11 Next Page   
  Topic: CCM IMESHUSHA JEHANAMU TANZANIA, HOTUBA YA MCHUNGAJI KWA TAIFA < Next Oldest | Next Newest >  
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Dec. 12 2003,02:34   

Munishi,
Kubali ukweli kwamba shule ni muhimu  katika maisha ya leo, upambanuzi na uelewaji wa mambo unategemea kwa kiwango kikubwa sana na shule uliyokuwa nayo. Na wanabodi wanataka kujua una kiwango gani cha shule acha kelele zako na porojo. Kubali ama kataa ni kwamba huwezi kuingia ikulu kwa uzoefu wa biashara za machinga na kuimba kwaya.
Munishi wewe ni mtu wa ajabu sana tena unasikitisha kwa kauli zako juu ya CCM na serikali tawala, umelelewa na CCM na serikali tawala na leo hii umekuwa milionea cha ajabu unageuka na kuanza kutukana ama mkono uliokulisha leo unageuka na kuanza kuupaka kinyesi.
Ninakuja Nairobi hivi karibuni kikazi na ni lazima nifike kanisani kwako nione unafanyeje kazi ya mungu kama si uwongo tu bali unafanya kazi ya shetani kwani unataka kuleta kosovo ndani ya Tanzania.
Katika posting zako inaonesha kabisa kwamba unachuki na serikali tawala kwa sababu zako binafsi za kibiashara na wala si kisiasa, wamekuzuia kuuza kanda zako zenye nyimbo za uchonganishi na imekuwa nongwa.
Jina langu kamili ni Bwabwaja Ahmed Bwabwaja na ninatumia jina hilo hapa  sina cha kuficha kama wewe unavyotumia jina lako kamili labda mimi sijaweza kutoa picha yangu katika bodi hii  kwani sioni umuhimu huo.
Mpaka sasa hakuna kitu cha maana ulichoweza kuwaeleza wanabodi kwanini unataka kuwa raisi zaidi ya kumwaga lawama tu kwa CCM na serikali tawala kama vile hakuna hata kitu kimoja kizuri kilichofanywa na CCM na serikali tawala.
Munishi, kuwa kiongozi wa watu kunataka hekima, uchambuzi wa kina, uzoefu na kutokuwa na jazba na ninavyokuona wewe wala usijisumbue hata kidogo kuwania kiti cha uraisi wa Tanzania na wala ujumbe wa nyumba kumi, bali endelea kuimba nyimbo zako huko ukimbizini Kenya.

   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Dec. 12 2003,08:48   

Quote (MTANZANIAA @ Dec. 10 2003,16:08)
HONGERA Munishi

Kina Bwabwaja na wenzake Mizambwa ambao wanaonekana kama maadui leo, Munishi anaweza kuwahitaji huko aendako wamsaidie kuunga mkono hoja yake. Wanasema katika siasa hakuna adui wa asili. Adui leo anaweza kuwa rafiki kesho. Pole Lakini Munishi hayuko kwenye chama cha kisiasa kwa hiyo yote asemayo hapa ni dini tupu.

Hata kwa mtutu na mabomu bado hamjaninpata katika ULONGO wenu wew na Munishi. Sijaona point ya maana iliyotolewa, unapomlaumu au kumchukia mtu yeyote na bila kutoa sababu za msingi; hapo lazima utaonekana umepungua ama BOLT imelegea kichwani. Toa sababu za msingi.

Serikali ni mimi na wewe. Tutakaojenga nchi ni mimi na wewee. Tunaovunja nchi kwa sasa ni mimi na wewe. Kwa hiyo huwezi kujitoa hata kidogo.

Viongozi wa Serikali wanajitahidi kuyaweka maisha ya Watanzania wote yawe nafuu  kwa kupunguza mfumuko wa Bei za Bidhaa, lakini mimi na wewe hatulioni hilo.

Ndugu MTANZANIA, pamoja na MUNISHI nawaomba ili tuwaelewe na tujue kuwa mna nia ya kuwakomboa Watanzania, kwanza fuateni nyayo za UPINZANI wa Mh. Mrema anazofanya kwa sasa. Saidieni Serikali katika kupunguza Kero mbali mbali kwa Wananchi siyo kutuletea MANENO YA MAHUBIRI HATUPO KANISANI HAPA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Tunahitaji vitendo ili tujue kweli mnayoyasema siyo MAHUBIRI.

