndugu Munishi,
Naona uko kimya kidogo labda umetingwa na shughuli za hapa na pale lakini kumbuka kwamba wanabodi wanasubiri kwa hamu sehemu ya pili ya historia ya maisha yako ili waweze kupata picha halisi ya Munishi.
Na pia naomba nikukumbushe kwamba mtumishi wa mungu ni mtu mkubwa sana kuliko raisi wa nchi kwani hakuna kama mungu, maraisi na wafalme wanawategemea watumishi wa mungu katika utawala wao ndiyo maana makanisani na misikitini watumishi wa mungu (mashehe na wachungaji) wanaongoza ibada ya kuwaombea watawala watawale vizuri,kwa amani na maamuzi yao yalenge katika haki na wala yasilenge kwa shetani.
Wewe ni mtumishi wa mungu kama unavyojiita nadhani ingekuwa ni vizuri na hekima kuendelea kuwaombea watawala wetu waongoze kwa haki na amani ili maisha ya watanzania yawe kama unavyotaka kwani cheo cha utumishi wa mungu ni kikubwa sana, na wala si vyema na busara kutumia maneno machafu na makali kwamba unawania kiti cha uraisi ambacho ni kidogo kuliko cheo cha utumishi wa mungu.
Posting zako zimejaa uchochezi wa kutaka kuleta vurugu katika Tanzania kwa kuonyesha mabaya tu yanayofanywa na serikali tawala, umeshindwa kuonyesha zuri hata mmoja ambalo limefanywa na serikali tawala na hiyo si kweli kwamba toka uhuru hakuna mazuri yaliyofanywa na serikali tawala.
Kama mtumishi wa mungu ongea ukweli na kuwa na hekima kwani watumishi wa mungu ndiyo kimbilio la mwisho kwa watu wote hata wenye dhambi wanamtafuta mtumishi wa mungu ili kuungama ama kuomba msaada wa kuombewa msamaha, jaribu kuwa mkweli ili kujijengea heshima na tumia busara kabla ya kuanza kufanya kitu chochote ama la utumishi wako wa mungu una mashaka.
Usichanganye kabisa dini na siasa kwani kwa kufanya hivyo unataka kumwaga damu za watanzania. Ukabila una nafuu kubwa sana kuliko madhara ya kuchanganya dini na siasa, ona yanayoendelea kati ya palestine na Israel ama northern Island. Ninasema hivi kwa sababu ninaona unatumia dini (injili) kama fimbo ya kutukania serikali iliyopo madarakani, na kesho atazuka mwingine atatumia koran kwa hilo je tutafika kweli?. Kwanini usiamue kwamba uchungaji basi na ukajimwaga katika ukumbi wa siasa?, utawezaje kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja?. Munishi kaa chini na fikiria kwa makini sana kama kweli unaipenda na kuitakia mema Tanzania. Wakenya wliweza kuitoa KANU madarakani kwa kutumia siasa na wala dini, Zambia nako walitumia siasa kumtoa Kaunda, Malawi walitumia siasa kumtoa Banda. Tafadhali usitumie udini wala ukabila kwani ni hatari kubwa.
Kweli watu wanayaona mabaya ya CCM, lakini vyama vya upinzani havina sera za nguvu za kuweza kuibwaga CCM na pia vinaonekana wazi kwamba ni vyama vya kihuni tu, sasa wewe kama unazo hizo sera basi anzisha chama cha siasa na tumia hizo sera ili kuitoa CCM madarakani.

   
kalesa



Group: Members
Posts: 10
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 04 2003,00:12   

