10 Next Page   
  Topic: CCM IMESHUSHA JEHANAMU TANZANIA, HOTUBA YA MCHUNGAJI KWA TAIFA < Next Oldest | Next Newest >  
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Dec. 09 2003,07:59   

Quote (aawakil @ Dec. 08 2003,19:33)
Ndugu Munishi,

Ahsante sana na nimekuelewa vizuri. Hii inaonyesha kwamba kweli unawafikiria watanzania walio nje na hicho ni kitu muhimu sana. Mtanzania ni Mtanzania awe mahala popote duniani. Kura yangu umepata.

Ndugu,

sijakuelewa vizuri kwa kauli yako hii. Kwani ni nani aliyekuambia kuwa Watanzania waliopo nje hawathaminiwi. Labda nyinyi ndiyo hamuithamini nchi yenu na Watanzania nyumbani.

Unaweza kutupatia mfano wa siku ambayo Ubalozi ulikutaa kuwa wewe si Mtanzania.

Kama wewe ni ulitorokana kukimbilia huko ulipo basi lazima kuna kosa ulilifanya hapa nchini ndio maana unaogopa kurudi, sasa unataka kumtumia Munishi kwa manufaa yako binafsi, Karibu ukitubu utasamehewa tu usijari.

Tanzania ni nchi ya amani ingawa labda wewe unafikiri tofauti. Amani ya Tanzania itaendelea kuwepo kizazi hata kizazi.

Kingine sijakuelewa au labda mimi upeo wangu ni mdogo wa kuelewa. Hivi naomba mnaojua "kama kwenye Uchaguzi Mkuu huwa kuna makaburasha ya Kura yanapelekwa nje ya Nchi kwa ajili ya Watanzania walipo huko kupiga kura. Maana umesema kura yangu umepata!!!!!!!!!! Usitake Kumdanganya Munishi aanze kuhesabu Kura atakazo pata kumbe siku ikifika apatwe na ugonjwa wa Moyo.

INANIUMA SANA!!!!!
Jina Kubwa

   
Uwazi



Group: Members
Posts: 176
Joined: July 2003

Posted: Dec. 09 2003,11:07   

Quote (Munishi @ Dec. 08 2003,12:36)
Katiba ya Tanzania ni ya watanzania. Siyo mali ya CCM. Lazima kila mtanzania ahusike katika kuirekebisha au kuibadili. Kuna mengi yanayohitaji marekebisho na mengine yatatolewa kabisa. Najua kwamba nikiingia ikulu na katiba ya sasa itanikwamisha mengi. Tanzania ni sawa na gari iliyonoki injini. Inataka  matengenezo kamili ndani ya injini. Siwezi kuifanyia Tanzania MAREKEBISHO INAYOSTAHILI bila ya katiba mpya. Hata kama kipengele kimoja kitabadilishwa niweze kugombea bila chama cha kisiasa, hilo siyo lengo langu.

Munishi

Ama kweli hii demokrasia ya vyama vingi ni jalala. Tutasikia hata yale yasio wezekana. Kwa mara ya kwanza tunaweza kuona mkokoteni ukivuta farasi, badala ya farasi kuvuta mkokoteni.

Ndugu Munishi P'se get real, unapotoa majibu yako lazima utoe a practical answer/solution sio utopia. Nitakuuliza tena kwa mara mwisho and this is litmus test if you are really serious, kama utaendeleza porojo I'll rest my case and you will hear me no more.

Kipi kitaanza kwanza wewe kwenda Ikulu au kubadilisha katiba?! Definetely kinachowezana kwako kabla ya kwenda Ikulu ni kubadilisha katiba kwanza. Kwasababu kama katiba haijabadilishwa wewe huwezi kugombea nafasi ya Urais achilia mbali ndoto za kwenda Ikulu.

Njia za kubadilisha katiba zinaelewekea, through referendum au kwa kutumia Bunge.

Sasa ninacho kuomba utueleze je wewe umejiandaa kwa vipi kubadilisha hiyo katiba ya Tanzania. Je ni kitu gani umeshafanya ili uweze kuibadilisha hiyo katiba kabla ya 2005? Tafadhari tueleze kwa kina njia unazo/utakazotumia kubadilisha katiba usipige porojo tu hapa.

