4 Next Page  
  Topic: CCM IMESHUSHA JEHANAMU TANZANIA, HOTUBA YA MCHUNGAJI KWA TAIFA < Next Oldest | Next Newest >  
aawakil



Group: Members
Posts: 22
Joined: July 2003

Posted: Nov. 22 2003,21:25   

Ndugu Munishi,

With due respect I have read all your points but I feel you have left out one of the very important issues which should be addressed.

Mr. Munishi you are aware that many Tanzanians left for abroad for greener pastures and this happenened during the Nyerere era when there were a lot of economic hardships and many have left presently and are leaving. Now my question to you is what are your plans of inviting this Tanzanians who are abroad so they too can invest and contribute to the economy.
You are aware that many Tanzanians are abroad for many years now and have taken citizenships of their respective countries for being entitled to recieve all the benefits. Do you have any plans of introducing DUAL CITIZENSHIP to allow Tanzanians to hold dual citizenship and allow freedom of movement. I do know the benefits of dual citizenship are many. Could you please elaborate on this issue.
Thank you for your feedback

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 24 2003,12:33   



NYUMBANI NI NYUMBANI

http://munishi.com/

Pamoja na kwamba unaweza kupata mali na utajiri ugenini, lakini huwezi kupata kila kitu ugenini. Ndio maana Nyumbani ni nyumbani hata kukiwaje. Sera zangu kuhusu Watanzania walio nje, ni kuwaomba warudi nyumbani tuijenge Tanzania. Hata ukiwa na nini ugenini huwezi kuthaminiwa kama ukiwa nyumbani. Kuna mengi ugenini ambayo kila kukicha yatakukera. Swali kwamba utarudi lini kwenu, ni mojawapo ya mambo yanayokera. Hata ukipewa uraia wa kujiandikisha, huwezi kupewa uzito sawa na wazawa wa huko. Ombi langu kwenu Watanzania mlio nje: Karibuni nyumbani kwani CCM iliyoharibu nchi mwisho wake umefika. Leteni mali zenu na hakuna atakayewasumbua. Tutawapa nafasi za kwanza za uwekezaji katika nchi yetu.

Mimi mwenyewe nimekaa ugenini kwa muda mrefu. Japo ni taifa jirani ambalo hatupitani sana katika mila na utamaduni, hukosi ya kukukera kama mgeni. Mfano niliwahi kushinda nishani ya mwanzilishi wa kuimba nyimbo za injili (SOLO) Lakini kwa sababu sikuwa raia, vyombo vya habari vilisema kwamba nishani hiyo apewe mzawa. Wakampa nishani kwa sababu ni mzawa lakini mwanzilishi ni mimi. Vitu vidogodogo kama hivyo vinakukumbusha nyumbani.

Pamoja na kwamba Mkapa na CCM walikuwa wameniwekea ukuta nisikanyage Tanzania, mwenyewe niliamua liwalo na liwe na nikarudi nyumbani.Nilifurahi sana kuwaona wazazi, ndugu na jamaa zangu ambayo zaidi ya miaka kumi tulikuwa hatujaonana. Japo nilifuatwa kila nilikoenda na watu tofauti, haikuniondolea furaha yangu ya kuwa nyumbani. Sitaki kuongeza chumvi niseme kwamba nilikamatwa na kusumbuliwa, lakini nyendo zangu zote zilifuatiliwa.

Kilichonihuzunisha ni habari za kukamatwa kwa wenye maduka ya kanda za muziki. Kosa lao lilikuwa kuuza kanda ya Munishi toleo la saba kwa jina "MPENDE ADUI" Ilidaiwa kwamba ndani ya kanda hiyo kulikuwa na maneno "CCM aliyoanzisha Nyerere, Sasa imezeeka. Sera zake zimeiharibu Tanzania, Na Ujamaa ulishindwa kabisa, Watanzania Msiirudishe CCM madarakani." Hayo ndiyo maneno yaliyodaiwa kuwa  ya "UHAINI."  Wenye maduka nchi nzima waliwekwa ndani kwa kile kilichodaiwa "AMRI KUTOKA JUU" Wengine waliachiliwa baada ya kukaa mwezi kwenye CELL za polisi bila kufikishwa mahakamani. Wengine walitoa rushwa ya malaki ya shilingi za kitanzania kununua uhuru wao. Wengine walionywa vikali kutouza kanda zozote alizoimba Mwinjilisti Munishi.


