Munishi
Group:
Members Posts: 77 Joined: Nov. 2003
|
 |
Posted: Dec. 24 2003,18:46 |
 |
 http://munishi.com/
HERI NJEMA
YA KRISMASI NA MWAKA MPYA WENYE MAFANIKIO TELE
Mathayo 2:1-18
Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme
Herode, Tazama Mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona
nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. Basi Mfalme Herode
aliposikia hayo, Alifadhaika na Yerusalemu pia pamoja naye.
Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, Akatafuta
habari kwao Kristo azaliwa wapi? Nao wakamwambia, katika Bethlehemu
ya Uyahudi, Kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, Nawe
Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika wajumbe wa
Yuda. Kwa kuwa kwako atatoka MTAWALA atakayewachunga watu wangu
Izraeli.
7 Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani
akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota. 8
Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia mkaulize sana mambo ya
mtoto. Na mkiisha kumuona mniletee habari, ili mimi nami niende
nimsujudie.
9 Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika
njia na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, Hata
ikaenda kusimama juu ya mahali alipokuwapo Mtoto.10 Nao walipoiona
ile nyota walifurahi furaha kubwa mno.11 Wakaingia nyumbani,
wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye. Wakaanguka wakamsujudia,
Nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu, dhahabu na
uvumba na manemane. 12 Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto
wasimrudie Herode, Wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.
13
Na hao walipokwisha kwenda zao, Tazama, malaika wa Bwana alimtokea
Yusufu katika ndoto, Akasema. Ondoka umchukue mtoto na mama yake,
ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie, kwa maana Herode anataka
kumtafuta Mtoto amwangamize. 14 akaondoka akamchukua mtoto na mama
yake usiku akaenda zake Misri.15 Akakaa huko hata alipokufa Herode,
ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema.
Kutoka Misri nalimwita mwanangu.! 16 Ndipo Herode alipoona ya kuwa
amedhihakiwa na wale Mamajusi, alighadhabika sana. Akatuma watu
akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehem na viungani
mwake mwote. Tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule
aliouhakikisha kwa wale mamajusi.
17 Ndipo lilipotimia neno
lililonenwa na nabii Yeremia akisema.18 Sauti ilisikiwa Rama, Kilio
na maombolezo mengi.Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali
kufarijiwa kwa kuwa hawako. 19Hata alipofariki Herode, Tazama
Malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, 20
AkasemaOndoka umchukue mtoto pamoja na mamaye ushike njia kwenda
nchi ya Israeli kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.21
Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli. HILO
NI NENO LA MUNGU KAMA LILIVYOANDIKWA KATIKA KITABU KITAKATIFU CHA
MUNGU BIBLIA. AMEN.
Ndugu zangu wapendwa mabibi na mabwana.
Tunaposheherekea kuzaliwa kwa Yesu, ni muhimu tuyatafakari kwa
makini yote yaliyoambatana na tukio hilo. Kwanza ni furaha ya
Mamajusi walioongozwa na nyota hadi alikozaliwa mtoto Yesu.
Walifurahi sana, wakaanguka kumsujudia na kumtolea zawadi za dhahabu
uvumba na manemane.
Pili ni unafiki wa mfalme Herode
kuwatumia mamajusi hao hao kumletea habari za alikozaliwa Yesu. Siyo
kwa lengo la kufurahia kuzaliwa kwake ili amwabudu, bali alichukizwa
na alitaka ajue alikozaliwa ili amwangamize. Herode alikuwa
mwanasiasa. Ilimbidi awatumie mamajusi wamfanyie uchunguzi wa wapi
alikozaliwa Yesu kwa sababu askari wake wasingeweza kuufanya
uchunguzi huo. Suala zima lilikuwa la Kiungu, na lilihitaji
wataalamu wa nyota kujua wapi Mwokozi angezaliwa. Mambo ya Kiungu
kwa wanasiasa kitendawili wanachomhitaji Mungu awategulie. Lakini
Mungu hawezi kujichunguza mwenyewe ili ajiangamize. Mamajusi
waliitii amri ya Mfalme, na walikuwa tayari kufanya kama Herode
alivyotaka bila kujua madhara yake kwa Yesu.
