18 The End Page 1
  Topic: CCM IMESHUSHA JEHANAMU TANZANIA, HOTUBA YA MCHUNGAJI KWA TAIFA < Next Oldest | Next Newest >  
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 85
Joined: Oct. 2003

Posted: Mar. 09 2004,00:27   

Kwa mtaji huu inaonesha wazi kwamba mwaka huu mirembe itajaa wagonjwa. Ndugu waziri wa Afya tafadhali andaa mirembe hospital iwe tayari kupokea wagonjwa hao.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 96
Joined: Nov. 2003

Posted: Mar. 09 2004,13:42   


http://munishi.com/

CCM NDIYO KIINI CHA MATATIZO YETU TANZANIA

Machozi yananitoka nikiyakumbuka mateso ya CCM Tanzania. Wananchi tulifanywa watumwa wa CCM katika nchi yetu. Michango ya lazima ilikuwa ni kawaida. Walisema wanataka pesa za chama. Ukisema wewe siyo mwanachama wanasema watanzania wote ni CCM wapende wasipende.  

Viongozi wa CCM walionekana kama miungu wadogo. Nasema hata sasa wanaonekana hivyo. Dola ndiyo iliyoogopewa Tanzania. Polisi na viongozi wa CCM waliogopewa kuliko moto wa Jehanum. Wenyewe walihesabiwa kuwa JEHANAMU Tanzania. Wangeweza kumkamata wamtakaye, wakamtesa wakamfungulia kesi bandia, wakamfunga jela. Hata kutokuwa na kazi ilikuwa ni kosa la jinai.

Kazi waliziharibu wenyewe, halafu wakatunga sheria ya kuwakamata wasio na kazi. Waliwaita wazururaji. Nasikitika kwamba sheria hiyo inayokiuka haki za binadamu bado inatumika hadi leo. Kazi ya serikali yangu itakuwa kutengeneza mazingira yatakayozalisha kazi nyingi kwa watanzania, na siyo kujinaisha kutokuwa na kazi. Mtu kukosa kazi siyo kosa lake. Kwa nini afungwe jela kwa kukosa kazi?

CCM walitaifisha mashirika yote na kuyafanya mashirika ya UMMA. Madudu yaliyofuatia wenyewe mliyaona. Mashirika yote yalikufa. Majumba yote yalitaifishwa na kuitwa MSAJILI WA MAJUMBA.

Watanzania walinyimwa haki yao kujijengea nyumba. Hata waliojaribu kujenga walijenga mabanda kuepuka usumbufu  wa serikali ya CCM wakati huo ikiongozwa na Nyerere. Hata leo makazi ya watanzania yanatisha. Mashamba kama ya kahawa moshi yalitahifishwa na kufanywa mashamba ya Umma.

Wazungu waliokuwa wakiyamiliki mashamba hayo walitimuliwa na Nyerere akaweka Wazanaki wenzake wayasimamie mashamba hayo. Leo hii siyo mashamba tena bali ni mbuga ambazo hazina wanyama pori. Ajira ngapi za watanzania zilipotea kwa sera mbovu za CCM? Leo hii Mkapa anawatimua watanzania kwenye machimbo ya dhahabu MERERANI na kuwauzia Wazungu. Anadai kwamba watanzania hawana nyenzo za kuchimba madini. Watazipata wapi wakati tangu mwanzo walilemazwa na CCM wasifanye chochote katika nchi yao?

CCM wamejua mwisho wao umefika ndiyo maana wanauza kila kinachouzika wajiwekee akiba tutakapowavua madaraka. Wanajisumbua.

Mkapa anajitahidi kukusanya kodi na kuzidi kuwadidimiza watanzania walionyanyaswa na CCM kwa miaka arobaini. Kwangu mimi Mkapa hajafanya chochote Tanzania zaidi ya kuiuza nchi yetu kwa mabepari ambao watanzania hatuwezi kushindana nao kibiashara. Hii ni kutokana na sera za CCM zilizotangulia kuwadumaza watanzania katika kila kitu. Ndio maana tumegundua kwamba CCM ilishusha Jehanamu Tanzania, na tunataka mabadiliko Tanzania na tunayataka sasa.