Je wewe Munishi unaweza kuitisha referendum? hiyo mandate umeipata wapi?

Je wewe Munishi unaweza kupeleka musuada wa mabadiliko ya katiba bungeni? hiyo mandate umeipata wapi?

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 09 2003,14:51   



NANI ALIKUDANGANYA WANANCHI HAWAWEZI KUIBADILI KATIBA??

http://munishi.com/

Hii katiba ya sasa ni ya CCM. Tena ni batili. Hatuitaki. Lazima tuwe na katiba mpya kabla ya uchaguzi.Tunataka katiba yetu wananchi. Katiba iliyoko ina ujanja ujanja mwingi wa Nyerere kuendelea kuiweka CCM madarakani. Yenyewe ndiyo inayosema haiwezi kubadilishwa na Munishi au wananchi wa Tanzania, mpaka bunge la CCM lifanye hivyo. Hiyo ndiyo maana nzima ya kuibadili.

Ingekuwa nzuri haja ya kuibadili isingekuwepo. Kwa hiyo tutaikiuka ili tuibadili. Hatuwezi kuifuata katiba ili tuibadili katiba hiyo hiyo. Kusema kwamba katiba lazima ibadilishwe na sijui nani hiyo hatujui. Tunachojua ni kwamba wananchi wa Tanzania hawaitaki katiba ya sasa. Na hao ndio watakaoibadilisha. Wataibadili vipi? Subiri uone.

Tume ya uchaguzi ndio wanaotakiwa kuweka shinikizo hilo. "HAKUNA UCHAGUZI BILA KATIBA MPYA." Tayari tumewapelekea malalamiko yetu. Tunachofanya sasa ni kuwaelimisha wananchi kuhusu vipengele vinavyowakandamiza katika katiba. Wavijue na wakati wa kutoa maoni yao, waseme kile wasichokitaka katika katiba.

Kuna mengi lakini la msingi litakuwa kuyapunguza madaraka ya rais, na kuyahamishia kwa wananchi na bunge.

Sema kama una la kusema. Ikiwa huna bora unyamaze milele. Sipendi sana wakati unapofungua huo mdomo wako UWAZI hapa. Tena uende kabisa.  

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 09 2003,16:22   

MADARAKA NI KILEO KINACHOWEZA KUMLEVYA YEYOTE

Katiba ina mengi yanayohitaji marekebisho, zaidi ya kuruhusu mgombea binafsi. Wananchi wanapaswa kuelimishwa kuhusu katiba ya sasa ili waamue kipi warekebishe. Baada ya kuyakusanya maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya katiba, Katiba mpya iandikwe.

Madaraka ni ulevi unaoweza kumlevya yeyote. Ndiyo maana tunapendekeza kwamba madaraka ya rais yapunguzwe katika katiba mpya. Tusijidanganye kwamba tutafanya hivyo baada ya uchaguzi, kwani rais atakuwa ameshaapa akitumia katiba ya zamani. Ni vyepesi kwake kusema kwamba aliapa kuilinda na kuitetea katiba ya zamani.

Hatubadili katiba kwa sababu ya Munishi, Bali tunafanya hivyo kwa ajili ya watanzania na vizazi vijavyo. Tukiwa na hayo mawazoni, Zoezi la kuandika katiba mpya linatakiwa kuanza mapema iwezekanavyo.


   
Augustine Moshi



Group: Members
Posts: 318
Joined: May 2003

Posted: Dec. 10 2003,05:54   

Ndugu Munishi,

Kazi ya Urais inataka uzoevu wa kazi, na hasa kazi za uongozi. Nionavyo kwenye historia yako, uzoevu wa kazi ulio nao ni wa kuimba nyimbo na wa kufanya biashara kwenye ngazi ya machinga. Huo sio uzoevu unaotosha kwa kazi ya Rais wa nchi.

