12 Next Page   
  Topic: CCM IMESHUSHA JEHANAMU TANZANIA, HOTUBA YA MCHUNGAJI KWA TAIFA < Next Oldest | Next Newest >  
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 17 2003,17:51   


http://munishi.com/

MATESO YA CCM SASA BASI

Watanzania tunataka mabadiliko. Tuanze ENZI MPYA BILA CCM


   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 17 2003,17:55   


http://munishi.com/

MATESO YA CCM SASA BASI

Watanzania tunataka mabadiliko. Tuanze ENZI MPYA BILA CCM


   
kobbs



Group: Members
Posts: 238
Joined: June 2003

Posted: Dec. 17 2003,20:51   

Munishi,
una maana gani unaposema tuanze maisha mapya bila CCM? una maana CCM kama chama ndio tatizo letu watanzania? yaani kufanikiwa kuiondoa CCM uchumi wa tanzania utakuwa kama wa sweden?. tunaomba uongee kama mgombea ambaye uko serious. tuambie mambo ambayo unataka kufanya ili kuibadilisha tanzania. chama ni jina tu, tunaweza kukibadilisha wakati wowote lakini tukabaki wale wale, unafikiri CCM leo ikibadili jina na kujiita DDM, tanzania itaendelea? kwani nchi zingine afrika ni maskini kwa sababu zinatawaliwa na CCM? mimi si mwanachama wa chama chochote na wala siitetei CCM na sera zake, lakini sikubaliani na hoja zako kwamba tatizo letu ni CCM, hizi ni hoja cheap sana na unaweza kuwauzia watu wasiosoma kabisa na nina hakika watanzania wanaoandika kwenye ukumbi huu wote ni wasomi wazuri, wanahitaji zaidi ya hapo. bila shaka tuna matatizo makubwa zaidi ambayo tunatakiwa kuyashughulikia. unatakiwa utwambie ni yapi kisha sasa usema CCM imeshindwa kuyashughulikia na wewe utaweza kuyashughulikia. hiyo ndio hoja unayotakiwa kuijadili. lakini sisi wanabodi tunachoshwa sana na kampeni zako zinazoambatana na posting zenye picha za rangi na maandishi makubwa yakiikashfu CCM na Nyerere tu bila kutoa input za maana. akina Nyerere walimpinga mkoloni, baada ya mkoloni kuondoka wakashindwa kuiendeleza nchi, wewe utafanyaje? tunaomba sera zako, acha kutu-patronize bure bila kuja na vitu ambavyo ni viable.

   
kobbs



Group: Members
Posts: 238
Joined: June 2003

Posted: Dec. 17 2003,20:52   

Yaaani enzi mpya bila CCM ni Munishi tu? hakuna watu wengine?

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Dec. 18 2003,03:41   

Kobbs,
Asante sana ndugu yangu kwa kuona ukweli kwamba huyu Munishi hana mpango wowote zaidi ya matusi na lawama tu.
Ni kweli kabisa kama ulivyosema kwamba tunahitaji atueleze atafanya nini ili kuikomboa nchi yetu toka hapa ilipo,vinginevyo anatupotezea muda na wakati kwa kusoma pumba zake kwa kuzipamba na mapicha makubwa ya rangi yanayoonyesha sura yenye makovu ya Munishi.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 18 2003,11:47   


http://munishi.com/

TATIZO LA TANZANIA NI CCM

Matatizo ya Tanzania ni CCM. Miaka arobaini madarakani, wameharibu kila kitu. Utalaumu nini Tanzania ukose mkono wa CCM?

Kichwa kuuma, husababishwa na mengi. Utakosea sana kununua "HEADACHE" kutuliza maumivu ya kichwa, kumbe macho ndiyo sababu kichwa kuuma. Bila kutibu macho, utajisumbua bure lakini kichwa bado kitaendelea kuuma, na kinaweza kusababisha viungo vingine mwilini kuuma.

CCM ndio chanzo cha matatizo yetu Tanzania. Hakuna marekebisho bila CCM kutoka madarakani. Utaanzia wapi?

Ni kweli kwamba CCM ni chama tu, na watu ndani ya chama hicho ndio waliotunga sera mbovu  zilizoipelekea Tanzania kuwa ilivyo. Sambamba na hilo, ndiyo maana tunataka KATIBA ibadilishwe ili  Munishi niingie madarakani  bila chama.

Ni katiba mpya ndiyo itakayotengeneza mazingara mazuri  ya watanzania kuongozwa kujiongoza. Na mtu tayari kufanya yote hayo ni mimi Munishi. Kama kuna wengine siyo kazi yangu kuwatafuta, wajitokeze hapa kwenye ukumbi huu wamwage siasa zao hapa. Mimi siyo mwanasiasa na sitarajii kuwa mmoja. CCM wakitoka madarakani baada ya katiba waliyoiharibu kurekebishwa na kuwa katiba ya wananchi iliyo na mawazo ya wananchi kwa ajili ya wananchi, kila kitu kitakuwa shwari. Uchumi wetu unaweza usiwe kama wa Marekani kwa mwaka mmoja, Lakini utakuwa ukielekea huko. CCM Kiini cha matatizo Tanzania kitakuwa kimetoka.