Hizo kelele za kubadilisha Katiba hazitatusaidia chochote sisi wananchi, zitawasaidia nyiee Wanasiasa. Hivyo msituambie chochote kuhusu mambo ya Katiba maana naona ndiyo mmeifanya kuwa hoja ya kutupotezea muda wetu hapa. Tunahitaji hoja za kujenga Wananchi siyo kujenga matumbo yenu!!!!!!!!!!!!!


INANIUMA SANA!!!!!!!!
Jina Kubwa

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Dec. 12 2003,21:06   

Asante sana ndugu Mizambwa kwa kuona ukweli katika hili jambo. Huyu kiumbe aitwaye Munishi hana sera hata kidogo bali ni lawama na matusi matupu na cha kusikitisha ni kwamba anatumia injili kutukana na bila aibu anajiita mchungaji.
Nimejaribu sana kumweleza Munishi hapa si mahali pa injili kwani hapa si kanisani na kama anataka kumwaga injili aende kanisani ama jangwani. Hana sera za maana anazomwaga ili aweze kuwashawishi wananchi kwamba anafaa kuwa raisi bali kila asemacho ni pumba tupu na uchonganishi mtupu kwa nia ya kumwaga damu ya Watanzania tokana na yeye kuwa Kenya ukimbizini (Asylum).
Munishi eleza sera zako kwa wananchi ueleweke si rahisi kukupa nchi bila ya kueleweka, acha matusi, jazba na uwongo. Na bila kusahau endelea kueleza historia ya maisha yako kwa ukweli kwani kuna mambo hukuelezea hapo nyuma wakati unatoa sehemu ya kwanza ya historia yako na mimi Bwabwaja ninasubiri umalize ili nibwabwaje ukweli kuhusu maisha yako kwani ninakufahamu vizuri sana.

   
aawakil



Group: Members
Posts: 22
Joined: July 2003

Posted: Dec. 13 2003,02:39   

Ndugu Munishi,

THE FOLLOWING IS AN ARTICLE FROM THE GUARDIAN NEWSPAPER(IPP MEDIA) WHICH APPEARED ON SATURDAY DEC 13/2003

By reading the following article it looks like CHADEMA is more serious on this issue of dual citizenship than CCM. Chadema has a much more broader view and wants to do whats best for the country.









CHADEMA for dual citizenship



Saturday, December 13, 2003 .

By  Ludger Kasumuni

The opposition party, CHADEMA, has said if it comes to power, it will legalise dual nationality to enable foreigners marrying Tanzanian women to be granted citizenship.
Speaking in Dar es Salaam yesterday, the Vice-Chairman of CHADEMA, Dr Wilbrod Slaa MP, said that by allowing people to acquire nationality status of two countries, would not only guarantee gender equality, but also attract investment.
“The provision of dual nationality in the immigration law is important for our country to adopt, because many African countries have legislated it. In Kenya, there is discussion going on. Ghana has adopted it,” Dr Slaa said in a party forum for policy review.
Dr Slaa, who is also the Acting Party Secretary General, said many investors are not ready to come and put long-term investment in the country, because of the existence of immigration law against dual nationality.
“This issue was also brought in parliament by some legislators, but the government of CCM is yet to support it,” said Dr Slaa, who is Member of Parliament for Karatu.
On his part, the former Chairman of CHADEMA who chaired the forum, Edwin Mtei, said for the sake of maintaining gender equality, it was imperative to allow the non-nationals who are the husbands of female Tanzanians to get nationality status.
Under the current immigration law, foreigners who marry Tanzanian women are not granted nationality status, but they just live through special permits or visa.
Earlier, a senior lecturer of political science at the University of Dar es Salaam, Prof. Daudi Mukangara, said that the decision of CHADEMA to hold dialogue for policy review was important for the opposition party to win more electorate.
According to him, party policies were important for making the party stable, popular and more predictable.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 13 2003,13:33   



MSINGI MBOVU WA NYERERE TUTAUBOMOA

http://munishi.com/

Suala la wanawake wa Tanzania kuolewa na raia wa nje siyo tatizo. Mradi nia iwe walipendana siyo kisingizio cha kupata uraia. Hiyo itakuwa kazi ya idara ya uhamiaji  kujua.  Natilia maanani kubadilishwa kwa katiba kwani ndiyo itakayowawezesha wananchi kutoa maoni yao jinsi wangependa waongozwe. Porojo za vyama vya kisiasa huwa lengo lake ni kupata kura waingie madarakani. Wakishaingia msishangae wakifanya vinginevyo. Sitaki kuwatapeli wananchi wa Tanzania nitafanya hili na lile. Kazi yangu ni kuwaonyesha makosa ya serikali iliyotangulia ili wakati wa kuibadili katiba waondoe vipengele vilivyowakandamiza.

