14 Next Page   
  Topic: CCM IMESHUSHA JEHANAMU TANZANIA, HOTUBA YA MCHUNGAJI KWA TAIFA < Next Oldest | Next Newest >  
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Jan. 02 2004,12:55   


http://munishi.com/

MUNISHI SIKUWA NA SIYO PUNGUANI

Nilipoandika Post zangu pamoja na picha sikuwa punguani. Pia kuandika post ndefu ninafanya hivyo nikiwa na akili TIMAMU kabisa. Nilimkosoa UWAZI kwa sababu alikosea, na siyo ili nionekane najua kiingereza kuliko yeye. Kujua au kutokujua kiingereza hakunifanyi niwe nimeelimika au kutokuelimika. Inasikitisha kwamba kipimo cha elimu Afrika ni kujua au kutojua Kiingereza na Kifaransa. Kwangu huo ni upuuzi. Mbona wasomi wa Uingereza wasipime elimu yao kwa kukijua kiswahili? Kwa nini sisi?

Siyo kwamba siujui ukweli kwamba watanzania wengi hawana utamaduni wa kusoma post ndefu, Najua lakini nafanya hivyo kuubadili utamaduni huo.

Na katika hilo nimefanikiwa sana. Tayari magazeti fulani yameanza kutumia makala zangu kutoka ukumbi huu. Mengine yanataja mwandishi, na mengine hayataji. Lakini ujumbe unafikia walengwa. Pia kuna redio kadhaa nchini wameanza kusoma makala zangu katika ukumbi huu.

Mtu mwenye akili akikushauri kipumbavu ukausikiliza ushauri wake, unakuwa mpumbavu naye anabaki mwerevu.

Ndiyo maana naukataa ushauri wa BI LISHE kwa nia nzuri. Picha bado nitaendelea kutumia katika kuwasilisha ujumbe wangu hapa. Usijali kwamba picha zangu zina MAKOVU, hiyo ndiyo "IMAGE" yangu na siwezi kuwa mwingine.


Siyo lazima kila mtu aandike mengi nifanyavyo, Lakini nashauri kila mtu ajitahidi kuandika kwa ubora awezavyo kwani wanaofaidika na mijadala hii siyo wanabodi peke yetu. Inawasaidia wengi na msishangae utamaduni wetu Watanzania ukasambaa ulimwenguni kote kupitia ukumbi huu.

Neno lililoandikwa lina nguvu za kubadilisha mengi katika jamii. Internet ni chombo kizuri tunachoweza kukitumia kujibu mashambulizi mengi kutoka mataifa ya Magharibi. Msipochunga Utamaduni wetu waafrika utatoweka katika uso wa dunia. Nayajua matumizi ya Internet, na sijatumia hata robo ya yale Internet inayoweza kufanya katika maisha yetu.

Kuna watu waliofanya kisomi wakagundua Mtandao wa Internet, hawahitaji kujiita wasomi kwani tunapoutumia mtandao tunajikumbusha usomi wao. Inashangaza kuwasikia wengine wasiojua matumizi yake wakiwaonya wengine wasiutumie ipasavyo. TUWAPUUZE HAO.

Huwezi kumwambia RAIS MTARAJIWA aache kutumia picha katika kampeni zake za uchaguzi. Mimi ni Rais mtarajiwa, na wakati umefika kwa watu kama BI LISHE kuanza kunitambua hivyo. Siyo lazima waanze kuniita BABA WA TAIFA, lakini heshima siyo utumwa. Nipeni heshima inayonistahili.

Siyo vizuri kujipigia debe mwenyewe lakini hata mimi siyo kidogo. Mtu ambaye Nyerere alinitaka niseme kwamba nimemaliza shule darasa la saba nikakataa na kujiendeleza mwenyewe mpaka kiwango hiki nastahili pongezi. Siyo rahisi.
Wale waliokubali kwamba wamemaliza shule ndio ambao hawana utamaduni wa kusoma. Kwao walisoma ili wafanye mitihani. Walipomaliza mitihani na vitabu wakaweka chini. Ni wavivu sana kusoma. Hata hawaoni sababbu ya kufanya hivyo kwani shule walimaliza na wao ni wasomi.

