Munishi
Group:
Members Posts: 77 Joined: Nov. 2003
|
 |
Posted: Nov. 29 2003,13:43 |
 |

NIANZE
KUJIBU SWALI LA MHESHIMIWA PILLA
Siwakilishi chama chochote
cha kisiasa na maoni yangu lazima katiba irekebishwe iruhusu
wagombea binafsi. Kuhusu picha katika posti zangu, kwangu ni muhimu
kutumia picha kwa sababu ukumbi huu unaruhusu hilo. Wanasema katika
mawasiliano picha ina thamani ya maneno elfu moja. Una uhuru wa
kusoma hoja bila kuiangalia picha na una uhuru wa kuiangalia picha
bila kusoma maneno. Kwa hilo nawapongeza BCSTIMES kutuwekea ukumbi
ulio na mengi ya kusisimua.
Maisha ni safari ndefu. Kuna
mabonde na milima, Kuna kupanda na kushuka. Pole ndugu Augustine
Moshi. Haikuwa nia yangu kukuhuzunisha kwa historia yangu, lakini
niliona ni muhimu niseme kweli. Penye ukweli uongo hujitenga.
Mimi siyo tajiri kama alivyogusia mmoja wetu. Lakini ukilinganisha
na maisha utotoni, kweli mimi ni tajiri. Mkate ambao tulikuwa
tukiupata mara moja kwa mwaka, sasa unapatikana kwangu kila siku.
Mchele kama tulivyokuwa tukiuita ulikuwa unapatikana wakati wa
sikukuu ya Krismas pekee. Sasa watoto wangu ndio wanaopanga siku
gani wanataka wali au pilau. Kwa hilo namshukuru Mungu. Lakini
sijihesabu kuwa tajiri, kwani matajiri nawajua.
Mwingine
tayari ameanza kunisakama kwamba historia nimeandika nionewe huruma.
Hata sijaanza kuandika tayari wameanza. Hilo limekuwa tatizo langu
na wanadamu. Leo wanasema hivi, ukifanya wanasema vile.
Mimi
siyo MR.CLEAN, lakini siyo jambazi. Kulingana na Nyerere, Mkapa
alikuwa MR. VERY CLEAN. Lakini leo iangalie mikono ya Mkapa uone
damu iliyojaa mikononi mwake. Nyerere angeambiwa kwamba Mr CLEAN
MKAPA angekuja kuamuru mauaji ya kutisha Zanzibar asingekubali.
Wanadamu hubadilika. Wabaya wanaweza kuwa wazuri, na wazuri leo
wakawa wabaya kesho.
Kuna mtu aliuliza kwamba nchi yetu
inahitaji vitu vingapi ili iendelee. Kwa majibu ya haraka ninaweza
kusema Watu, Ardhi, Siasa safi na uongozi bora. Ndivyo
nilivyofundishwa shuleni. Lakini ukweli ni kwamba tunamhitaji Mungu
katika kila tufanyalo wanadamu ili tuweze kuendelea. Nchi ikiongozwa
katika misingi ya KWELI NA HAKI, itaendelea. Vinginevyo mtakuwa na
watu, muwe na ardhi na siasa mbovu ya ujamaa, na bado maendeleo
yatakuwa ndoto kwenu.
Siku mia moja za uongozi wangu sitaki
kusema zitakuwaje, kwani itategemea na yale mabaki nitakayoyakuta.
CCM wanachukua kila kinachoweza kuchukuliwa. Wanauza kila
kinachouzika. Wanabomoa kila kinachobomoka.
Sitaki
niwadanganye watanzania kwamba siku mia moja za kwanza zitakuwa
peponi. Tutaanzia mahali tutakapoikuta Tanzania. Na ni matumaini
yangu kuwa kwa neema za mwenyezi Mungu mafanikio makubwa
tutayapata. Kitendawili kiko katika KATIBA. Tunataka ibadilishwe
ili niingie ikulu bila siasa.
|