   
Pope



Group: Members
Posts: 29
Joined: June 2003

Posted: Mar. 09 2004,13:54   

Munishi umeishiwa unapoint nzuri sana lakini hujui kuzijengea hoja huna jipya!!!! ninachoona kwenye thread zako ni kujipigia debe tuu, panda jukwaani tusikie vitu vyako, umeshindwa dini utaweza siasa bwana, siasa mchezo mchafu unaingia kwa kubebwa unatoka kwa kusukumwa, unachaguliwa na kutemwa kwa taarifa ya habari shauri yako tena kama fala fulani!!! hakuna mwanasiasa asiye muongo na wewe mtu wa Mungu utaweza kaka? ila naamini wapo wachungaji wasiowaongo kama unavyojiita (mchungaji wa familia yako tuu) maana sijui kwa upeo wangu mdogo ni kondoo wapi unaowaongoza. anyway tuko nyuma yako.

--------------
In GOD I trust!!

    
Tito-Mwiula



Group: Members
Posts: 131
Joined: Feb. 2004

Posted: Mar. 11 2004,01:45   

Stop dwelling in the past, Azimio la Arusha is the thing of the past. You can't keep blaming what Nyerere did 20 to 40 years ago for your failures today. There is no Azimio la Arusha anymore and Nyerere is dead. If you are poor today you only have yourself to blame and not Nyerere.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 96
Joined: Nov. 2003

Posted: Mar. 13 2004,17:00   


http//munishi.com

Yes Nyerere is DEAD, And Mkapa will die soon. Thats why we want CCM DEAD. Nyerere used CCM. Mkapa is  using it now to kill innocent Tanzanians. When I say CCM is the souce of all the problems we are facing in TZ it is true. We want it DEAD like Nyerere the founder. Thats when we will be free.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 96
Joined: Nov. 2003

Posted: Mar. 15 2004,15:18   


http://munishi.com/

Nyerere alikosea, na Mkapa bado anakosea

Serikali ya Tanzania inakosea kuuza mashirika ya umma kwa watu binafsi. Siasa ya ujamaa ambayo hatujaikana hadharani inakataza hilo. Wananchi wanapolalamika kuhusu soko huru wana haki ya kufanya hivyo kwani hawajatayarishwa kuingia katika mfumo wa soko huria.Wanachokijua ni mfumo wa kuingoja serikali iwafanyie kila kitu. Hata kuwatoza Watanzania kodi ni makosa. Kodi ni pato la ziada kutoka katika biashara. Kama watanzania hawajaingia kabisa katika ushindani wa kibiashara katika soko huria, kuwatoza kodi ni kuzidi kuwadidimiza na kuwafanya watoke kabisa katika huo UTANDAWIZI wa SOKO HURIA.

Unaitwa UTANDAWIZI yaani wizi uliotanda. Kabla ya kuwafundisha watanzania hu UTANDAWIZI, kuwalazimisha kuingia ndani yake ni sawa na kumtosa mtu asiyejua kuogelea baharini. Matokeo wote tunayajua. ATAZAMA. Watanzania tangu waingizwe kwenye soko huru, wanazama na hawawezi kupiga mbizi. Afrika ya kusini ndio wanaofaidi. Makampuni mengi ya kigeni yamechipuka, hata yanayouza mchicha kutoka Afrika ya kusini. Wakulima wetu hawana soko la kisamvu, kwani kisamvu kutoka afrika kusini kinauzwa kwenye maduka makubwa yaliyojengwa kisasa, tofauti na mchicha wetu ambao hutandikwa chini katika soko la kariakoo.