Lakini wakimeza kiburi waulizeili picha ionekane hapa mtu anatakiwa afanyeje? Niko tayari kuwapa somo kuhusu "HTML" Lakini kwa kuwa ni wasomi, wako tayari kufa na tai shingoni wasije wakajidhalilisha hapa.

Kifupi mimi ni mhariri wa gazeti la injili kwenye Internet, najua sababu zinazoweza kunifanya nihariri post zangu. Kwanza ni nafasi, Na katika hilo sijatumia hata robo ya nafasi inayotolewa hapa kwa post moja. Pili tunahariri ili kutoa nafasi kwa matangazo ya biashara.

Nikipata wadhamini watakaodhamini posti zangu hapa itanibidi nihariri ili niwape nafasi ya kutangaza OMO na KIMBO yao hapa. Watapata nafasi nzuri sana ya kutangaza bidhaa zao kwani posti zangu husomwa na kusomwa mpaka watu wanasinzia bila kuacha kusoma.

Mpaka wasomaji wangu wananiomba nipunguze chakula kwani hawawezi kusema wameshiba waache kula. Yaani wanakula tuuu. Hata huo ni ushahidi nitakaoutumia kuwaonyesha wafadhili jinsi posti zangu zilivyo maarufu hapa.

   
Uwazi



Group: Members
Posts: 176
Joined: July 2003

Posted: Jan. 04 2004,06:34   

Quote (Binti Lishe @ Dec. 31 2003,13:40)
Huko nyuma mie nilidhani kwamba Munishi ni punguani, lakini kutokana na kumkemea na kukosoa kiingereza cha Uwazi nimegundua kwamba kumbe Munishi ana akili timamu kabisaa!  Sasa ndugu yangu Munishi kwa kuwa umeonyesha kuwa una akili timamu, tunaomba usikilize kilio cha wengi cha kufupisha maandiko yako na pia tunakuomba uache kutubandikia picha zako.  Imetosha!

People

Happy new year u all. People honestly speaking I'm seriously re-thinking about my contribution in this forum. My first impresion was that, this forum is a place where intellectual discussions take place. But to my disappointment it seems that this forum is for people who are intellectual lazy (sorry foy my sincerity) because of the high degree of intellectual laziness shown in this forum. It seem as if I'm in a wrong place and the bottomline is that; I can't belong to a bunch of ignorant people. So people if u don't read from me anymore, it is because of these reasons I've mentioned.

Imagine there is this lady Binti Lishe, eti alikuwa anamuona Munishi punguani, lakini baada ya Munishi "kunikosea" kiingereza changu amemuona ana akili timamu. What kind of thinking is that? By the way what Mr. Munishi did was copy and paste one of my msgs without even singled one mistake I made, sasa eti huyo Binti Lishe tayari ameshamuona ana akili timamu. If I ask her what specifically Mr. Munishi corrected me, it will takes all ages Binti Lishe to answer me. What I'm afraid most is that, next time Binti Lishe atatuambia kwamba tumpigie kura Mr. Munishi kwakuwa amemkosoa Uwazi kiingereza halafu Mr. Munishi atamuchagua mchapa kazi Magufuri kuwa waziri mkuu. Mind u that huyu Binti Lishe ni kiongozi wa UVCCM and u are still wondering why Tanzania is HIPC (Highly Indepted Poor Country) if the kind of leaders we're having is like Binti Lishe.