Mfano msingi aloujenga Nyerere Tanzania lazima tuubomoe. Haufai, na ni makosa kuendelea kujenga juu ya msingi mbovu.

Sina matatizo na watu waliomuogopa Nyerere, au tuseme waliompenda kwani ilikuwa haki yao kufanya hivyo. Kwetu sisi ambao hatukumuogopa, tunajisikia kuonewa kama hatutapewa nafasi ya kujadili yale yaliyotufanya tusimuogope Nyerere , japo wengine wanatuelewa vibaya kwamba hatukumpenda Nyerere.

Hata kama tungempenda Nyerere kuliko wakereketwa wake, isingekuwa sababu ya kutetea hata yale Nyerere mwenyewe aliyokiri kushindwa. Huwezi kumpenda mtu zaidi ya alivyojipenda mwenyewe. Watanzania wengi wanajidanganya kuwa walimpenda Nyerere kiasi cha kuyapenda mpaka yale ambayo Nyerere mwenyewe aliyachukia. Huo siyo upendo tena mnisamehe nikiuita wendawazimu.

Nyerere anaitwa mwanzilishi wa taifa la Tanzania sina utata hapo. Msingi alioujenga na baadaye akakiri kushindwa ndio ninaotaka tuujadili hapa.

Tukitilia maanani kanuni za ujenzi kama anavyotueleza mtaalam wa mambo ya ujenzi.

Katiba ni MENU ya msingi wa nchi. Ndiyo inayosema msingi ulichimbwa kiasi gani na unaweza kubeba ghorofa ngapi kwenda juu.Pia inatueleza kokoto saruji na mchanga zilichanganywa sawa au la. Ukiisoma katiba utajua ni kwa nini nyumba hii tunayojaribu kuijenga ina nyufa kiasi hicho na ni karibu kuanguka.

Ikiwa tumeisoma katiba ituambie kila kitu kiliwekwa sawa halafu tukijaribu kuongeza ghorofa inaporomoka, Kitaalam tunamwita mhandisi wa kwanza atueleze kama kweli msingi ulijengwa sawa na Katiba inavyosema akisema ndivyo tutamuuliza mbona nyumba ina nyufa? Aseme sijui muulizeni mhandisi wa pili maana mimi niliweka msingi na kujaribu kuijenga kwa miaka zaidi ya 30 ikanishinda nikampa Mhandisi wa pili.

Kitaalam hatutachoka ila tutamwita mhandisi wa pili na tumuulize vipi mbona pamoja na "ruksa" nyumba bado ilikuwa na nyufa? Aseme Nilimwambia mhandisi wa kwanza msingi ulichimbwa vibaya kwa hiyo ilitakiwa uende chini mpaka ufikie MWABA. Na kwa sababu msingi uko kwenye jiwe jepesi linaloitwa ujamaa na kujitegemea bila Mwamba ambao ni Mungu ndio maana nyuma haikosi nyufa. Nilimwambia tuvunje nyumba na tuchimbe msingi upya akaninyooshea kifimbo na kuniambia thubutu!!! Mhandisi wa pili aendelee kusema alijitahidi hivyo hivyo kuziba nyufa na kuendelea kujenga lakini aliruhusu vijengo vingi vya chini ili kuepusha kuporomoka kama angeendelea kujenga kama mhandisi wa kwanza alivyotaka ajenge. Amalize kwa kusema jitihada zake za kujaribu kurekebisha hazikumaliza nyufa, na kwa sababu ya kujaribu kutumia akili yake ili kuiokoa nyumba isiporomoke walitofautiana na huyo mhandisi wa Kwanza aliyemwambia kuwa ameigeuza ikulu yka kuwa mahala pa biashara. na isitoshe anaongozwa na mwanamke. Kwa hasira huyu mhandisi wa pili alimjibu kuwa huwezi kunitukana matusi ya nguoni. Nyumba uliiharibu wewe na ulisema wazi kwamba ulikosea, ukaniita niirekebishe, na tayari nimekuambia inataka nini ili irekebike, na wewe hutaki niirekebishe bila ruksa yako. sasa mawili chukua nyumba yako uendelee kuijenga mwenyewe.