Bado hatujajua madhara ya mazao yanayokuzwa na kemikali nyingi, lakini subirini mtaona. Mayai ya kuku wa kienyeji anayejiokotea chakula chake mwenyewe ni bora kuliko yale ya kuku wa KISIASA. Nawaita wa KISIASA makusudi japo najua jina wanalotumia ni kuku wa GREDI . Siasa inaingia pale ambapo wanasiasa wanalinda maslahi ya wafanyibiashara, hata kama biashara yenyewe ina madhara kwa wananchi. Hapa ninalenga machungwa maembe vitunguu, nyanya na mazao yote kutoka South Africa. Yanalimwa katika mashamba makubwa ya MAKABURU, na wanatumia chochote ili wazalishe haraka kwa ajili ya biashara. Nasikia kwamba wenyewe wala hawawapi mifugo wao mazao hayo wachilia mbali kujaribu kuyatumia kama chakula.

Mkapa naye anatuambia ni UTANDAWIZI na amewaruhusu MAKABURU kujaza nchi yetu mazao ambayo kiafya siyo mazuri kwetu. Tukilalamika anasema sisi ndio hatujui maana ya soko huria. Hata kama tunajua UTANDAWIZI kuliko makaburu na Mkapa, haitaondoa ukweli kwamba hatuhitaji machungwa kutoka afrika kusini wakati Tanzania ina machungwa ya kuitosha na mengine yanauzwa KENYA. Afadhali nao Afrika ya kusini wayakubali machungwa ya BONGO kuuzwa CAPE TOWN. Pengine yanauzwa huko mimi ndio sijui. Lakini nina mashaka. Jamani! hata mchicha sasa unapatikana SUPER MARKET? tena siyo mchicha wa Tanzania, unatoka nje ya nchi. Sawa. Huo ndio UTANDAWIZI Mkapa na serikali yake wanataka tuupigie makofi.

Hapana hatuwezi kushangilia wakati tunaona wazi kwamba wananchi wanaumizwa na sera mbovu za serikali anayoiongoza Mkapa. Tanzania ina mali nyingi za asili lakini zote Mkapa amewakabithi wageni kwa kigezo cha SOKO HURIA. Madini ya Tanzanite hupatikana Tanzania pekee, lakini Kenya ndio waliopata zawadi kwa kuongoza katika kuyatoa mawe hayo. Kilichofanyika ni kwamba Tanzanite yote ilinunuliwa na Wakenya na kupelekwa kwenye soko la kimataifa kupitia Kenya. Siyo madini tu, hata mlima Kilimanjaro watalii wengi wanajua kwamba uko Kenya. Yaani kiutalii wenzetu Kenya wamejitangaza na sasa wanatangaza mlima Kilimanjaro pamoja na mbuga zetu za wanyama lakini wanasema ziko kwao. Masai Mara inajulikana kuliko Serengeti na watalii wanaposisitiza kwenda serengeti wanaambiwa waache kila kitu Kenya kwani huko wanakokwenda ni vichakani sana na watu wa huko ni wa ajabu sana wanaweza kuwaibia pesa na vitu vyao. Watalii wanapitishwa Namanga kwenda kuona mbuga zetu wakati matumizi mengi wameyatumia Kenya. Tena wanapita Namanga wakitumia gari la Kenya, ndani wana maji ya kunywa kutoka Kenya na watakacholipa Tanzania ni kiingilio kwenye mbuga za wanyama na kurudi kuimalizia safari yao Kenya. Mkapa hata hiyo anataka tumsifie kwamba sekta ya utalii ameiinua vilivyo.
Siyo nia yangu kukosoa kila kitu, lakini kukiwepo la kusifu nitasifu. Kwenye Serikali ya Mkapa na CCM sioni la kusifia na siwazuii wanaoliona kulisifia.