Vile vile, sikuona kwenye historia yako mahali ulipopata upenyo wa kuelewa Kiingereza cha kusoma na kuandika vizuri. Na naona hupendi kupost kwenye mada za Kiingereza za bodi hii. Nasikitika kusema kwamba sijaamini kuwa unamudu Kiingereza kiasi cha kutosha.

Umepata mafanikio makubwa sana kwa kushughulika wewe mwenyewe. Unajituma, na unao uwezo wa kujifunza haraka haraka na bidii ya kazi. Sio kosa lako kwamba hukusoma zaidi. Hata hivyo, ni vema ukaelekeza nguvu zako kwenye malengo utakayoweza kuyafanikisha, na hili la kuwa Rais sio mojawapo. Ukiamua kujiunga na chama cha siasa na kugombea ubunge, unaweza kabisa kufanikiwa, na utakuwa mbunge machachari kweli kweli.

Augustine Moshi

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 10 2003,10:45   



KIINGEREZA NI LUGHA SIYO ELIMU

http://munishi.com/

Bwana Augostino Moshi.
Kama usemayo ni kweli, hata ubunge sifai. Hata huko kiingereza ni lazima. Pengine nirudie kazi yangu ya umachinga.

Sina tabia ya kuchangia mada zaidi ya mbili pengine ndiyo sababu hunioni kwenye MADA MCHANGANYIKO, Na hata zile za kiingereza. Napenda kuuma ninapoweza kutafuna. Sijasoma mada zako za  KIINGEREZA lakini sasa nitashawishika kuzisoma. Natamani sana kuona jinsi unavyoutema UMOMBO kuliko malkia wa Uingereza.

Pia sina tabia ya kuchomekeza maneno ya kiingereza kwenye mada zangu ili niwakumbushe watu kwamba Kimombo kimetulia kichwani. Kwangu huko ni kuchanganyikiwa na kukosa lugha ya kujieleza kwayo.

Lugha ni chombo cha mawasiliano, na huwezi kutumia vyombo vitatu kwa pamoja  kuwasiliana eti sababu ni unajua kutumia vyote vitatu. Kila chombo kikitumika mahali pake na wakati wake, hiyo ndiyo njia nzuri ya kutumia lugha nyingi kama unazijua.

Ikiwa unaegeza tathmini yako katika historia yangu, bado sijaimaliza. Nitaimalizia tu japo kufanya hivyo nawapa watu kisu wanikate kwacho.

Heri wanigonge kwa rungu nililowapa mwenyewe, kuliko watumie uongo kuniita jambazi kumbe siyo. Bora kuitwa huna elimu wakati unayo, kuliko kinyume chake.

Elimu haina mwisho, lakini ina mwanzo. Tatizo la elimu yangu ni kwamba sina karatasi za kuonyesha mwisho wake. Kama hii inamaanisha sina elimu basi na iwe hivyo.

Ni ahueni maishani. Watanionyesha njia kumbe naijua. Watanihurumia kumbe nawahurumia. Wengi watajitokeza kunisaidia badala waombe msaada kwangu. Ubongo wangu utatulia zaidi. Katika hilo mimi nina sifa za kuwa  kiongozi mzuri.

Nitasikiliza ushauri kwa sababu sijui sana. Nyerere alikuwa anajua mengi, hivyo alikuwa hashauriki. Madudu aliyofanya Tanzania wote mnayaona. Nakubali sijui mengi tena sina elimu. Hiyo kwangu ni sifa tosha kugombea kiti cha URAIS.

Lakini kuhusu kiingereza nakijua. Hilo siyo tatizo. Huitaji elimu kujua kiingereza. Ni lugha tu kama KIMASAI na KISUKUMA. Wamasai wanaongea kimasai na wengi hawakusoma. Wasukuma wanakoroga kisukuma na Kinyamwezi kabla ya kuuona mlango wa shule.

Kuhoji kwamba sifai kuwa Rais kwa sababu ya kiingereza ni kuishusha hadhi yako katika ukumbi huu. Bado naamini kwamba Moshi siyo kama mimi. Pengine alipata nafasi ya kukaa darasani kwa muda mrefu kuliko mimi. Kama hivyo ndivyo, tunategemea atoe  sababu zitakazotushawishi kwa nini Munishi asiwe rais.