Kama Nyerere alikosea, tukisema inawauma nini? Makosa ya mtu ni makosa hata kama mwenyewe alikufa. Kwamba sasa hayuko duniani ndio wakati mzuri wa kujiuliza kwa nini alikuwepo, na dunia ilipata faida gani kuwa naye. Na sasa hatunaye, dunia ina pengo gani kumkosa ? Tamzania na dunia nzima haina pengo kumkosa Nyerere bali inapumua kwamba mwiba mguuni umetutoka. Nyerere hakuwa na haya kuutetea uongo ufanane na kweli. Nje kwenye vyombo vya habari alijionyesha kama mpenda haki na mpigania uhuru, lakini kwa ndani alikuwa akifanya kinyume chake. Huwezi kuwa mpigania haki wakati unawanjima watanzania haki ya kuyatoa mawazo yao. Ndivyo alivyofanya Nyerere, na kuna watu wanauita huo ni uzalendo. Kwao uzalendo ni kuwaweka watu kizuizini na kutunga sheria ya kuwashitaki wakati wako kizuizini.

Je nimsifu Nyerere? Ndiyo nitamsifu. Alikuwa KIONGOZI. Sifa ya kuwa kiongozi siyo lazima iambatane na MZURI. Katika hili Nyerere alikuwa KIONGOZI MBAYA. Ubaya wa Kiongozi siyo lazima uwe kwenye sura na maumbile, japo wako wengine wa hivyo. Sera za Nyerere za ujamaa na kujitegemea ndizo zilizokuwa mbaya. Akaambiwa sera ni mbovu, naye akautumia uongozi wake na sura na maumbile yake ya kuvutia kuzitetea sera zake mbovu mpaka zikaiharibu Tanzania. Kwamba aliweza kuzitetea sera zake mbovu kwa mbinu na hila zote hizo ndizo sifa zinazomstahili. Binafsi sioni sifa nyingine ya Nyerere.

Mbinu mbaya ambayo inanifanya nitamani kwamba mifupa yake ipelekwe gerezani, ni hii ya kuhakikisha kwamba Tanzania inabaki bila KIONGOZI kwa miaka mingi baada yake.Alitengeneza wale aliowaona wanafaa kuiongoza Tanzania baada yake na akahakikisha siyo viongozi. Kiongozi ni yule anayeweza kutengeneza njia mpya, na ikakosa mahali pa kutokea, na akarudi akatengeneza nyingine. Kifupi ni kwamba kiongozi ni yule anyedhubutu kuanzisha kitu kipya. Tanzania tulikuwa na Nyerere akaanzisha kitu ambacho hakikuwa kipya sana, ila alikipaka rangi kionekane kama ni chake. Kilipokwama hakuwa na ujasiri wa kuanza kingine mapema, bali alipoteza muda wa WATANZANIA kuyatetea mawazo mabovu. Alipomwachia Mwinyi, hakumwacha naye aanzishe kitu kipya kama kiongozi, bali alimtaka afuate nyayo zake ambazo zilikuwa zikielekea porini bila matarajio ya kuyafikia malengo. Mwinyi alipojaribu kufuta nyayo na kuandika zake, Nyerere alimkemea hadharani kana kwamba siyo yeye aliyemweka madarakani. Sasa tuna Mkapa aliyewekwa na huyo huyo Nyerere, lakini kwenye ramani ya dunia ni kama TANZANIA haiko. Nchi ikikosa kiongozi huwa haisikiki kwa shari wala kwa kheri. Tanzania kwa sasa haina kiongozi, na ikiwa wananchi hawatafanya mageuzi ya kweli, tutabaki bila kiongozi na sijui ni kwa muda gani.