Walifanya
vyote. Walimtii Mungu na pia waliitii mamlaka ya wakati huo kama
biblia inavyotufundisha. Lakini walipofikishwa mahali ambapo
ingewapasa kuchagua nani wa kutii kati ya mamlaka na Mungu, wao
walichagua kumtii Mungu kuliko Herode. Walipofika mahali ambapo
Mwokozi wetu Yesu alikuwa amezaliwa, mawazo yao yalikuwa wamrudie
Herode wampashe habari.Mamajusi hawakuijua nia ya Herode sawa na
tusivyojua nia ya dunia kusheherekea Krismasi kwa vishindo kila
mwaka. Kila mtu ana nia tofauti, na Mungu pekee ndiye anayejua nia
ya kila anayesheherekea kuzaliwa kwa Yesu Leo.
Lakini Malaika
wa Mungu aliwatokea katika ndoto na kuwaonya wasijaribu kurudi kwa
Herode. Waliijua hatari ya kufanya hivyo, lakini walimtii Mungu.
Hatua yao ilimkasirisha sana Herode, na ilibidi aamuru watoto wote
wa kiume kuanzia miaka miwili kwenda chini wauawe.
Jambo
lililopaswa kuwa la siri kati ya Mungu Malaika, Nyota na Mamajusi,
likamhusu kila mtu baada ya mwanasiasa Herode kuingilia kati.
Waliuawa watoto kutoka katika kila dini, ndiyo maana sishangai
Krismasi inaposheherekewa na watu wa dini zote. Tukio lililokusudiwa
kuleta furaha duniani, shetani akaligeuza likawa kilio. Nyumba
nyingi zililia kwa watoto wao wa kiume kuuawa kulingana na amri ya
Herode.
Pia usisahau kwamba Mungu alimwamuru Yusufu amchukue
mtoto pamoja na mamaye wakimbilie Misri. Na hii ni baada ya
kuhangaika siku nzima akitafuta nyumba ili mtoto azaliwe.
Ilikosekana Nyumba yenye nafasi kwa Mwana wa Mungu kuzaliwa, lakini
nyumba za anasa hazikosekani duniani. Ukiangalia kwenye TV yako
utashangaa Yesu anatafuta pa kuzaliwa na wengine wanavunja nyumba za
mamilioni ya pesa zianguke chini. Si bora wangeacha kwanza Mwokozi
azaliwe ndani na kama kuzibomoa wabomoe baada ya Yesu
kuzaliwa?
Mariamu ndiyo kwanza alikuwa amejifungua mtoto wa
Kiume kwa uwezo wa kiungu, lakini alijifungua kama wanadamu wengine.
Hapa ni mama aliyehitaji mapumziko, lakini ilibidi aanze safari ya
kuwa mkimbizi wa kidini Misri. Tena hapa ni mtoto ambaye ndiyo
kwanza ameingia ulimwenguni, na wazazi wanaanza safari usiku na
baridi kali jangwani. Sijui nisemeje hapo. Nani alikuwa akichanganya
dini na siasa hapo? Herode au Yesu mwana wa Mungu? Na je wakati huo
Yesu kule Misri angeitwa mkimbizi wa kisiasa au
kidini?
Krismasi ya kwanza ikachanganyika furaha na huzuni.
Pengine ndiyo maana kila mwaka wakati wa sikukuu ya Krismasi shetani
huangamiza watu kwa ajali barabarani.
Sitaki kumtukuza
shetani, ndiyo maana nasema kwamba wale wanaoongozwa na Mungu
wataziona hila za shetani na kuziepuka. Siyo lazima uumie na
kuhuzunika wakati kuzaliwa kwa Yesu kunamaanisha furaha ya kweli
moyoni. Ukiyajua yote hayo, utajijua wewe unaisheherekea
sikuku hii katika kundi gani.
Usijali kama tarehe 25 mwezi wa
12 ndiyo tarehe halisi ya kuzaliwa kwake, La Muhimu ni kwamba kweli
Yesu alizaliwa. Pia usijali jinsi watu ulimwenguni kote
wanavyosheherekea kwa nia na maana zao, bali jiulize wewe una nia
gani. Ikiwa nia yako ni ili umwabudu na kukubali afanye kile
kilichomfanya azaliwe, yaani azaliwe moyoni mwako awe Mwokozi
wako binafsi, una heri. Tumuombe Mungu atufunulie siri
iliyofichwa katika kuzaliwa kwa Yesu. Mwisho nawatakia Kismasi ya
fanaka, Pamoja na mwaka mpya wenye mafanikio. |