Kwa hizo alizotoa zinamfanya aonekane tusivyomdhania. Ila kabla hatujamhukumu kwamba anayo makatasi bila elimu, ngoja tumsikie tena.

Nisianze kujipigia debe, Hakuna mahali mtu anapoweza kufanya kazi ya urais awe na uzoevu. Pia hakuna chuo kinachofundisha uzoevu. Kwamba lazima mtu awe na uzoevu wa kazi fulani kwangu ni kichekesho. HUWEZI KUWA MZOEVU KABLA HUJAANZA. Nyerere alikuwa mwalimu. Huo ni uzoevu wa RAIS? Mkapa alikuwa mhariri. Hata huo ni uzoevu? Basi hata mimi ni mhariri wa gazeti la injili kwenye Internet http://munishi.com/ kwa nini nisiwe rais? Tena ni mwalimu wa kuwafundisha watu maneno ya Mungu, Je hata hapo sifai? Sifa zote walizokuwanazo marais walionitangulia ninazo.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 10 2003,14:33   



WANASHERIA TANZANIA WAMELALA

http://munishi.com/

Napata shida akilini. Watanzania wasomi siwaelewi. Hawaioni katiba ilivyo na kasoro nyingi. Hata hawaoni umuhimu wa katiba kurekebishwa. Huo ndio uzalendo katika nchi yenye amani na umoja wa kitaifa.

Hakuna amani katika nchi isiyo na sheria. Pia hakuna umoja kwenye nchi ambayo sheria zote ni CCM chama kinachotawala.

Katiba ndiyo chimbuko la sheria zote. Ikiwa mbovu na sheria zinakuwa mbovu. Tanzania tuna katiba mbovu iliyozaa sheria mbovu. Sijui wanasheria Tanzania wanafanya nini. Siwasikii kokote wakisema katiba irekebishwe. Inaonekana wanafurahia hali ilivyo. Pengine wanafaidika na hali hiyo. Sheria zinapokuwa rahisi kupindishwa ili kuwanufaisha wanasiasa na wale waliounganika kisiasa, Wananchi walio wengi ndio watakaoteseka. Watanzania wameteseka kwa muda mrefu sasa, Ndiyo maana tunasema lazima katiba ibadilishwe.

Marekebisho ya Katiba ni mawazo yaliyofikia wakati wake, na ole wake atakayejaribu kupingana nayo. Yatamzoa kama mafuriko yazoavyo kila kilicho simama njia yake.

   
MTANZANIAA



Group: Members
Posts: 13
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 10 2003,16:08   

HONGERA Munishi
Kama kuna mada imenivutia katika ukumbi huu ni hii aliyoanzisha Munishi. Leo nimeisoma kutoka mwanzo hadi mwisho, ni kama muvi, mbabe akiwa MUNISHI. Wanamchapa na kila aina ya makombora lakini hafi.Unapodhania kwamba sasa Munishi kwisha, unamuona ameamka huku akitupa makombora yanayowatisha kina Uwazi Pilla na Bwambaja.

Wakati mwingine wanajifanya marafiki ili wambane, Na Munishi anawashitukia na kuanza kuwalima wote. Kila mbinu inatumika hapa kumweka Munishi chini lakini kijana wa watu anajitetea kama mwanaume. Laiti lingetolewa gazeti la mada hii kama ilivyo. Mitaani lingeuzwa kama keki moto. Kila bongo inayopambana na Munishi imenolewa kiasi utafikiri wote ni CCM.

