Munishi
Group:
Members Posts: 77 Joined: Nov. 2003
|
 |
Posted: Nov. 28 2003,13:46 |
 |

NIKO TAYARI KUJIBU MASWALI YENU
http://munishi.com/
Siogopi maswali. Nitajibu maswali, lakini sitapoteza muda kujibu
maswali ambayo tayari nimeyajibu katika post zangu hapa. Nikifanya
hivyo nitakuwa najirudia tu wakati lengo kubwa ni kumwaga sera zangu
hapa. Sijui kwa nini watu wanapiga resi mahali pamoja tuuuuu, hiyo
inaonyesha kwamba katika yote niliyosema hapa, hapo ndipo wameona
kamwanya ka kunibana.
Na wanafurahi kusema Munishi hapo tumemuweza. Nani? Kusema nilizaliwa
mwaka 1960 huko Moshi mnafikiri kutanipunguzia nini? Au nikisema
nilianza masomo katika shule ya msingi Kindi Chini Muyuni mpaka
darasa la nne kutaniondolea uwezo wangu kufanya niyatakayo?
Hapana. Haitanipunguzia chochote.Ninataka kuwa rais wa Tanzania
mpya yenye katiba mpya. Na nimeanza kuongea na wananchi wa
Tanzania ambao wanabodi ni kati yao. Ni wananchi wa Tanzania ndio
wenye uwezo wa kunikataa nisiwe kiongozi wao, na siyo maajenti fulani
wa CCM kuongea hapa wakijidai wanafanya hivyo kwa niaba ya wananchi
wa Tanzania. Hawataweza kunizuia kwani wakati wa kuyatimiza maono
hayo ni sasa na siyo baadaye. Pamoja na kwamba mna uhuru wa kuniuliza
maswali, pia mheshimu uhuru wangu wa kutojibu yale yaliyolengwa
kunidhalilisha. Mfano siwezi kujibu chupi yangu ni ya rangi gani.
N.K
Wengi wamedai kunifahamu sana hata wamediriki kuniita jambazi. Inashangaza
kusikia kwamba watu hao hao ndio hawanifahamu na wanataka CV yangu.
Kwangu naona kama wanataka kuitumia CV yangu kuniponda kwamba sifai
kuwa rais. Baada ya kuliamgalia kwa makini suala hilo nimeamua kuandika
historia yangu kwa mkono wangu mwenyewe. CV ambazo nimewaelekeza
kuzisoma kwenye Internet ni zile zilizoandikwa na vyombo mbalimbali
vya habari na kwangu hizo ndizo zinazofaa sana kwani sikuandika
mwenyewe. Lakini kwa kuwa walinihoji wakaandika kwa nini msisikie
kutoka kwangu mwenyewe?
HAPA NI SEHEMU YA HISTORIA YANGU

Faustin Munishi katikati mwaka 1974 nikiwa na shemegi aliyemuoa
dada yangu wa kwanza. Ni mwarusha wa Sanawari Loruvani Arusha, na
unajua kwa nini picha hiyo ilichukuliwa. Nilikuwa nimevunjika mguu
wa kulia, ndioyo maana nayajua yale maumivu Mkapa anayoyapata sasa.
Hiyo ndiyo picha ya udogo wangu kuliko zote nilizo nazo. Lakini
bado ipo ili wale wanaouliza alama mwilini mwangu wajue ni alama
za ajali ndogo ndogo maishani na siyo vinginevyo.
Nilizaliwa mwaka 1960 Katika kijiji cha Kindi Muyuni wilaya ya Hai
mkoani Kilimanjaro. Wa saba kuzaliwa kati ya ndugu tisa, na nilikuwa
wa kwanza kijana wa kiume kati ya dada zangu sita walionitangulia.
Alianza Nkankiwa, akafuatiwa na Felisiana, aliyefuata aliitwa Regina,
akafuatiwa na Amelina aliyefuatiwa na Maria halafu mimi. Baada ya
mimi walifuatia ndugu wa kiume na wa kike na kuifanya idadi kamili
kuwa tisa watoto wa mzee Sitefano Sarubare na mama Mkabauni makombo
Ngumbe. Wazazi walikuwa wakulima wadogo wadogo , japo baba alikuwa
akifanya kazi kwenye mashamba makubwa ya kahawa yaliyokuwa yakimilikiwa
na wazungu. Japo kwa sasa mashamba hayo hayapo. Hii ni kutokana
na sera za Nyerere kuwatimua wazungu waliokuwa wakimiliki mashamba
hayo na kuyafanya mali ya umma. Kwa sasa ni mbuga zisizo na wanyama.
Hakuna kahawa hakuna lolote.