Hii ndiyo kanda ambayo Serikali ya CCM iliipiga marufuku

Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kuna mama mmoja ambaye sakata hiyo haikumwendea vizuri na hivi tunapozungumza ni marehemu. Walikuwa wakimwita Mama Tony, mkazi wa Kindi chini Muyuni kilomita mbili kutoka  sekondari ya wasichana "WERUWERU." Bila kujua kwamba kanda ya Munishi imepigwa marufuku na serikali, yeye alikuwa akiziuza kwenye duka lake lililoko soko kuu la Moshi. Duka lake liko kwenye mlango wa kuingilia sokoni, na pengine ndiyo sababu likawa maarufu.

Ilifika siku ya siku, ambapo maofisa kutoka kituo cha polisi Moshi wealifika dukani kwake wakiwa wamevalia kiraia. Waliikuta kanda hiyo inaimba kwani ilikuwa haibanduki kwenye kinanda hasa ikizingatiwa kwamba ndiyo kwanza ilikuwa imetoka jikoni na ilikuwa inauza kama keki moto. Maofisa walijifanya kana kwamba hawaijui kanda yenyewe na wakauliza wapewe kanda ya Munishi kwa jina Mpende Adui. Walipopewa moja, walisema kwamba waongezewe tatu kwani walikuwa wanne. Baada ya kupewa walidai risiti na wakalipa pesa. Kilichofuatia hata wewe unakijua.

Walimuamrisha huyo mama kufunga duka, na wakaandamana naye kituoni. Alishinda huko mchana kutwa, na usiku wake wakaandamana naye nyumbani kwake kufanya upekuzi bila kibali kutoka mahakamani. Hawakupata walichokitafuta, kwani kanda zote zilikuwa dukani, na tayari walikuwa wamezibeba. Chini ya godoro walikuta pesa taslimu milioni tano za kitanzania. Waliuliza kwa nini pesa kiasi hicho ziko nyumbani na siyo benki? Majibu waliyoyapata yaliwasisimua zaidi. Mama Tony aliwajibu kwamba mume wake yuko Mererani kwenye machimbo ya dhahabu na kwamba shimo lake lilikuwa limetoa mawe. Pesa nyingine zimewekwa benki na hizi milioni tano ni matumizi ya nyumbani na dukani.

Walibishana wenyewe kama wabebe pesa ziwe kielelezo cha kesi ya kanda, na baada ya kubishana wao kwa wao pesa ziliachwa nyumbani na wakaandamana na Mama Tony kituoni.Usiku wa manane, askari wale wale walirudi nyumbani kwa mama Tony wakidai walisahau kitu fulani ndani ya nyumba. Walimkuta msaidizi wa nyumba, na walipofunguliwa breki ya kwanza ikawa ni kwenye chumba cha kulala na wakapekua godoro ili waone kama mzigo wa pesa bado uko. Walipoambiwa kwamba pesa zimepelekwa kwa mzee Mererani usiku huo, unajua jinsi walivyojisikia. Waliondoka shingo upande na kuwaacha wanakijiji waliogubikwa na woga wa magari ya polisi kijijini usiku wa manane ambapo siyo kawaida ya kijiji hicho kutembelewa na wageni kutoka serikalini.

Asubuhi yake Mzee mwenye nyumba aliwahi mapema polisi kuanza jitihada za kumtoa mke wake ndani hata kwa dhamana. Mikwala aliyowekewa ilikuwa babu kubwa. Kwanza aliambiwa kwamba shauri lao kubwa sana kwani amri ilitoka juu. Mzee wa kichagga kutoka Mererani akaanza kutumia pesa kumtoa mke wake. Aliongea na wazee maafande wadogo karibu wote bila mafanikio. Usisahau kwamba maongezi yanafanyika baa na bili zote za pombe pamoja na miguu ya mbuzi anayelipa ni Mzee wa Mererani. Wiki tatu zikakatika na mama Tony bado yuko ndani. Baada ya kuuliza nini kinachotakiwa ndipo alipoelekezwa amuone mkuu wa kituo. Aliyempa ushauri huo ni afande ambaye cheo chake ni koplo jina lake tunalo. Alimwambia mkuu wa kituo cha  polisi Moshi siyo mtu rahisi kuona kwa hiyo lazima mipango dhabiti ifanywe ili mkutano wake na mkuu wa polisi ufanikiwe. Mzee alikubaliana na kila kitu ili mradi mke wake atoke.