For Mr. Munishi stop ur day dreaming, u're uneducated person. Tanzania dont need a leader of ur calibre. U're unfit even to be a councillor let alone the president of United Republic of Tanzania. I swear before God if Mr. Munishi will become a president of URT one day, then I'll denounce my Tanzanian citizenship, I'll rather take a citizenship of another country, kuliko ku-accept humility ya kuongozwa na STD seven. I'm a man of proud.

If u dont believe me Mr. Munishi, wait and see, history will vindicate me, my simple advise to, u better stick on singing mapambio kanisani kuliko kuota ndoto mchana kweupe. Na kama utaendelea kutuma gabbage zako hapa kwenye bodi I'll quit this forum. There are many open fora where I can productive spend my time.

Sorry people, I'm kind of person who cant tolerate STUPIDITY

Uwazi

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Jan. 04 2004,07:04   

Uwazi,
Ninashangaa kuona kwamba ulikuwa bado kuona ukweli huo. Hapa ni kupotezeana muda tu kwa kusoma rubbish za huyu kichaa munishi, kwani hana mbele wala nyuma bali ni kabwela fulani hata kuandika shida leo anaota kuwa raisi wa Tanzania.
Nitaungana na wewe kuukana Utanzania pindi tu huyu chizi akichukua nchi, ni bora nikaombe ukimbizi Somalia ama Kosovo kuliko kubaki Tanzania chini ya Raisi Jambazi.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Jan. 05 2004,09:56   


http://munishi.com/

UWAZI UNAZIDI KUCHEMSHA
Kwamba sasa umeona uandike post ndefu ya kiingereza, hiyo inathibitisha kwamba kweli wewe huwezi kujieleza vizuri kwa kiingereza.  Yote hayo ya nini? Mimi mwenyewe nilikutetea kwamba hata kama uliharibu kiingereza hiyo siyo lugha yako. Ila ninaushangaa mtizamo wako kukihusu kiingereza. Kwako ni ishara ya usomi na unatutaka tukuone msomi kwa sababu unajua kutumia kiingereza. Hapo ndipo unapokosea.

Matisho yako kwamba msomi wewe hatutakusikia tena, na sababu ni kwamba umetuona wote hapa wajinga, yanaonja vibaya sana. Tena kusema kwamba utabadili uraia Munishi nikiingia madarakani huo ni wendawazimu. Ikiwa Mkapa alipowaua waislamu zaidi ya sabini Zanzibar hukubadili uraia, kwa nini ufanye hivyo wakati mtumishi wa Mungu Munishi atakapoiongoza Tanzania katika misingi ya haki? Kwako ni sawa Mkapa akiwaua waislamu, Mradi tu ana shahada ya chuo kikuu. Tena ni sawa Nyerere azifanyie majaribio sera mbovu za ujamaa Tanzania kwa sababu tu hakuishia darasa la saba.

Nyerere kosa lake kubwa lilikuwa kujiona msomi kuliko watanzania wote. Sera zake ziliiharibu nchi yetu Tanzania na UWAZI hakuukana uraia kwa makosa ya Nyerere. Kisa "MAKOSA YA MSOMI SIYO MAKOSA" ALikosea.

Siwatetei walioishia darasa la saba kuwa marais wa Tanzania, kwanza hawatathubutu kuwania kiti hicho. Kwangu kuthubutu kuwania urais Tanzania inaonyesha wazi kwamba kiwango changu kielimu ni zaidi ya darasa la saba. Hata kuweza kuitumia kompyuta na kuandika ujumbe hapa inahitaji elimu zaidi ya darasa la saba. Kwa hiyo mkubali mkatae Munishi elimu yangu ni zaidi ya darasa la saba. Ila kwa wale wanaotumia kigezo cha elimu kama mtaji wa kunipinga waendelee kufanya hivyo wakijua kwamba kiwango changu kielimu ni tofauti na wanavyonifikiria.