Huitaji kuwa msomi wa chuo kikuu kujua kwamba CCM ndio chanzo cha kila tatizo Tanzania. Lakini kama wewe ni msomi na hujagundua kwamba CCM ndio chimbuko la matatizo Tanzania, nakupa pole. Nchi masikini duniani haziongozwi na CCM, lakini Tanzania ilitokea kutawaliwa na CCM kwa zaidi ya miaka 40 na watanzania wana kila sababu ya kutaka CCM itoke kwenye maisha yao. Je itamaliza matatizo yao? Ndiyo. Wengine watafaidi matunda ya ukombozi, na kuna wale dhaifu ambao hawataishi kuonja matunda ya ukombozi. Lakini haitukatishi tamaa ya kujikomboa.

Gari ambayo mitambo yake ya kujaza betri moto ni mibovu, inahitaji mitambo mingine na siyo betri mpya. Ukikosea uweke betri mpya na yenyewe itamalizwa nguvu kwani mitambo ya kuijaza nguvu imekufa. Tanzania iliwekwa betri mpya yaani Mwinyi na MKAPA, na zote zimenyonywa  moto zikawa hazifai.
Ndiyo maana Tanzania inahitaji mitambo mipya  inayozalisha sheria na utengamano. Hii ni KATIBA MPYA itakayoketa uongozi mpya, utakaoleta ENZI MPYA, itakayoleta maisha mapya, yatakayoleta maendeleo, yatakayorekebisha hali ya uchumi wetu, utakaosababisha kila kitu kurekebika na kuwa jinsi ambavyo hakikuwa wakati wa CCM. Hata makovu ya Munishi usoni msishangae kuona yamerekebishiwa Muhimbili na siyo Uswiss kama anavyofanya MKAPA. Mmewahi kujiuliza kwamba MKAPA anatumia milioni ngapi kwa siku huko anakotibiwa? Msiombe kujua maana machozi yatawatoka.


   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 22 2003,12:35   



http://munishi.com/

ETI HAPA NI WASOMI TUPU?

Wimbo huu umenichosha, umerudiwa vya kutosha. Kama lengo ni kutisha, Sasa naona yatosha. KOBBS ndiye anayeongoza, kuimba wimbo husika. Eti hapa wanaoandika, ni wasomi wa kutisha. Mbona posti zao hazilingani na sifa zao? Mnataka kuwaingizia baridi wengine waogope kuandika hapa. Katika hilo hamtafanikiwa. Hakuna atakayekuja hapa, awe hajui kusoma. Na kama anajua kusoma kwa nini asiwe msomi?

Au msomi ni nani? Je yule anayeweza kutaja kila kitu kwa asilimia zake? Au ni yule anaweza kuandika hapa kwa lugha ya kiingereza? Nijulisheni nijue. Pengine ni yule ambaye posti zake zimejaa maneno ya kiingereza yakipishana na yale ya kiswahili? Au maana ya msomi hapa ni yule anayefumbia macho ukiukwaji wa haki za binadamu Tanzania? Pengine msomi ni yule anayeweza kuzitetea sera mbovu za CCM? Napata shida kupambanua, siyo vibaya mkanifahamisha. Hakuna unaloweza kulifanya bila kupewa darasa. Liwe popote ni darasa. Kwangu ni vigumu kupambanua nani hajapitia darasa lolote maishani. Nifahamisheni.

Kulingana na KOBBS, CCM ni chama kama chama kingine. Haoni haja ya kukibadilisha, kwani CCM siyo Tatizo Tanzania. Na yeye ni mmoja wa wasomi Tanzania. Inaonekana kwamba wasomi wengi wana mitizamo kama ya KOBBS. Kama hivyo ndivyo, basi CCM wapewe miaka mingine arobaini kuiendeleza Tanzania. Na baada ya miaka mingine arobaini Tanzania itakuwa imezalisha wasomi wengine wenye mitazamo kama ya wasomi wa leo, na hiyo ina maana kwamba CCM watapata miaka arobaini mingine ya kuitawala Tanzania. Na wasomi bado watakuwepo wakati huo watakaoamua sasa Tanzania imepiga hatua za kutosha, CCM iwape wengine waharibu waliyoyajenga kwa karne nne. Lengo zima la usomi na wasomi litakuwa limetimia.