Hatimaye alifanikiwa kukutana na mkuu wa kituo cha  polisi Moshi.Mkutano ulifanyika kwenye hoteli kubwa kuliko ile waliyokuwa wakikutana na maafande, kwa hiyo bili za vinywaji na vyakula zilikuwa kubwa kuliko awali. Mzee wa Kichagga alichanganyikiwa alipoambiwa kwamba shauri lake hata mkuu wa kituo haliwezi, kwani hata yeye alipokea amri kutoka makao makuu Dar kwamba wote watakaokamatwa na kanda za Munishi wawekwe ndani hadi uchaguzi umalizike. Mwezi ukaisha na mama Tony bado alikuwa kituo cha polisi Moshi. Ilimbidi mzee wa Kichagga atumie kila pesa aliyokuwa nayo kununua uhuru wa mke wake. Hatimaye alifanikiwa kumtoa katika kituo cha polisi, na alipokuwa akiongea nami hakumbuki ni pesa ngapi alizotumia katika harakati za kujaribu kuununua uhuru wa mkewe, lakini alisema ni mamilioni ya shilingi. Mama Tony alitakiwa kuripoti polisi mara mbili kwa wiki na alifanya hivyo kwa mwaka mzima. Mpaka wakati walipoambiwa kwamba faili ya kesi yao imefungwa, Maisha yao hayakuwa sawa tena. Pesa zilikuwa zimewapungukia. Biashara ilikuwa imezorota, Bado maofisa wa polisi walikuwa wakija dukani na nyumbani kwao kila wanapoamua kufanya hivyo.


Afya ya mama Tony ilianza kuzorota japo hakudai kuteswa alipokuwa kituo cha polisi kwa muda mrefu. Mwenyewe alisema hakuwahi kupigwa na askari wakati wote akiwa rumande ya polisi, lakini anasahau kwamba haikumpasa awe hapo zaidi ya masaa ishirini na manne bila kufikishwa mahakamani.  Mwezi wa nane mwaka huu 2003 Mama Tony aliaga dunia baada ya kulalamika kwamba kichwa kinamuuma siku moja kabla ya kifo chake. Siyo nia yangu kukihusisha kifo chake na serikali ya CCM, lakini msomaji unaweza mwenyewe kuangalia mchango wa CCM katika kifo cha mama Tony na ufukara wa mume wake.

Alikuwa milionea wa Mererani, lakini baada ya serikali kuyaingilia maisha yake sasa hana pesa. Hata nauli ya kwenda Mererani kujaribu bahati siku hizi anaomba. Mbaya zaidi amempoteza mke wake mwaka huu. Watoto yatima, Baba mjane, na kanda zake hawakumrudishia. Kanda alikuwa amezinunua kutoka kwa wakala aliyekuwa amezifuata Nairobi. Hii ndiyo CCM ambayo kila nikisema haifai kuwa madarakani wengine hawanielewi. Nashukuru wengi wananielewa hasa wale waliowahi kukutana ana kwa ana na mateso ya CCM. Jamaa na marafiki wa Waislamu zaidi ya sabini waliouawa Zanzibar wakati wa uchaguzi uliopita watanielewa nisemapo CCM ni chama cha wauaji. Wenye maduka ya kanda walionyanganywa kanda walizonunua kwa pesa taslimu, watanielewa kwa nini nasema CCM ni Chama cha Majambazi.