Kama kuwaua watu huko Zanzibar kunastahili kusifiwa basi mkapa apokee sifa kutoka kwenye gazeti la UHURU na MZALENDO na siyo kutoka kwenye gazeti la INJILI ninaloliandika mimi Munishi. Ikiwa kuwaruhusu Makaburu watuuzie hata mchicha nayo inastahili kusifiwa, basi nitamsifu nikiwa kaburini. Tena kama nchi inayoongozwa na mwandishi wa habari MKAPA ndiyo inayoongoza katika kuwanyanyasa waandishi wa habari, na mnataka tumsifie Bwana Mkapa basi kalamu zetu zimekataa kuandika sifa hizo. Ikiwa mnataka tumsifu Mkapa kwa kuingia kwenye mijadala ya Internet na kujiita BIG BOY Huku akiwatusi watu matusi ya nguoni ili wasitoe hoja za kumkosoa yeye na serikali yake, basi sifa hizo atazipata kutoka kwa wendawazimu kama yeye. Watu ambao hawalali bila kumwaga damu ya wananchi waislamu wasio na hatia. Wanatekeleza agizo la mabwana zao Amerika bila kujua lkwamba Marekani wana malengo yao ya kumiliki mali zote asili duniani. Waarabu ambao wengi wao ni waislamu wana kitu ambacho Marekani wanakimezea mate. Wanawaletea UTANDAWIZI ili wawaibie katika huo wizi uliotanda.

   
Tito-Mwiula



Group: Members
Posts: 131
Joined: Feb. 2004

Posted: Mar. 17 2004,01:43   

The government can't force people to buy something simply because it is made in Tanzania. Nyerere tried that and nobody liked it. What local businesses need to do is produce a better product than what's coming from abroad, have better marketing and people will buy their products. Also If South Africans have the know how and capital to utilize resources in Tanzania and in return provide meaningful employment to Tanzanians........then why not? Let them farm because Tanzanian farmers have failed, let them run these industries because Tanzanian CEOs have failed.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 96
Joined: Nov. 2003

Posted: Mar. 18 2004,18:36   


http://munishi.com/

Sina matatizo na watanzania kununua bidhaa kutoka nchi nyingine. Binafsi sinywi soda hata ya Tanzania kwani ni sukari na rangi. Lakini huwa nakunywa kinywaji hiki kutoka Kenya.

Je kufanya hivyo nahujumu watengenezaji wa soda Tanzania? Hapana natumia uhuru wangu kuchagua. Tatizo langu ni CCM kuharibu mazingira ya watanzania kufanya biashara.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 96
Joined: Nov. 2003

Posted: Mar. 19 2004,12:54   


http://munishi.com/

UONGOZI MBAYA WA CCM UMEWAFANYA WATANZANIA WASIIONE TOFAUTI YA UKOLONI WA WAZUNGU NA UKOLONI WA CCM AMBAO UNATUTAWALA HATA LEO.

Ni kutokana na uongozi mbaya wa CCM ndiyo maana watanzania tuko tulivyo. Hali yetu ya sasa inategemea historia yetu tangu tupate kile Nyerere alichokiita UHURU. Kwangu mimi hatujawahi pata UHURU mpaka CCM watoke madarakani.

Kwa Nyerere kujifanya kumtoa mkoloni ili yeye aendeleze ukoloni wa CCM, hakukuleta tofauti Tanzania. Ilikuwa sawa na kuruka majivu kukanyaga moto. Ndiyo maana tunasema kwamba CCM IMELETA JEHANAM TANZANIA. Yaani umasikini maradhi na ujinga bado ni maadui walioweka kambi Tanzania licha ya Nyerere na CCM yake  kujidai kupambana nao.

Tunataka mabadiliko ya kweli na Munishi amenituma Mungu niikomboe Tanzania. Sina mashaka na hilo ndiyo maana sioni haya kusema kwamba RAIS WA NNE TANZANIA NI MIMI

FAUSTIN STEPHEN MUNISHI.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 96
Joined: Nov. 2003

Posted: April 05 2004,15:32   


http://munishi.com/

Kwanza namshukuru Mungu.
Nashukuru kwa wote walioniunga mkono, na kukubali kunipa kura niwe rais wa nne Tanzania. Pia nashukuru kwa wote walionipinga. Lakini kwa kuwa nitakuwa rais lazima niheshimu uhuru wa wale walionipinga kwani sasa nitakuwa rais wao tu. Nitawatendea haki sawa na watanzania walioniunga mkono.

Sasa ni wakati wa kulijenga Taifa letu chini ya uongozi wa Mungu akimtumia mtumishi wake Munishi.
Mungu ibariki Tanzania.

18 The End


Page 1