Mkapa siyo kiongozi kwani kwa miaka kumi hajaanzisha kitu Tanzania kilichoshindwa wala kufanikiwa. Yuko tu. Hajulikani yuko upande upi. Tunajua kwamba yeye ni mkomunisti kama aliyemuweka madarakani, lakini hataki kujionyesha wazi kulingana na wakati huu wa soko huria.  Kutokana na hali ya nchi yetu kukosa kiongozi, pia inakosa sera. Watanzania hawawezi kuonyesha kwamba hii ndiyo sera yetu kama nchi. Yaani tuko tuko tu.

Wakati umefika kwa Watanzania wenyewe kujichagulia KIONGOZI wa kuwaongoza na siyo mtawala wa kuwatawala. Wafanye hivyo haraka kabla nchi yetu haijafutwa katika ramani ya dunia. Ni jambo gumu linalohitaji baraka za MAULANA RABUKA kuliwezesha. Watanzania wote ni waumini wa dini mbali mbali jambo litakalopelekea zoezi zima kuwa rahisi kuliko tulivyotegemea. Kila mmoja katika madhehebu ya dini yake amwombe Mungu atupe kiongozi atakayetuongoza kuyafikia maendeleo hapa duniani, na baadaye tuingie kwenye ufalme wake wa milele mbinguni.

   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Dec. 13 2003,15:55   

Ndugu Munishi mimi binafsi nimeshachoka na MAHUBIRI YAKO. Huna cha maana unachotueleza kila siku ni kelel za Katiba.

Je, sisi wananchi inatusaidia nini. Tuambie vitu vya maana na siyo MAHUBIRI.  Anza kuonyesha vitendo katika vitu vya kutuletea maendeleo, inaonyesha kuwa wewe hata ukichaguliwa utakuwa na MAHUBIRI yasiyo na utekelezaji. Huna lolote la maana katika maendeleo. Miaka yote mitano utakuwa unarekebisha Katiba!!!!!!!!!!!!!!!!!

NASEMA HIVI; TUMECHOKA NA KELELE ZA KATIBA. YAONYESHA DHAHIRI HAUFAI.

Mimi binafsi nimechoka katika kuchangia mada hii.

KWAHERINI NAHAMIA MADA ZINGINE ZENYE MAANA!!!!!!!!!!

SAMAHANI SANA KAMA NILIWAKWAZA KATIKA MADA HII. NDIYO MAANA YA MJADALA.

ASANTENI SANA KWA USHIRIKIANO KATIKA MADA HII.

INANIUMA SANA !!!!!!!
Jina Kubwa

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 13 2003,16:54   



Watakuja na mioto wataondoka wamejiinamia kwa huzuni. Kwao elimu ni kujua lugha ya kiingereza. Wanasahau hata hapa tunasoma. Shule wao walimaliza, na wanajiita wasomi. Wamendanganyika. Ukisoma wanayoandika hayafanani na shahada wanazodai kuwa nazo. Elimu yao inatiliwa mashaka.

Kwao mahali pekee pa kupata elimu ni darasani. Ni watu wa ajabu sana. JKT iliingiza baridi kwenye bongo zao. Ni sawa na breki za gari zilizoingiza hewa ndani. Ukikanyaga ukifikiri una breki utashangaa. Gari haisimami. Lazima utoe hewa kwenye bomba linalopitisha mafuta ya breki ndipo gari yako iwe na breki. Nyerere aliingiza hewa katika bongo za wasomi wetu akitumia JKT. Alibaki mwenyewe mjuzi wa kila kitu. Siyo ajabu waliimba ZIDUMU FIKRA ZA NYERERE. Walikuwa sawa. Nani mwingine aliruhusiwa kufikiri Tanzania?

Woga ndio uliotawala mawazo yao. Hawawazi kingine isipokuwa CCM aliyoanzisha Nyerere na sasa imezeeka. Sera za ujamaa ziliharibu Tanzania na CCM haifai kurudishwa madarakani.  Sisi tunasonga mbele. Enzi mpya Tanzania ni lengo letu. CCM sasa basi. Tuna hamu ya kuiona Tanzania mpya bila CCM. Tanzania ni mali yetu watanzania na siyo mali ya CCM na Mkapa.

Nchi ya Tanzania ni mali ya watanzania wote na siyo ya Mkapa na CCM kama inavyoekea kuwa.Vitendo vinavyofanywa na serikali ya chama tawala CCM vinaonyesha wazi jinsi wanavyofikiri kuwa Tanzania ni mali yao.