Mchungaji Munisi kuna mambo umezungumzia yamenigusa sana haswa ukizingatia ukweli wake, lakini nadhani maudhui ya ujumbe wako hayakuwa katika silka na desturi za kitanzania. zaidi umeonyesha jazba isiyo kifani sasa basi kama wewe kweli unaitakia mema nchi yetu ni bora ukajiunga kwenye jukwaa fulani la kisiasa ili wananchi wapate jua nini mtazamo wako kisera ni kweli kuna mambo yanaitaji mabadiliko katika utendaji wa nchi lakini kila kitu kina muda wake na mahali pake tafadhali fafanua nini utafanya kumnyanyua mwananchi wa nchi kiuchumi au nini kifanye lawama tuu hazitoshi kuipeleka nchi yetu mbele

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 04 2003,14:39   



Jamani Poleni sana.
Sikuwepo kwa siku chache. Nilifiwa na ndugu yangu huko Moshi. Niko Mjini Moshi kwa mazishi, na jana tarehe 3.12.03 tulimzika ndugu yetu Pantaleo Saunyaki Munishi aliyekuwa dereva wa Marehemu Kombe ambaye kifo chake kilizua utata huku wengi wakiamini serikali ilihusika na kifo cha mkuu huyo wa zamani wa kikosi cha usalama wa Taifa.

Pantaleo Saunyaki Munishi alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu. Madaktari walisema kwamba alikuwa na kansa tumboni.

Mara tu baada ya kumaliza shughuli za mazishi Moshi, Nitakuja tuwe pamoja kuendelea na kampeni zangu kuwania kiti cha urais.

Kama mjuavyo, mawasiliano ya Internet Tanzania na hasa mikoani ni ndoto ambayo wengi hawajaiota. Vibanda vya kuwasiliana kwa njia ya Internet ni vichache na pia kasi ya kuunganishwa ni sawa na sufuri. Unangoja dakika tano ndipo ukurasa ufunguke na kabla hujamaliza kuandika ulichokuwa unaandika, unaambiwa kwamba nusu saa imeisha.

Ndiyo maana nakubaliana na msemaji aliyesema kwamba hapa ni watanzania wachache sana wanaoweza kupata habari wakitumia Internet. Nami nahisi kwamba serikali inachangia katika kuhakikisha kwamba huduma hii inabaki kama anasa isiyoweza kufikiwa na wengi. Hilo wanaliweza kwa kupunguza kasi kwa wale wanaotoa huduma za Internet. Ikiwa ukurasa unafungua kwa dakika tano, nani wenye kipato cha kuwawezesha kuwa kwenye Internet kwa muda wa masaa mawili?

   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Dec. 04 2003,17:06   

Pole sana Ndugu Minishi kwa msiba uliowakuta. Hiyo yote ni kazi ya Mungu, daima haina makosa.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la bwana lihimidiwe.

   
aawakil



Group: Members
Posts: 22
Joined: July 2003

Posted: Dec. 04 2003,19:55   

Ndugu Munishi,

Kwa niaba ya watanzania tunaoishi na kufanya kazi Canada tunatuma salaamu za rambi rambi kwako na familia yako kwa jumla kwa msiba uliyo yapata kufiwa na ndugu yako mpendwa.
Tunaomba mwenyezi mungu kwa rehema zake amlaze mahala njema peponi.Tafadhali pokea na kubali rambi rambi zetu.

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Dec. 05 2003,00:30   

Ndugu Munishi,
Kwa niaba ya familia yangu napenda kukupa pole kwa msiba uliokupata. Hayo ni mapenzi ya mungu. Mungu alitoa na mungu amechukua. Chukua muda kidogo upumzike kabla hujaanza kujibu maswali ya wanabodi.

   
Pillar



Group: Members
Posts: 319
Joined: July 2003

Posted: Dec. 05 2003,07:28   

Pole ndugu Munishi natoa rambi rambi zangu kwako na kwa ndugu na jamaa wote.

Pillar

   
Uwazi



Group: Members
Posts: 176
Joined: July 2003

Posted: Dec. 05 2003,08:54   

Dear Munishi

Ninatoa pole zangu za dhati kwa kufikiwa na ndugu yako. Mungu akupatie uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Pia Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMEN.

R.I.P Pantaleo

7 Next Page