Dawa ni kuitoa CCM madarakani kwa njia ya kura. Kura yako ndiyo uhai wako. Usikubali kuiuza kwa pesa au ahadi za uongo kutoka CCM. Wakikupa pesa kula lakini kura yako usiwape CCM. Nasema pesa pokea kwani ni mali yako. CCM hawana kilicho chao bali kila walicho nacho waliwanyanganya wananchi wa Tanzania. Mungu amesikia kilio cha watanzania na ameanza kutusaidia kuufikia ukombozi wetu. Mungu wabariki wananchi wa Tanzania. Wasaidie kuitoa CCM madarakani bila umwagikaji wa damu. Watanzania walio nje wape moyo wa kurudi kuja kuijenga nchi yetu ya Tanzania. Tumeomba machache katika jina la Yesu. AMEN.

   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Nov. 24 2003,13:01   

Taaluma yako ni ya Muziki, huna hata uwezo wa Kuongoza isipokuwa kuongoza kwa maneno ya mahubiri.

Mimi kwa ushauri wangu nakuomba nenda kagombee uongozi katika Kanisa lako. Narudia tena kukueleza kuwa si vizuri kuchanganya Dini na Siasa. Kwani lazima utaleta mgogoro wa Kidini, au Kisiasa kisha kuvunja amani uliyopo ingawa hutaki kuiona.

Chagua kimoja uwe nacho katika maisha yako.

"USIFANYE NYUMBA YA BABA YANGU KUWA NYUMBA YA BIASHARA"

INANIUMA SANA!!!!!
Jina Kubwa

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 24 2003,15:03   



Mchungaji Faustin Munishi Rais Mtarajiwa Tanzania

http://munishi.com/

Injili inalinda maslahi ya Mungu duniani. Watu dunia na vyote vilivyoko ni mali ya Mungu. Hatuwezi kunyamaza wakati Mkapa na kundi lake wanapowaua waislamu zaidi ya 70 huko Zanzibar kwa sababu za kisiasa. Hata kama waliouawa siyo wakristo, lakini ni watu wa Mungu. Tukilinyamazia kesho itakuwa zamu yetu kuuawa. Hatuna nia kujiunga kwenye siasa, lakini wanasiasa wanapoyaingilia maslahi ya Mungu, chombo pekee kukemea hayo ni INJILI. Tunapowakemea wanasiasa, ndiyo tunaihubiri Injili. Tunaponyamaza ndiyo tumechanganya siasa na dini. Kwa hiyo sisi tunaokemea maovu yatendwayo na Mkapa, ndio tunaoihubiri Injili. Wale wanaowaunga Mkono kina Mkapa na kikosi chake cha mauaji ndio tunaotakiwa kuwaambia waachane na siasa kwani itawatoa katika kweli. Nasikitika kusema kwamba tayari wameshatoka katika kweli. Kwa hiyo siwezi kuacha kuyakemea maovu wanasiasa wayatendeayo jamii. Nikifanya hivyo nitakuwa nimekoma kuihubiri Injili.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 25 2003,11:29   



MKINICHAGUA NITAUINDA SERIKALI YETU  SIYO YANGU

http://munishi.com/

Kinyume na ilivyo sasa, Mkinichagua kuwa kiongozi wenu 2005 nitaunda serikali yetu. Katiba ya sasa inamruhusu rais kuunda baraza lake la mawaziri. Katiba mpya ambayo ndiyo ninayoipigania, Bunge ndilo litakalochagua mawaziri. Wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi, ndio watakaowachagua mawaziri wakitumia kura. Watakaogombea nafasi za uwaziri siyo lazima wawe wabunge, lakini ni lazima wawe wanataaluma katika wizara husika. Hakuna njia za mkato katika hili. Wananchi ndio watakaokuwa na uwezo wa kuwafuta mawaziri kazi, baada ya malalamiko yao kufanyiwa uchunguzi na mahakama. Hata majaji wa mahakama kuu watachaguliwa na bunge. Kila taasisi itakuwa huru kufanya sawa na taaluma zao bila kuingiliwa na wanasiasa. Kazi kubwa ya rais itakuwa kuwasikiliza wananchi wanataka waongozwe vipi, na kuangalia jinsi gani wananchi wenyewe wanaweza kusaidia katika kujiongoza.