Ukumbi huu umegawanywa sehemu ya kiingereza na kiswahili. Kwako kuandika kiingereza sehemu ya kiswahili huoni kwamba unakiuka taratibu za ukumbi? Msomi gani ambaye hata taratibu za ukumbi zinakushinda? Kama una hamu sana ya kuandika kiingereza si ufanye hivyo mahali pake? Ukifikiri unatengeneza kumbe UNAZIDI KUCHEMSHA. Hata kwa hilo unataka tukusifie?  Watu sasa tumeijua sehemu ya pili ya uwazi. BI LISHE unamsakama wa nini? Yeye na wengine wengi katika ukumbi huu wameuona upuuzi wako ulioandika humu lakini hawakuambii. Siyo kwamba wanakuogopa, bali hawataki kuingilia uhuru wako wa kuamini kwamba kujua kiingereza ndiko kuelimika. Hata kama ingekuwa hivyo ndivyo, basi UWAZI hujaelimika kwa sababu hata kiingereza hukijui vizuri. Jitihada zako kutuonyesha kwamba unakijua, ndizo zinazotufanya tuwe na mashaka zaidi.

Waliponiona nimethubutu kukuambia hivyo usoni bila kuogopa una makaratasi kutoka chuo gani, Ndipo wengine walipodiriki kusema sasa wametambua kwamba mimi nina akili timamu. Nilikataa sifa zao, kwani sijawahi kuwa punguani. Kwa mtazamo wangu, pengine walikuchukulia msomi wa hali ya juu sana. Lakini mimi kwa kusoma posti zako wewe hujaelimika kama unavyotutaka tuamini. Ila umefuta ujinga tu. Lakini kama umeamua kuhama ukumbi huu, Nenda salama na uwasalimie uendako. Hata huko usishangae kuwakuta wajanja watakaokushitukia utapeli wako wa kuwataka wakuone wewe pekee ndiye msomi katika ukumbi huo. Kwa hiyo jiandae kuhama kila utakapoenda. Hata hapa ni afadhali kwani walikuwa wanausitiri uchi wako. Munishi ndiye niliyeshindwa kuvumilia upumbavu wako nikakuambia usoni. SIOMBI MSAMAHA KWA HILO.

   
Mkandaraha



Group: Members
Posts: 3
Joined: Dec. 2003

Posted: Jan. 05 2004,13:09   

Hivi kweli sisi wote hapa ni " bunch of ignorant people?"
UWAZI omba radhi kwa matamshi hayo.

Hatujali kama hutaandika tena hapa, wala hatuoni la maana sana uliloandika hapa zaidi ya kujidai.

   
MTANZANIAA



Group: Members
Posts: 13
Joined: Nov. 2003

Posted: Jan. 05 2004,13:25   

BWABWAJA JIULIZE
Kama kweli Munishi ni mjinga hivyo? Serikali inasumbuka nini kuizima kanda yake?

Wote waliojibu katika hoja hii nao wajinga? Basi hata UWAZI na Bwabwaja wamo katika ujinga huo.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Jan. 12 2004,10:51   


http://munishi.com/

DINI ISIWE KIGEZO MNINYIME KURA

Dini yangu isiwe kikwazo mninyime kura. Badala yake iwe kivutio michague kwa wingi. Watu wa dini zote mpeni nafasi Mungu aingilie kati uongozi wa nchi yetu. Mungu aliwekwa kando tangu mwanzo Tanzania. Kilichoongoza ni mawazo potovu ya Nyerere yaliyotaka kuchukua nafasi ya Mungu. Yalishindwa vibaya kwani mwanadamu hawezi kushindana na Mungu. Hata leo Tanzania mtajidanganya ikiwa mtairudisha siasa madarakani. Mambo yatakuwa mabaya kuliko awali. Kwani mmeonyeshwa njia na makusudi mkaikataa. Ni matumaini yangu kwamba watanzania wataitikia wito wa kumchagua Munishi kama rais wa kwanza kuchaguliwa bila kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa.