Kwa bahati mbaya baba alifariki kabla ya wengi wetu kuzaliwa, na
kusema ukweli wengi hatukumuona kwa sura. Baada ya kifo cha baba
yetu mpendwa, mama alikumbana na matatizo mengi. Moja kubwa
kuliko yote ni kutakiwa arudi kwao akafanye mpango wa kuolewa kwani
alikuwa bado msichana mdogo mwenye watoto wawili tu. Mama
alikataa kata kata kwenda kwao na misimamo yake ndiyo inayotufanya
tuitwe kwa jina la baba japo wengi wetu siyo baba yetu kidamu. Kuacha
dada yetu mkubwa na ndugu aliyekufa kipindi kimoja na baba, wengine
tulizaliwa na ndugu wa marehemu baba kama ilivyo mila na desturi
za Kichagga. Mtu akifa na mke wake akatae kurudi kwao kuolewa tena,
Kichagga ndugu wa marehemu huzaa na mke wa marehemu kuendeleza jina
la marehemu. Wote tulisema kwamba baba yetu amekufa na wengine husema
hivyo hata leo.
Wakati huo alikuwa na mvulana na msichana, japo baada ya siku chache
yule mvulana alifariki na kubaki dada tunayemwita wa kwanza kuzaliwa
kwetu. Huyo alikuwa Nkankiwa. Hata jina lenyewe linakupa picha mama
alikuwa akipitia matatizo gani wakati huo. NKANKIWA maana
yake ni mwanamke wa shida na taabu nyingi. Pengine ni kutokana na
shida na matatizo aliyokuwa akiyapitia mama wakati huo ndipo akaamua
kumwita mtoto jina la kuja kumkumbusha hali hiyo baadaye.
Baada ya mimi kuwa mtu mzima niligundua kwamba baba yangu kidamu
yuko hai japo hakuchukua majukumu yeyote ya kunilea. Mama
ndiye aliyeteseka kutulea kwa shida japo shinikizo la kumtaka ahame
awaachie ndugu wa baba KIHAMBA lilikuwa likiwekwa kila kukicha.
Hawakufanikiwa kumwamisha mama babada ya wazee wa kijiji kuamua
kwamba mama lazima akae kwenye shamba la marehemu alee watoto wake
ambao ndio sisi. Ndiyo maana majina yangu ni Faustin Stephen Munishi.
Japo baba yangu kidamu ni mzee Alex Ndasikoi Munishi ambaye yuko
hai hata leo. Kwa wale waliowahi kuona picha za arusi yangu kwenye
web site yangu http://munishi.com/ watakuwa wamemuona
mzee Alex Msomi wa nyakati za kikoloni na amewahi kuwa mwenyekiti
wa chama cha ushirika KNCU Moshi kwa miaka mingi. Lakini yeye na
Nyerere hawakuwa wakipatana kwani Mzee Alex alikuwa akimwita KICHOMBA
CHA NGARENYI. Msije mkasema kwamba yeye ndiye aliyenifundisha kumchukia
Nyerere kwani hatuna uhusiano wa karibu sana. Ikizingatiwa kwamba
hakunilea, na isitoshe walitaka kuwamisha mama kwenye shamba la
marehemu baba, halafu uongeze kwamba hajanikatia KIHAMBA, japo kila
nikienda nyumbani sikosi kumpelekea sukari na suti kali kali, Unajua
uhusiano wetu naye ni wa namna gani. Mimi hupenda kubishana naye
kuhusu masuala yote kwani kulingana na yeye hakuna wasomi kama wale
waliosoma enzi za wakoloni, na yeye ni mmoja wao.
Ni swali gumu kumuuliza mama, lakini mimi niliuliza. Mama
alinisimulia yote. Kuanzia kifo cha baba yetu, na mateso aliyoyapata
baadaye. Kwa sababu ya shamba aliloacha baba, Wengine kati ya ndugu
zake hawakutaka mama abaki katika hilo shamba. Walihoji kwa kuwa
mama bado msichana, basi arudi kwao ili ndugu wa baba wachukue shamba
la Sitefano. Misimamo ya mama ndiyo iliyotufanya sisi tuendelee
kuitwa kwa jina la marehemu baba yetu. Alikataa katakata kwenda
kuolewa tena na akabaki hapo atunze kaburi la marehemu baba
mpaka leo. Pamoja na kwamba walimega shamba la baba na kubakiza
kipande kidogo, bado mama alivumilia na ndiyo maana hata leo tuna
mahali tunapoweza kupaita nyumbani. Hatuoni haya kuitwa watoto wa
Sitefano kwani kimalezi tulilelewa katika shamba aliloliacha hata
kama ndugu zake ambao ndio baba zetu wa damu walitaka mama aondoke
arudi kwao.
Kifupi ni kwamba tulilelewa na mama mzazi katika mazingira magumu
sana. Dada zangu watano hawakuweza kuuona mlango wa shule, lakini
wote wameolewa na wana wajukuu. Mimi na dada niliyemfuata ndio tuliobahatika
kwenda shule, pamoja na ndugu yangu na dada yetu wa mwisho. Wanne
tu katika familia ya watoto tisa ndio tuliobahatika kwenda shule.