Pongezi zangu nampa Munishi lakini amchunge sana UWAZI. Kila akitupa kombora linampata Munishi na inakuwa bahati kumsikia tena. Linakuwa la kuotea tena kali la uhakika. Mwingine wa kuchunga ni Pilla anayejifanya rafiki ili kumpunguza makali Munishi afikirie ana rafiki wa kumtetea hapa. Atakosea sana akifanya hivyo. Wote lao Moja kuona Munishi anaondoka hapa kichwa chini akiwa amejiinamia. Lakini mtoto wa Kichagga amekataa "kabisa babangu kweli."

kuna huyu anyejiita Moshi wa Augustino, Huyu ni kama Yuda msaliti. Wanamtumia sana kumweka Munishi sawa ili waje wammiminie makonde. Sijui kama Munishi ameliona hilo? Kama hajui kikulacho kiko wapi basi aendelee kumwendekeza Moshi. Jasho jembamba litamtoka.

Kina Bwabwaja na wenzake Mizambwa ambao wanaonekana kama maadui leo, Munishi anaweza kuwahitaji huko aendako wamsaidie kuunga mkono hoja yake. Wanasema katika siasa hakuna adui wa asili. Adui leo anaweza kuwa rafiki kesho. Pole Lakini Munishi hayuko kwenye chama cha kisiasa kwa hiyo yote asemayo hapa ni dini tupu.

Miye MTANZANIA nimerudi baada ya kuona Munishi ameamka tena kwa ukali baada ya kuangushwa chini na lile zoezi la kulazimishwa kuandika historia yake hapa. Mimi nilisema "Mungu wangu Munishi sasa kwisha."
Nilikuwa nimeanza kutoka uwanjani nikidhani mpira sasa umekwisha. Kumbe hiyo imemsaidia Munishi kuupata msingi imara wa kusimama. Wengi tumemfahamu zaidi, na imewakata kilimi waliokuwa wanamzulia kwamba yeye alikuwa jambazi sugu.

Kumbe Munishi ndivyo alivyo? mtu jasiri, asiyekata tamaa maishani, anayejituma, mchapa kazi kwa bidii. Anajiamini alivyo na huwezi kumyumbisha kwa yale anayoamini ni sawa. Hanunuliki kwa sifa au pesa. Mwenye misimamo.

Kama ameweza kurudisha magoli yote na kuongoza, hapa, hata Tanzania iliyofungwa magoli ya umasikini na CCM Munishi atayarudisha magoli yote na kufunga ya ushindi. Watanzania wanaweza kuurudisha utukufu uliopotezwa na CCM kwa kumchagua munishi awe Rais wao.
Tuko pamoja Munishi. Songa mbele Ikulu inakungoja. Ila usinisahau katika ufalme wako. Hata ubalozi hapa Marekani unanitosha. Sitaki makuu.

   
Bwabwaja



Group: Members
Posts: 66
Joined: Oct. 2003

Posted: Dec. 11 2003,05:00   

Munishi,
Ndugu A.Moshi kakueleza ukweli unaostahili kabisa wewe endelea kuimba na kuhubiri injili yako lakini hii ndoto ya mchana ya kuingia ikulu sahau kabisa kwani huna sifa na vigezo vya kukupeleka ikulu.
Shule ni kitu muhimu sana ndugu yangu napenda uelewe, na huwezi kuongoza nchi kwa kutumia uzoefu wako wa biashara za machinga, unahitaji kwenda shule ili kupata upeo ama uwezo wa kupambanua na kuelewa mambo. Ndugu A.Moshi alivyosema kuhusu Kiingereza hakuwa na maana kama wewe ulivyoelewa bali alikuwa na maana ya shule inayokubalika na wala si shule ya ngumbalu au ya kubabaisha.
Kwanini unang'ang'ania injili sana katika posting zako?, huoni kama unachanganya dini na siasa?, kwa maana kwamba usitumie dini kupingana na siasa ni kitu hatari sana na vilevile ni hatari kutumia siasa kupingana na dini.
Munishi, kwanini umeficha ukweli kuhusu maisha yako jinsi ulivyokuwa?. Unakumbuka katika shuhuda zako ulizokuwa unatoa mara tu baada ya kumpokea Yesu?. Mimi ni mtu ninayekuelewa vyema sana kwa hiyo tafadhali toa hitoria ya kweli ya maisha yako kabla sijaimwaga ama kuibwabwaja katika ukumbi huu.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Dec. 11 2003,11:31   



http://munishi.com/

SIOGOPI TUHUMA ZA KWELI LAKINI UZUSHI NI SIFA YA CCM
Kama kusoma ni karatasi wanazopewa watu baada ya kudai wamemaliza shule, basi maana nzima ya kusoma imepotea. Nashukuru kwamba wengi hawazithamini karatasi wanazopewa watu na ndiyo maana makampuni yanakuwa na mahojiano na watu kabla ya kuwaajiri.