Dini yeyote ikitumiwa kuongoza nchi mafanikio huwa mengi. Watakaoyapinga ni waumini wa dini nyingine. Na watafanya hivyo kwa kutokuijua dini yao sawasawa. Mwinyi alikuwa mkweli kwa imani ya dini yake.Wakati wa uongozi wake misikiti mingi ilijengwa, mashule mengi ya kiislamu yalianzishwa, na wakristo wasioijua dini yao waliliona hilo kama tishio kubwa kwao.

Mafundisho kamili ya dini ya kiislamu ni kutenda haki kwa kila mtu, kutokunywa pombe, na mengine mengi. Ikiwa mtu wa dini nyingine atawafundisha watu kutenda hayo, mimi nitafurahi kwamba yale niliyotaka kuwafundisha watu, sasa yanafundishwa. Sitojali anayeyafundisha kama ni mtu wa dini yangu. Wakati wa Mwinyi watu walikuwa wacha Mungu sana. Uongozi wake uliegemea sana mafundisho ya dini aliyoiamini, jambo lililonifanya nami kuongeza bidii katika kumcha Mungu kutumia dini niliyoiamini. Na karibu kila dini iliyouona uislamu kama tishio wakati wa Mwinyi ilifanya hivyo. Hali hiyo ilipelekea Tanzania kama taifa kumcha Mungu kwa mioyo yao yote. Nini kingezuia baraka za Mungu kumiminika Tanzania? Zikamiminika baraka mpaka watanzania wakashindwa kuyaamini macho yao.

Sasa tuna Mkapa Mkristo  kwa jina kama alivyokuwa Nyerere. Anaiongoza nchi siyo kutumia misingi ya dini yake, bali porojo za siasa. Kwenye siasa uongo na ujanja ujanja ndivyo vinavyotawala. Nini kitawazuia watanzania nao kuwa waongo na wajanja wajanja? Wanayaona kwa viongozi nao wanafanya yayo hayo. Ndiyo maana rushwa, wizi, magendo vimeshamiri na vilishamiri wakati wa Nyerere na Mkapa. Sisemi wakati wa Mwinyi hakukuwepo na hayo, lakini si kwa kiwango hiki. Baba mlevi na mvutaji wa sigara hawezi kuwa na sababu za kutosha kumwelezea mtoto wake asilewe wala kuvuta sigara. Haijalishi sheria kali atakazojaribu kuweka, zitavunjwa zote. Makapa anaweka sheria kali kuwazuia watu wasifanye maovu ambayo yeye na serikali yake wanayafanya. Nani mjinga atii sheria hizo? Ndio maana utaona kwamba maovu badala ya kupungua yanaongezeka.


Imani ya Mungu ni suala la mtu binafsi na Mungu, lakini mtu huyo akiwa kiongozi haimuondolei haki yake ya kumwabudu Mungu kama dini yake inavyomfundisha. Hata akiwafundisha watu yale anayoyaamini kwa dhati kutoka moyoni mwake hafanyi kosa. Tatizo hutokea wakati kiongozi anapojaribu kuwabudu Mungu kwa kutumia imani ya dini zote. Hawezi , na haiwezekani ndio maana wengi huamua kusahau imanizao za kidini na kuitumia siasa pekee kuongoza. Kwa sababu siasa ni uongo, inashindwa kabisa kumaliza maovu nchini. Matokeo yake nchi inaongozwa kwa mbinu za nani kamzidi nani kwa kiwango gani cha uongo.

Ndiyo dini haiwezi kabisa kumaliza maovu yote, wala haitakiwi ifanye hivyo. Inachotakiwa kufanya ni kuwafundisha watu wawe waaminifu katika imani zao, na wawafundishe wengine kuyashika yale wanayoyaamini kwa hiari yao wenyewe. Kifupi tunataka nchi iwe na ushindani wa kumcha Mungu bila kulazimishana kufanya hivyo. Baraka amani, utulivu uponyaji, na  miujiza Mungu atakayoitenda maishani mwa mtu, ndiyo itakayokuwa changamoto ya kumfanya kila mtu awe na bidii ya kumcha Mungu kwa moyo wake wote.