Nilianza elimu yangu ya Msingi katika shule ya msingi Kindi Chini
Muyuni mwaka 1967 chini ya mwalimu Augusti Nderiananga. Nilisoma
hapo mpaka darasa la nne, na kwenda Shule ya Msingi Kindi Juu kuendelea
na darasa la tano kwani Muyuni ilikuwa mpaka darasa la nne tu wakati
huo. Kwenye shule ya Kindi juu ndipo kipawa changu cha kuimba kilianza
kujidhihirisha. Chini ya mwalimu Mkuu NKWELA ambaye naye alikuwa
mwalimu wa muziki, shule yetu ilijishidia zawadi ya juu mkoani Kilimanjaro
kwa wimbo wa kumlilia Karume. Wakati huo ndipo Karume alipouawa
na Nkwela alitunga wimbo wa kumlilia Karume ambao mimi niliongoza
kama kwaya master.
Mwaka 1974 ulikuwa mwaka niliofanya mtihani wa kuingia kidato cha
kwanza na sikuchaguliwa kuendelea. Mipango ilifanywa nikapelekwa
Dar mwaka huo huo. Wazazi wengi kutoka Mkoani Kilimanjaro walikuwa
wamegundua kwamba serikali ilikuwa inafanya ubaguzi katika kuwachagua
watoto watakaoingia kidato cha kwanza. Kuna mikoa ambayo ilikuwa
inabanwa makusudi ili mikoa mingine ipitishe watoto hata kama hawakufaulu.
Shule ilipatikana Dar na nikapewa jina la mtoto wa kizaramo aliyekuwa
ameacha shule. Lengo lilikuwa nirudie darasa, na uhakika wa kuchaguliwa
kuendelea na kidato cha kwanza ulikuwepo kwani jina lilikuwa Yusufu
Ramadhani. Wachaga wengi wasomi hawakusomea Kilimanjaro. Walipeleka
watoto wao mikoa mingine, na wakatumia majina yao kuchaguliwa kuendelea
na elimu ya sekondari.
Nilisoma katika shule ya msingi Kurasini kwa miezi sita nikiwa Ninaishi
na mtoto wa jirani yetu kijijini kwa jina la Ndeyanka Sabba. Yeye
ndiye aliyekuwa amepewa jukumu la kunitunza wakati wote wa masomo
yangu Dar. Kwa kuwa alikuwa mfanyibiashara ndogo ndogo za kuchoma
nyama pamoja na kuuza sigara katika vilabu vya KANGARA na NMC iliyokuwa
imepakana na UDA, Nilifanya kazi hizo kabla na baada ya shule. Asubuhi
ilinibidi niamke saa kumi na moja, nichukue boksi la sigara nipitie
kwenye bonde lililotenga Keko Magurumasi na Keko Machungwa, halafu
nitokee NMC iliyopakana na UDA. Hapo kazi yangu ilikuwa kuwauzia
sigara makuli waliokuwa wakipakua magunia ya unga na kuyapakia.
Tena madereva wote na makondakta wa UDA ilikuwa lazima wanione asubuhi
niwauzie sigara na wengine niwakopesha. Ningefanya hivyo mpaka saa
tatu asubuhi ndipo mlezi na tajiri wangu Nyeyanka Saba angefika
kutoka Kariakoo akiwa na nyama tayari kutengeneza mishikaki na ndizi
za kuchoma. Sasa tatu na robo ilikuwa ni saa yangu ya kuanza tena
mwendo kuelekea Kurasini shuleni. Nikitoka shuleni, moja kwa moja
mpaka kwenye vilabu vya KANGARA Keko Magurumbasi kuendelea na kuuza
sigara pamoja na nyama za kuchoma mpaka saa tano usiku.
Maisha yalikuwa magumu, na nilianza kupanga kurudi nyumbani Moshi.
Mwajiri wangu ambaye alipaswa kuwa mlezi hakuniruhusu. Japo alikuwa
hanilipi mshahara, alishauri niache shule ili nifanye kazi zake.
Nilikubali kwani Dar ilikuwa chungu kwangu kama pilipili. Nilifanya
kazi kwake miezi kama mitatu nikatoroka kwenda Moshi. Ilikuwa hivi.
Baada ya mauzo ya sigara NMC ilkuwa nije nyumbani niweke boksi la
sigara za NMC chini, halafu nichukue boksi la sigara za Keko Magurumbasi
kwenye klabu ya Chibuku na Kangara. Sikufanya hivyo. Nilichukua
pesa zote za mauzo ya siku hiyo nikaenda Kisutu kupanda gari ya
kwenda Moshi. Maneno ya shule na kufanya biashara Dar yakaishia
hapo.
ITAENDELEA
5 Next Page
|