Wanafanya hivyo kwa kujua kwamba wengine kama BWABWAJA watakuwa wamebeba shahada bandia lakini hawana elimu inayostahili. Wengi wanaojiita wasomi wana shahada bandia. Ama walisukumizwa shuleni kwa sababu wazazi walikuwa na uwezo kipesa, ama walikuwa wameunganishwa kisiasa.

Hapa mna nafasi ya kuhojiana na Munishi ana kwa ana. Ni rahisi kuujua  uwezo wa elimu yake kutokana na yale anayoyasema hapa.

Kama nisingekuwa mkweli ni rahisi kununua shahada za kutoka chuo chochote kinachojulikana na kuwaonyesha. Wengi wenu mna shahada za namna hiyo. SIOGOPI TUHUMA ZA KWELI LAKINI UZUSHI NI SIFA YA CCM. Wamenizulia Mengi, niko tayari kusikia mengine.


Nakubaliana na hoja kwamba kuwepo shule zinazotambulika ili kupima watu wana elimu gani. Lakini shule hizo zikiwa Tanzania nchi ambayo kila kitu ni siasa, nina mashaka na wasomi waliopitia katika utaratibu huo. kunazalishwa watu wa ajabu sana. Wavivu kufikiri, Waoga kutangaza misimamo yao, Watu wasioweza kufanya maamuzi hata yale yanayohusu maisha yao ya kila siku. Ndiyo maana hata hapa wanaogopa kutaja majina yao kamili, kwani hawajiamini.

Haiingii akilini Dr. mwenye PHD apoteze muda wake hapa kutoa maoni akitumia jina BWABWAJA? Kwa nini asiseme Dr. Fulani wa fulani ndiye anayetoa maoni hapa? Itatusaidia wasomaji kuyatilia maanani maoni yake. Hao ndio wasomi wa Tanzania.

Ndiyo maana sioni ajabu wenzao kutoka Kenya na Afrika kusini ndio wanaoshikilia nafasi za juu katika sekta binafsi Tanzania huku wasomi wa Tanzania wakifanya kazi za utarishi katika nchi yao na shahada zao. Wanalipwa duni kwa sababu wanaonekana duni. Hata hapa ukiwasikia wakitoa maoni bado ni duni. Nyerere aliwadumaza akitumia JKT ili wawe duni katika kila kitu.

Kwangu watu kama hao ni hatari kuliko wale ambao hawakuuona mlango wa shule. Cha ajabu hao ndio waliosimamia  mashirika yetu ya umma badala ya sekta binafsi iliyokuwepo kabla ya azimio la Arusha. Walifanya nini pamoja na DR.Nyerere? waliharibu mashirika yote na sasa tunapozungumza yamekufa. RTC, KAMATA, Mashamba ya kahawa, mikonge,na mengine mengi. Yalikufa chini ya uongozi wa DR.Nyerere.

Hatuwahitaji watu wa namna hiyo katika Enzi mpya.

Ndugu MTANZANIA Nashukuru kunipongeza. Nitaufuata ushauri wako kwa makini. Siyo wote wabaya, wengine nitatoa kutu ya CCM mawazoni mwao na nitawatumia sana katika uongozi awamu ya pili. Awamu ya kwanza ilikuwa rais kwani Nyerere aliwaonyesha watanzania Mzungu na kuwaambia kwamba hawa wakoloni ni wabaya sana. Ilikuwa rahisi kuaminika kwani Mzungu na mwafrika rangi zao ni tofauti. Mimi nasema kwamba Mkoloni mweusi CCM ni mbaya sana, na wachache hawanielewi kwa sababu rangi ya mkoloni wa sasa ni sawa na yetu.

10 Next Page