Kwamba serikali inaweza kuwaua raia wake kwa sababu wana mawazo yanayotofautiana na chama tawala, siyo tu ni kinyume na haki za binadamu, bali ni wendawazimu uliochanganyika na upumbavu wa hali ya juu.

Nauita upumbavu kwa sababu ni afadhali ungekuwa ujinga ambao unaweza kutoka wakati mhusika anapoelimishwa. Lakini kwa kuwa yalifanywa na watu wanaojiita wasomi tena wa vyuo vikuu, basi yanakuwa ya kipumbavu maana hatujui wahusika wataenda chuo gani tena kuelimika ili wajue kuwa katika dunia tunayoishi ni vigumu watu wote kukubaliana kimawazo, hata kama mawazo hayo yanatoka kwa Rais wa nchi.

Matata na chokochoko zilizoko duniani mara nyingi huanzishwa na watu wanaojifanya kujua kila kitu, na kumbe hawajui kwamba hawajui. Na Tanzania tuna Mkapa anayejifanya kujua kila kitu na kumbe hajui impasavyo kujua. Matokeo yake ni kwamba Tanzania itaigizwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo havijawahi kuonekana popote duniani.

Nasema itakuwa vita mbaya kwa sababu karibu kila mtu Tanzania amepitia mafunzo ya kijeshi, kosa alilolifanya Nyerere akifikiri kila mtu anapokuwa mwanajeshi ni rahisi kumtawala mtu huyo.

Jeshini hawaulizi maswali, bali wanatii amri. Ni kigezo hicho ndicho kilichomfanya Nyerere aamini kuwa watanzania wakipata mafunzo ya kijeshi watakuwa na nidhamu, na itakuwa rahisi kuwatawala. Alifanikiwa kuwatawala watanzania kwa karibu miongo miwili bila ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Siyo kwamba Tanzania haikuwa na matatizo, lakini alijua nini cha kufanya yanapojitokeza tofauti na anavyofanya Mkapa ambaye anafikiri kila tatizo linatatuliwa kibabe na kutumia nguvu za dola.

Watanzania aliowatawala Nyerere ni wale wale Mkapa anaoshindwa kuwatawala, tofauti ni kwamba Nyerere aliweza kuwaibia watanzania bila wao kujua, wakati Mkapa anawaibia waziwazi. Nyerere alikuwa akigundua wananchi wamemshtukia anawaomba msamaha wa geresha wakati mkapa anamwamuru mkuu wa Polisi awashughulikie wote wanaokuwa na mawazo tofauti na chama tawala. Nao Polisi kama 'Robots' na bila kutumia ubongo wao wanawamiminia risasi za moto ndugu na dada zao watanzania na kusababisha vifo ambavyo idadi yao haitajulikana kamwe. Serikali inasema ni watu 23 tu, wakati chama cha upinzanini CUF ambacho ndicho kilichoadhirika kwa wanachama wake kuuawa kinasema watu zaidi ya 300 waliuawa kinyama na mamia kujeruhiwa huku maelfu wakiwa wakimbizi wa kisiasa Mombasa Kenya kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ipate uhuru. Na yote hayo yamesababishwa na utawala wa kimabavu wa dikteta Mkapa.


Mkapa aliamuru mauaji ya kutisha Zanzibar, na kufuta jina la Tanzania kuwa kisiwa cha amani. Mwenyewe alikiri kwamba Tanzania imegubikwa na doa kubwa jeusi.

Kinachoshangaza na kogopesha siyo idadi ya watu waliokufa, bali tumefikia mahali ambapo Polisi wa Tanzania wanatumia bunduki zilizonunuliwa na watanzania kuwaua watanzania. Mbaya zaidi ni kwamba karibu watanzania wote waliokufa dini yao ni ya Kiislamu jambo linalolielekeza tatizo lenyewe kuwa la kidini zaidi kuliko kisiasa. Siyo kwamba likiwa la kisiasa pekee ni rahisi kulitatua, maana sidhani Tanzania ya leo kuna mwanasiasa anayejua siasa za kutosha kulitatua. Mkapa ni mtoto asiyekua kisiasa na siyo makosa yake.