Nchi inapokuwa na wacha Mungu wa kweli, ndipo kiwango cha maovu kinapoweza kupungua kama siyo kwisha kabisa. Lakini lazima ianzie kwa viongozi na hasa rais. Kiongozi akiwa mcha Mungu na siyo mnafiki, ni rahisi kuiambukiza nchi nzima. Siko hapa kuhukumu nani mcha Mungu na nani siyo, lakini nijuavyo mimi ni kwamba kila mcha Mungu atafanya kila linalowezekana kuwaelezea wengine yale anayofaidika nayo akiwa mcha Mungu. Ndiyo maana sioni makosa ya mwinyi kufanya mengi kuwasaidia waislamu wakati wa uongozi wake. Alifanya kama binadamu yeyote na hakuficha kama Nyerere alivyofanya kwa kanisa katoliki lakini kwa siri. Hiyo ni kuonyesha kwamba hakuwa na hakika na imani aliyoiamini ndiyo maana hakuthubutu kujionyesha hadharani kwamba ana upendeleo wa kidini. Pia hata hao aliowasaidioa hawakuweza kuitumia nafasi hiyo kumcha Mun\gu kwa dhati bali waliitumia nafasi hiyo kupata mali na viwanja vingi pamoja na waumini wengi ambao hawana msimamo na imani yao.

Waislamu na wakristo ni dini ambazo haziwezi kufutika katika uso wa dunia. Ni makosa na tena kupoteza muda kujaribu kutafuta misaada ya kuifuta dini nyingine duniani. Ni sawa na kujilisha upepo. Muhimu ni kila dini kuamka kutafuta nafasi ya kuongoza nchi. Wanasiasa wameharibu nchi kwani wao hupenda kuabudu vitu kuliko Mungu. Mimi ni mkristo, na sioni haya kusema kwamba nchi nyingi zinazodai kuwa ni za kikristo ndizo zinazoongoza katika maovu ya kila namna.Kosa lao ni moja tu. Kutokuruhusu viongozi waongoze sawa na imani zao kwa Mungu.

Kiongozi anapomcha Mungu na kutumia uchaji wake Mungu kuongoza, Mungu huongoza kupitia yeye. Na Mungu akiliongoza Taifa, nini kitakachomshinda? Kwa sababu wale wanaotuongoza siyo wachaji Mungu, mnajua wazi wanamcha nani. Vitu siasa, na shetani mwenyewe ambaye ndiye baba wa uongo wote. Mkiacha shetani aongoze nchi, kwa nini mnashangaa maovu wizi, rushwa na matambiko mengi ya kumwaga damu nchini? Hayo ndiyo matunda ya kazi za shetani. Tuungane dini zote kumwondoa shetani madarakani. Tanzania anatawala akitumia jina la CCM, lakini ni shetani mwenyewe.

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Jan. 14 2004,02:11   

Ya leo kali kama si chungu.
Munishi una maana CCM ni shetani ama CCM ni agent wa shetani?.Unaelewa unachokosema ama unasema kwa sababu unaweza kusema?. Fikiria kidogo na wala si sana kabla ya kuandika posting zako.

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Jan. 15 2004,02:59   

Kwako Munishi,
Wanabodi bado tunasubiri kwa hamu kubwa sana sehemu ya pili ya historia ya maisha yako, mbona hamna kitu bali blaa blaa tupu?.

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Feb. 02 2004,16:18   

Ndugu wanabodi,
Huyu kiumbe aitwaye Munishi yuko wapi mbona kimya kimezidi?
Nadhani kishaona kwamba hapa hapati mtu wa kumpa kura wala kumsaidia kupigia debe kampeni zake. Na hivyo ndivyo nilivyotaka.

14 Next Page