Wakati wa kupoteza muda kujadili nani anayefaa kutuongoza umepita. Sasa tunataka nani tusaidiane naye kujiongoza. Badala ya kuwatukana watu ambao hawajaonyesha nia ya kuwania urais, ni wakati wa kumuuliza aliyejitokeza atafanya nini tofauti na serikali zilizopita. Nimesoma kwa mshangao jinsi watu fulani wanavyopoteza muda kutaja majina ya watu na kuyapaka matope. Utawasikia wakisema fulani hafai au anafaa kuwa rais. Mbaya zaidi wataanza kuwatusi waliowataja na wenyewe wala hawana ndoto za urais. Pengine wenyewe wanajiona duni hawawezi lolote mpaka wapate mtu wa kuwaongoza. Swali ni je! wenyewe wanafaa kuongozwa.

Katika serikali yetu tutakayoiunda, kila mtu ni muhimu.Tutampa kila mtu nafasi ya kujinadi nini anaweza kukifanya vizuri zaidi na kutumia kipawa hicho kulijenga taifa. Ushauri wangu kwa hawa wanaopoteza muda wakitauta nani anayefaa kuwatawala, waanze sasa kuonyesha wao wanaweza kufanya nini nami nitahakikisha taaluma na vipawa vyao vinatumika kulijenga Taifa. Rais hawezi kuwa mtu aliyesomea kila kitu. Na haitakiwi iwe hivyo. Mara nyingi taaluma ya rais siyo muhimu akishakuwa rais. Mfano ni Mkapa ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari. Kinyume na ilivyotarajiwa, Yeye ndiye anaewatukana waandishi na kuwaita wajinga, isitoshe wengine anawaweka ndani  kutumia serikali yake kuzifungia kazi zao.

Wakati wa rais kuunda baraza la mawaziri akitumia ndugu na marafiki zake umeisha. Serikali zilizopita watu walikuwa wanasimamia wizara tofauti na taaluma zao. Mtu anaweza kujiuliza kwa nini serikali ilitumia pesa nyingi kuwasomesha na baada ya kuhitimu  wasipewe nafasi ya kuonyesha umairi wao katika taaluma zao? Siyo ajabu kila wizara ilikuwa "inaboronga."

Kama nilivyotangulia kusema, nitakuwa rais asiye na madaraka mengi kama ya Mkapa. Bunge ndilo litakaloamua mambo mengi ya kiserekali, na wananchi ndio askari wa kuangalia utekelezwaji wake. Wananchi ndio watakaokuwa na madaraka kuliko viongozi serikalini. Ulinzi mkubwa watapewa wananchi na mali zao, kinyume na ilivyo sasa ambapo wanasiasa ndio wanaolindwa kuliko wananchi. Siyo ajabu mkaniona mitaani baada ya kunichagua niwe rais wenu. Sitawaogopa kwa hiyo sitakuwa na ulinzi kama alio nao Mkapa. Sina madaraka mengi kwa hiyo maadui zangu watakuwa wachache. Mkapa analindwa kwa sababu mtu akiweza kumuua serikali yake imekwisha. Mimi haitakuwa hivyo. Kwanza serikali ni yetu, na mmoja wetu akiondoka serikali inabaki kwa sababu ni yetu.

Utendaji katika ofisi zote kuanzia ikulu utakuwa rahisi. Mafaili ya ikulu yatapungua kwani kila wizara itapewa nguvu ya kufanya mambo yake. Isitoshe IT ndiyo itakayopewa kipaumbele katika uongozi wetu. Badala ya mafaili kibao, kutakuwa na kompyuta chache kutunza data za kila wizara. Wananchi watawezeshwa kujua nini kinaendelea katika ofisi yeyote ya serikali kwa njia ya Redio TV na Internet. Kila juhudi zitafanywa kufikisha habari kwa wananchi ili wafanye maamuzi baada ya kuelewa. Ndugu wananchi nina mengi, lakini nikomee hapo ili niruhusu maswali. Naweza kuendelea na kuendelea kumbe ninayogusia hayakuhusu ulipo wakati huu. Nangoja kusikia kutoka kwenu. Usiogope kuuliza lolote ili unipe kura yako baada ya kuelewa nitafanya nini nikisaidiana na wewe kuifanya Tanzania mahali pazuri pa kuishi tofauti na serikali za awali.