Nyerere baba yake kisiasa hakutaka akue ili awe anamnywesha maziwa ya kisiasa kila siku. Alifikiri angekuwepo mpaka azaliwe mtoto mwingine ambaye naye kama Mkapa, mpango ulikuwa kwamba asiruhusiwe kukua bali aendelee kupewa maziwa ya kisiasa sijui ingekuwa mpaka lini.

Lakini alisahau kuwa mwanadamu hawezi kuishi milele duniani, ila mbinguni au motoni ndiko watu wanakoishi milele.

Mungu alipoamua kumchuku Nyerere {na sijui alimweka wapi,}Ndipo mambo yalipoanza kumharibikia Mkapa. Kama mtoto yatima kisiasa, hakujua aanzie wapi amalizie wapi. Ninasikitika kusema kuwa mpaka sasa Mkapa amechanganyikiwa kisiasa. Wanaojifanya kumshauri ndio wanaoharibu zaidi. Inavyoonekana hatujui ni nani hasa anaeiongoza Tanzania kati ya Mboma mkuu wa majeshi, Maita mkuu wa Polisi, na Kingunge Nguoyambali Mwiru mshauri mkuu wa Mkapa.

Habari kutoka vianzio vyetu zinasema kuna uvutano mkubwa kati hawa watatu kila mmoja akidai kuachiwa urithi wa Tanzania. Mboma anadai kuwa Nyerere alimwambia alinde muungano kwa nguvu zote na akiona kuna hatari ya muungano kuvunjika, Jeshi lichukue madaraka. Kingunge naye anadai kuwa Nyerere alimwambia atumie busara yote kuhakikisha siasa zinaendeshwa bila kumwaga damu ya Watanzania. Naye mkuu wa Polisi anadai kuwa Nyerere alimwambia awafuatilie kwa karibu wanasiasa kuhakikisha kuwa hawaiuzi nchi kwa mabepari wa mataifa ya magharibi. Mkapa naye anadai kuwa Yeye ndiye aliyeachiwa nchi kuhakikisha kuwa siasa ya ujamaa haifutiki Tanzania.

Ukiyaangalia madai yao, na uwe kidogo ulimfahamu Nyerere, utakubaliana nao kuwa wote wanasema ukweli. Ni ukweli kwa sababu mwalimu alitaka kuwaona kila siku Butiama wakilalamika kwaba hili halitekelezeki kwa sababu linapingwa na lile. Yaani alihakikisha kuwa la mkapa halitekelezeki kwa sababu linapingwa na Mkuu wa Polisi. Na lile la Mkuu wa majeshi linakwamishwa na KINGUNGE NGUOYAMBALI.

Wakati kila mmoja wao alipopeleka malalamiko yake Butiama ndipo Nyerere alipata nafasi ya kuwaonyesha jinsi walivyo wajinga, na inasemekana alikuwa akiwafundisha kama watoto wa Nasari. Ndio maana wote wanamwita mwalimu. Ni kweli alikuwa mwalimu wao.

Sasa Mwalimu hayupo, na wanafunzi wake wameanza kuvurunda mambo.Tayari Polisi wamewaua raia zaidi ya 50 wasiyo na hatia kwa madai kuwa walihudhuria mkutano wa kuda haki yao waliyonyanganywa na Serikali.

Wanajiona kama hawana haki ya kudai chochote katika nchi yao.Wakitafuta wa kulaumu wanamuona Nyerere waliyemwita BABA.

Wanaona Nyerere alikosea kuwaachia urithi watu wanne tu na kuwasahau watu milioni karibu 40 kutegemea maamuzi ya watu wanne.

Matatizo yanayopikwa Tanzania sasa hivi yana michango mingi iliyochangia kuyafikisha hapo yalipo,Lakini Nyerere pamoja na kwamba ni marehemu hawezi kuepuka lawama.Aliitawala Tanzania kama mali yake, na mawazo yake ndiyo yaliyokuwa sahihi, Na hata kama aliweka Mtu, alihakikisha ni mjinga atakayeketi miguuni pake siku zote kufundishwa.

Namkumbuka Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye Nyerere alifikiri ni mjinga, lakini baada ya kutawazwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano, alianza kufanya vitu vyake kama mwanaume anayefikiri. jambo ambalo lilimletea mikwaruzo na huyo aliyekuwa akijifanya kujua kila kitu.