   
kobbs



Group: Members
Posts: 238
Joined: June 2003

Posted: Dec. 22 2003,19:00   

Munishi,
kwanza nakuomba usanze kuwa na jaziba kwa sababu wewe ni mtumishi wa Mungu. lakini pia nakuomba sana usininukuu vibaya. bila shaka hii ndio tafauti kubwa kati yangu mimi na wewe. wakati wewe unaona CCM ndio tatizo letu kubwa na nchi haiwezi kufanikiwa bila CCM, mimi sioni hivyo kabisa. kuna makosa watu walishafanya yanayoyofanana na haya ya kwako. nimekupa mfano kwamba hata akina Nyerere wakati wanapigania uhuru walifikiri ili waendelee ni lazima wawafukuze wakoloni [kitu ambacho kilionekana ni kweli kabisa] lakini miaka 40 baada ya kuwafukuza tumeendelea kuwa maskini. ndio maana nikakawambia kuyaangalia matatizo ya tanzania kwa jicho la CCM tu ni kosa jingine kubwa, na wewe unaendelea kufanya kosa hilo. labda nikwambie wazi kwamba mimi ni mmoja kati ya watu wanaoamini kwamba kuna sera za CCM ni mbovu sana na ndizo zilizochangia matatizo tulioyonayo sasa. lakini si zote. kuna nzuri lakini zinawatekezaji wabovu na hivyo zinaonekana mbaya pia na kuna nzuri lakini hazitekelezwi kabisa na pia kuna matatizo mengine yanayotukabili wala hayahusiani kabisa na sera za CCM. ukiwa mgombea wa urais unatakiwa kuzielewa pande zote za shilingi na si upande mmoja tu.
Lakini pia ili tuwe na mjadala ambao ni productive, ni lazima tukubali kutafautiana inapolazisha hivyo. wewe unaweza kusema CCM ndio imeleta KIAMA, kisha mimi nikasema CCM kama chama haina uhusiano wowote na hicho kiama, bali viongozi wanaokiongoza na sera zao ndio KIAMA. kwani CCM ni nini? si kweli kwamba ni jina tu? je tukilibadili jina la CCM na kuita MUNISH GREEN PARTY, kisha rais wake akabaki kuwa ni Nyerere, Mwinyi au Mkapa na sera zao zikabaki kuwa zilezile tutapata maendeleo unayoyasema?. naomba bwana Munishi na wewe uondoke katika hilo boksi lako ulilojifungia ili uone mambo mangine ya kweli. Mimi sigombei urais, lakini nakushauri kama kweli uko serious na nia yako ya kugombea urais basi lazima uje na hoja ambazo zitakuwezesha kuwashawishi wapiga kura wako, na kitu hicho hakiwezi kuwa PROPAGANDA.
Umenishangaza pia uliposema wewe sio mwanasiasa na wala hutegemei kuwa mwanasiasa na bado unataka kuwa rais wa Tanzania! inawezekana kabisa, lakini haitakuwa mwaka kesho wala miaka 20 ijayo, kwa hiyo hutakuwa rais kwa sababu wakati mambo haya unayoyasema yatakapokuwa kweli utakuwa umeshakufa, au umesahau kwaba hata kwenye biblia imeandikwa umri wa kawaida wa watu kuishi hapa duniani ni miaka......
Kuhusu suala la usomi, nafikiri umeleta mjadala usiohitajika. mimi nilipinga kauli yako kwamba unafanikiwa kuwashawishi wajumbe wa ukumbi huu kuhusu hoja zako na kwamba kulikuwa na watu wacheche tu ambao walikuwa wanaonekana bado na ukataja mmoja wapo kama KOBBS. ndipo nilipokwambia ninayo elimu ya kutosha ya kuniwezesha kujua mbichi na mbivu kwa hiyo sihitaji kushawishiwa kwa propaganda bali naweza kuziona hoja za kweli zinazotolewa na mimi nikakubaliana nazo. una tatizo gani na hili bwana Munishi?. kumbuka kama wewe ni mgombea na una nia nzuri, utafaidika sana kwa kuchukua hoja za watu wengine kama challenge maana sasa unachofanya ni kama unajaribu kujijengea ukuta zaidi kwamba unachosema ndio cha kweli na hakiwezi kuwa na majibu yoyote mbadala kitu ambacho si cha kweli, au unatarajia kuupataje huu urais? kwa kuchaguliwa au kwa kurithi kama alivyofanya chifu MANGUNGO?

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Dec. 23 2003,03:44   

Kobbs,
Huna haja ya kushindana na Munishi hata kidogo kuhusu shule. Katika watu ambao hawakwenda shule acha kupita shule huyu ni mmoja wao.Haelewi nini maana ya shule na inafanana vipi.

   
Uwazi



Group: Members
Posts: 176
Joined: July 2003

Posted: Dec. 23 2003,05:41   

Quote (Bwabwaja @ Dec. 23 2003,03:44)


Kobbs

The problem with u is that, u're expecting too much from Mr. Munishi. What u're asking him to do is beyond his scope of comprehesion. Don't waste ur precious time with Mr. Munishi, on my side I've already dumped Mr. Munishi in the trush bin (sorry mr. Munishi for being BOLD to u).

What scares me most, is that some people here thinks that Tanzania problems will be fixed kama tutaongozwa na standards seven level, ambaye proffessional career yake ni kuimba MAPAMBIO kanisani.

HALLELUJAH for those who think that in this 21st  century a standard seven level will bring POSITIVE changes in Tanzania.

Uwazi

12 Next Page