   
MTANZANIAA



Group: Members
Posts: 13
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 25 2003,17:25   

Nakubaliana na Bwana Munishi Tanzania tunataka mabadiliko. Siyo tungoje kifo kitubadilishie viongozi, tunaweza kubadilika viongozi wa CCM wakiwa hai waone yale yanayoweza kufanywa na wengine bila wao madarakani. Ndiyo maana wote tunaungana katika kumuombea Mkapa apone haraka aone kwa macvho yake Watanzania wakiikataa CCM kwa njia ya kura.

Habari hizi za BBC hazikutufurahisha Watanzania wote.

"Tanzanians are following with keen interest the state of their president's health after he underwent hip surgery in a Swiss hospital.
President Benjamin Mkapa first became ill on the eve of a summit in August.

His poor health has led important political and economic meetings to be postponed and some diplomats and business leaders are worried.

Conflicting statements about the causes of the president's health problems have raised the concerns of some Tanzanians.

'Avoid travel'

After developing high blood pressure in August this year, Mr Mkapa was seen using a walking stick when receiving fellow leaders for a summit of the Southern African Development Community.

Later, State House issued a statement saying the president was suffering from arthritis, a disease that can cause pain and swelling of the joints.

Earlier this month, the speaker of the national assembly told parliament that he had to fly to the United States to represent President Mkapa after the head of state was advised by doctors to avoid travel.

Shortly afterwards, State House said the president would make an official visit to Geneva and would also use the opportunity to see doctors.

A few days later, State House issued yet another statement saying the president was fit and was performing his duties as the co-chair of the globalisation secretariat.

However, State House later announced that Mr Mkapa was admitted to hospital after surgery and would remain there for an unspecified time, awaiting test results.

Absent leader

Mr Mkapa will not be able to attend a special meeting of the business council later this month, which was due to be attended by Microsoft millionaire Bill Gates, the Aga Khan, heads of international financial institutions, and representatives of key car manufacturers.

Government sources say he is also unlikely to chair the East African Community heads of state summit scheduled for the end of the month.

The meeting is meant to witness the signing of the regional common market treaty.

Though it has not been confirmed when the president will be out of hospital, sources say it may take up to two weeks before a complete diagnosis is done and a confirmation of what exactly the president is suffering from. "

   
Pillar



Group: Members
Posts: 319
Joined: July 2003

Posted: Nov. 25 2003,22:35   

Ngoja ninywe maji kwanza. Mambo mazito hapa.

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Nov. 26 2003,01:16   

Kwako ndugu Munishi,
Nimepitia kwa makini sana posting zako zote katika mjadala huu. Umeongelea masuala mengi sana kwa wakati moja na wakati mwingine umekuwa unachanganya mambo ambako kunapelekea kuonyesha wazi kwamba huelewi unasema nini.
Sikiliza Munishi, Tanzania imekulea na kukufikisha hapo ulipo. Umeanza kuimba nyimbo za dini na kujipatia pesa ndani ya Tanzania yenye amani na utulivu wa hali ya juu katika dunia ya leo. Na ulianza kuimba nyimbo za dini (kujifanya mlokole) baada ya Serikali tukufu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kukudhibiti katika shughuli zako za ujambazi kwa kutumia silaha na uporaji wa magari pale Moshi na Arusha. Sina imani na wewe hata kidogo na mtu yeyote mwenye akili na anayempenda mungu hawezi kuwa na imani na wewe hata kidogo, unajiita mchungaji na kuhubiri injili ya mungu lakini katika posting zako unahubiri injili ya shetani kwa maana kwamba unataka kutuletea kosovo ndani ya Tanzania.
Wewe unataka kuwa Raisi wa Tanzania na sasa uko mafichoni Kenya (Ukimbizini) huoni kwamba unachekesha na kuonekana chizi?.
Jenga hoja kwa amani na lugha inayoeleweka na si matusi na kashfa, kumbuka fadhila ama kumbuka ulikotoka. Kwa umri wako wewe ni mtoto mdogo sana huwezi kumtusi hayati baba wa Taifa ambaye amefanya mambo makubwa yanathaminiwa duniani kote, muache hayati baba wa taifa apumzike kwa amani peponi.