Kwa sasa kuna Mkapa anayeitwa Rais wa Tanzania, Lakini nikienda Tanzania nitakutana na mzee Ali Hassan Mwinyi kwani kwangu huyo ndiye mtu aliyethubutu kuwa na mawazo huru wakati wa Nyerere kwenye uongozi wa Nyerere. Mkapa na wenzake wanatakiwa wajue kuwa sasa Nyerere hayuko, na majukumu ya kuiongoza Tanzania lazima yahusishe Watanzania wote.

Kiburi kwamba wao ndio walioachiwa nchi waache. Hata huyo wanaedai kuwa aliwaachia Tanzania haikuwa yake. Matatizo ya Zanzibar yatafutiwe uvumbuzi wa haraka unaozingatia haki na siyo ubabe kama serikali inavyojaribu kufanya.

Madai ya chama cha CUF kwamba uchaguzi urudiwe na iundwe tume huru, pamoja na kubadilishwa kwa katiba yatiliwe maanani kuinusuru nchi na vita vya kidini ambavyo vinaonyesha kila dalili ya kuanza. Wakristo wasifurahi kwamba serikali ya Mkapa inawazibiti Waislamu, wajue kuwa serikali hiyo hiyo inaweza ikawageukia na wao.

Mkapa aache mara moja kuitegemea Amerika kumsadia kutatua tatizo la Tanzania kwani sera za Marekani ni kuwanyanyasa Waislamu duniani kote.Wananchi wa Tanzania wana uhuru wa kuamini dini yeyote na ikiwa Wazanzibar wengi ni waislamu sioni sababu ya wao kuadhibiwa kwa sababu ya dini wanayoiamini.

Hata kama wanataka kuuvunja muungano kwa sababu wanazozijua wao, wawe huru kufanya hivyo kwani ni kinyume kuwalazimisha kubaki kwenye muungano ambao hawaoni faida yake.

Nyerere alipata sifa duniani kwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar, na Mkapa atapata sifa ya kutenganisha Zanzibar na Tanganyika kuepusha umwagikaji wa damu. Kila kitu kina wakati wake. Wakati wa Nyerere ulikuwa wa kuunganisha, siyo vibaya wakati wa Mkapa ukawa ni wa kutenganisha kwa faida ya walio wengi.

Kumuenzi Nyerere siyo kumwaga damu kutetea sera zake ambazo alizitetea bila kumwaga damu.

Mwisho ni vizuri Mkapa akajua kwamba yeye siyo Nyerere, na kuna vitu alivyoviweza Nyerere ambavyo yeye haviwezi. Pia asisahau kuwa kizazi alichokitawala Nyerere ni tofauti kabisa na kizazi anachokiongoza.

Sura nzuri na maumbile ya Nyerere yalimsaidia kusamehewa haraka na umma, Wakati sura ya kutisha na maumbile ya ajabu ya Mkapa yanamfanya awe mtu asiyesamehewa haraka akikosa.

Tayari Mkapa ameshaukosea umma wa Watanzania kwa kuamuru Polisi wawaue zaidi ya watu hamsini huko Zanzibar, sijui itawachukua muda gani kumsamehe. Lakini kama ningekuwa Mkapa, Ningejiuzulu niombe msamaha, halafu niunde tume ya marekebisho ya katiba ili wananchi watoe mawazo yao kuhusu jinsi wanavyotaka kuongozwa. Halafu wafanye uchaguzi ndani ya katiba mpya.

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Dec. 17 2003,02:28   

Munishi,
Huna mpya hata kidogo bali ni lawama zisizo na miguu wala mikono. Ongea vitu vya msingi ili ueleweke. Malizia historia yako ya maisha na mwaga sera za kuweza kukupeleka ikulu, acha kuhubiri injili kwani hapa si kanisani.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 17 2003,14:41   


http://munishi.com/

NYERERE MWENYEWE ALIKIRI KUSHINDWA

NIsemayo hapa ni kweli. Hata Nyerere mwenyewe aliwhi kukiri kushindwa kwa sera zake.


   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 17 2003,17:40   


http://munishi.com/

MATESO YA CCM SASA BASI

Watanzania tunataka mabadiliko. Tuanze ENZI MPYA BILA CCM

   
  141 replies since Nov. 17 2003,19:17 < Next Oldest | Next Newest >  

Pages: (15) < ... 6 7 8 9 10 [11] 12 13 14 15 >   


Track this topic Email this topic Print this topic