   
Uwazi



Group: Members
Posts: 176
Joined: July 2003

Posted: Nov. 26 2003,04:02   

Quote (Bwabwaja @ Nov. 26 2003,01:16)
Na ulianza kuimba nyimbo za dini (kujifanya mlokole) baada ya Serikali tukufu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kukudhibiti katika shughuli zako za ujambazi kwa kutumia silaha na uporaji wa magari pale Moshi na Arusha.

Bwabwaja

Ninaona umepasua jipu, historia ya Munishi ninaifahamu vizuri, sikutaka kumvisha paka kengele. Kusema kweli nilibaki kinywa wazi pale bwana mmoja alipomu-support Munishi.

Kama kweli mabadiliko tunayotaka ndiyo haya ya kuing'oa CCM na kuweka watu wa calibre ya Munishi, then we've a looooooong way to go.

Ukweli ni kwamba Watanzania wengi wameichoka CCM na wako tayari kuing'oa madarakani. Lakini Tatizo kubwa ni opposition. There is no serious and credible opposition in Tanzania. (Zanzibar is another case)

Most of oppositions walioko Tanzania ni wa calibre ya Munishi, they have very bad background. Sasa hapa Watanzania tunabaki bila choice bali kuipigia kura CCM. I'd better vote for CCM kuliko kumpigia kura gangster aliyejificha under the guise of ulokole.

Ndiyo maana nikamuomba Munishi at least anitajie kwa majina watanzania watakaounda baraza lake la mawaziri. Mwingine akanirukia eti nikifahamu majina yatanisadia nini? Nikaichukulia kama a joke of the day!! If someone doesnt know that (credible) name plays a great role in politics, I'm sure that s/he doesnt know also how to vote (to use his vote wisely).

That's the cost of democracy, if a nation/country majority of his people are ignorant u'll end up having ignorant/hypocrisy leaders.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 26 2003,07:49   



NAKANUSHA UVUMI UGONJWA WA MKAPA

http://munishi.com/

Kwanza kabisa  napenda kukanusha uvumi ulioenea Tanzania. Wengi wanasema Nyerere ndiye anayesababisha ugonjwa wa mheshimiwa Mkapa. Wanadai kwamba kuyauza mashirika ya umma kwa mabepari, ndiyo sababu Nyerere anataka kumwita Mkapa kuzimu haraka. Wanaendelea kudai kwamba ujamaa ambao Nyerere aliuingiza ndani ya mifupa ya Mkapa, ndio unaopingana na utandawizi na soko huria ndani ya nyama na mishipa ya Mkapa. Wanasema mifupa inauma kwa sababu ujamaa hautaki kutoka, pamoja na shinikizo unaowekewa na mishipa ya damu. Wanasema ndani ya Mkapa damu imeiwekea mifupa shinikizo ili iutoe ujamaa ndani, na mifupa imekataa hilo katakata. Matokeo mifupa inasagana yenyewe. Huo ndio uvumi ulioenea katika kila kona ya Tanzania.Wengine wanasema Waislamu waliouawa wakati wa uchaguzi uliopita ndio wanaomtesa Mheshimiwa Mkapa. Kuna wanaosema kwamba pengine ndugu wa jamaa waliowahi kuuawa au kuteswa na CCM ndio waliomloga Rais.

Mimi kama mchungaji  napinga uvumi huo kwa nguvu zangu zote. Mtu akisha kufa hana uwezo wa kurudi duniani kwa njia ya roho aje afanye lolote kwa walio hai. Hizo ni imani potovu za kishirikina ambazo hazina msingi wowote katika maandiko ya neno la Mungu. Pia siamini kwamba Mkapa amelogwa. Kwa maoni yangu Mkapa anaumwa kama kawaida ya wanadamu kuumwa. Maadui zake watakosea kufurahia kuugua kwa Mkapa, kwani hata akifa siyo adhabu tosha ya makosa aliyoyafanya. Adhabu inayomtosha ni kuwa hai maadui zake wamsamehe, na wamtendee mema badala ya mabaya aliyowatendea. Nakubaliana na maoni kwamba wote tunatakiwa kumuombea Mkapa apone haraka. Lakini kama ikishindikana, tutasema MAPENZI YA MUNGU YATENDEKE.

Binafsi ningependa kuendelea kupinga sera za CCM ambazo nazichukia sana na Mkapa akiwa hai. Nilipoanza kumpinga Nyerere mwaka mmoja kabla ya kifo chake, vyombo vya habari havikuandika. Nilipotoa kanda baada ya kifo chake Nyerere, wengine walinisakama kwamba Mbona alipokuwa hai sikusema lolote? Unaweza kuwahesabia haki kwa hilo lakini si kweli kwamba niliogopa kumkosoa Nyerere akiwa hai. Nilifanya hivyo. Lakini jinsi alivyokuwa amethibiti vyombo vya habari ungesemea wapi kwamba Nyerere alikuwa mwendawazimu? Sitaki wanaonipinga wawe na sababu ya kusema namkosoa Mkapa akiwa marehemu, ndio maana inanilazimu niombe apate nafuu.

Siyo kwamba hata Mkapa akiwa hai watakosa ya kusema, Hapana. Watasema Mengi sana. Wengine wanasema sifai kuwa rais kwa sababu  nilikuwa jambazi. Ningekuwa jambazi sasa hivi ningekuwa jela. Hasa baada ya kuikosoa serikali kesi zote zingefufuliwa. Lakini wanajua kwamba sijawahi kuiba mali ya mtu ndio maana wanatapatapa kutafuta matope ya kunipaka.

Tukirudi kwenye hoja, CCM lazima watoke madarakani. Haijalishi mbinu gani watakazotumia kuwafisha moyo wanaharakati za mabadiliko, lakini kutoka watatoka.

Serikali yetu wananchi tutakayoiunda haitalipiza kisasi.  Macho yetu tutayaelekeza mbele kuiendeleza Nchi na siyo kutafuta Mkapa tumweke ndani. Kwa hiyo Mkapa asiwe na wasiwasi kwamba nikichukua madaraka UKONGA ndiko kutakuwa nyumbani kwake. Hapana. Ikiwa Mtu aliamuru watu zaidi ya sabini wakauawa kwa sababu za kisiasa, hata ukamchukua umkatekate vipande sabini bado haitoshi kugharamia maisha ya wale sabini. Isitoshe utakuwa umongeza kifo cha mtu ambaye angekufa tu hata kama hukumuua. Adhabu kali kwa Mkapa ni kuwekwa benchi wao na CCM halafu waone nchi ikinawiri kwa miaka miwili ya kwanza. Inazidi adhabu ya kifo kwao. Lakini mali za wananchi lazima warudishe. Majengo na viwanja vyote vilivyo katika jina la CCM siyo mali ya chama bali ni mali ya wananchi wa Tanzania. Hayo tutachukua. Pesa zote za wizi walizojiwekea nje ya nci tutazichukua.

Tutaiomba jumuia ya kimataifa itusaidie katika kuhakikisha kwamba pesa zote viongozi wa CCM walizoiba zinarudi mikononi mwa Watanzania. Kabla hawajatupa mikopo, tutawaomba watusaidie kurudisha kilicho chetu kwanza na mikopo ifuatie. Mikopo ina masharti, lakini pesa zetu CCM walizoweka kwenye mabenki yao hazina masharti kwani ni zetu. Wana CCM watakaoamua kubaki nchini baada ya mabadiliko hatutawasumbua bali tutawaambia wafungue macho waone kazi ilivyopaswa kufanywa.

Wananchi wapendwa Msife moyo na kejeli za CCM. Kazi iliyo mbele yetu ni moja nayo ni kuitoa CCM madarakani. Kura yako ndiyo silaha yako. Hakikisha unayo na uitumie vizuri.Penye nia pana njia. Msife moyo. Mungu yuko upande wetu. Milima mingine itayeyuka yenyewe na mtapita kukiwa tambarare. Bahari nyingine zitakauka zenyewe na mtapita kama nchi kavu. Tusimame kama Daudi. CCM ni GOLIATHI, lakini jiwe moja ndani ya kombeo lilimaliza kiburi cha Goliathi. CCM mnaowasikia leo wakitamba nitawaletea kichwa chao wakiwa wamenyamaza.Umoja wetu ndiyo nguvu yetu.

4 Next Page