2 Next Page Page1  
  Topic: CCM IMESHUSHA JEHANAMU TANZANIA, HOTUBA YA MCHUNGAJI KWA TAIFA< Next Oldest | Next Newest >  
MTANZANIAA



Group: Members
Posts: 13
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 21 2003,15:36   


Mchungaji Faustin Munishi ambaye pia ni mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili Afrika ya mashariki na kati, Ametangaza azma yake ya kugombea urais Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao. Katika kufanikisha azma hiyo mchungaji huyo ametoa kanda za video katika CD maarufu kwa jina la VCD. Serikali nayo kwa upande wake imezipiga marufuku kanda hizo kwa kigezo kwamba zina kashfa dhidi ya Mkapa na CCM. Mengi yamesemwa kuhusiana na uhalali wa serikali kuzifungia kanda hizo, huku wengine wakiilaumu serikali kwa kufanya hivyo. Wanaona kitendo hicho kama UONEVU. Pia kuna mijadala iliyokuwa ikiendeshwa kwenye Internet kuhusiana na Mchungaji Munishi na Azma yake ya Urais. Pia hiyo serikali iliipiga STOP. Gazeti la Injili kwenye mtandao linakuletea sehemu ya mijadala hiyo bila kuhariri chochote.

Munishi tuko nyuma yako labda usema hutaki watu nyuma yako.

Uwazi anataka majina

Sasa majina ukitajiwa yatakusaidia nini? Mimi ni Mtanzania na ni mmoja wa hao watakaomsaidia Munishi kufanikisha malengo ya kuitoa CCM madarakani. Hata wewe bwana Uwazi kuwa wazi ujiunge nasi.


   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Nov. 21 2003,17:28   

Mimi binafsi hapo bado hamjanipata!!!!!!!!

Kiongozi yeyote anapo gombea uongozi lazima anakuja na maneno mazuri na ahadi kemkem ambazo baada ya kupata hakuna hata moja itakayotimizwa.

Kama Rais Bush wakati wa kampeni angewaambia Wamarekani kuwa waakimchagua ataua wanajeshi wake kule Iraq na Afghanistan au ataharibu uchumi wa Marekani kwa vita, sidhani kama kuna mjinga yeyote angempa kura yake. Lakini kwa kuwa aliwadanganya kwa ahadi motomoto walikubali kumpa na leo asilimia kubwa ya Wamarekani wanajutia uamuzi wao. Wengi walikubali kupokea hongo ili wamchague Bush leo wanajutia hongo ile inawatesa na kuwaacha yatima na wengine kupoteza ndugu na jamaa zao vitani. NA BADO WANAENDELEA KUTEKETEA!!!!!!!!!!!!!!

Hivyo wewe ndugu yangu hizo ngonjera tumezizoea za kuona fulani hafai ila mimi nafaa na ukichaguliwa unakuwa OVYOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!

HAUTUPATI NGOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!1

INANIUMA SANA!!!!!
Jina Kubwa

   
MTANZANIAA



Group: Members
Posts: 13
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 21 2003,17:41   

Sasa BOra lipi? Kuendelea kuteseka na CCM? au tukubali kubadilika? Bora kufa ukienda kuliko kufa ukiwa umekaa. Vyote ni vifo. Siamini kwamba Munishi mtumishi wa Mungu anatupotosha. Kama kudanganywa CCM wametudanganya miaka mingi mno. Bakini CCM mimi na watanzania wenzangu tena wengi tu tunataka mabadiliko. Usife moyo Munishi, tulio upande wako ni wengi kuliko walio kinyume chako. CCM HAPANAAAAAAAAAAAA!!!!!! TUMEKATAAAAAAAAAAAAA!!!!!

   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Nov. 21 2003,18:17   

Huyu Munishi ni mulongo ingawa ni mtumishi wa Mungu. Hapo alipo ana Kadi ya CCM, sijui ni shushushu huyu!!!!!!!!!!!!

Hapa anataka kuiba mawazo ya wana bodi tu. Mchunguzeni vizuri. CCM ina mashushushu wengi tena wengine wanajifanya kujiunga na upinzania na ikifika kipindi cha kukaribia uchaguzi wana kuwa ndio wa kwanza kuanzisha migogoro katika kile chama ili kukisambaratisha na kuifagilia CCm.

CCM ILIDUMU, INADUMU NA ITADUMU IKIWA NA WATU KIPAO!!!!!!!!!!!!!

MUNISHI MMOJA WAO!!!!!!!!!

INANIUMA SANA!!!!!
Jina Kubwa

   
s.crony



Group: Members
Posts: 79
Joined: July 2003

Posted: Nov. 21 2003,18:49   

"jina Kubwa" nakubaliana nawe CCM itakuwepo na kwa mwenendo wa vyama hivi vya kitapeli(upinzani) tulivyonavyo basi hakuna habari ya kuingoa madarakani,ila labda kipande ninachotofautiana nawe(nikutoe nje kidogo)-suala la USA na Bush si hongo ni wizi wa kura[QUOTE][/QUOTE]
ule ni wizi wa mchana kweupe kiasi ajabu kwa babu linalojiita la demokrasia kudai ushindi mahakamani.Kesi ya mhs.Munishi huu ni uwongo wa kitoto wa kuwapa hadithi za kutisha ili walale mapema.Nasikitishwa sana na kambi ya upinzani kuwa pamoja ktk kipindi hiki na kutukanana wkt wa uchaguzi ni mara mia afadhali ya CCM chenye maadili na taratibu nzuri za kuondoa tofauti zake tuachane na hawa wanafiki,long live CCM

--------------
s.crony

   
aawakil



Group: Members
Posts: 22
Joined: July 2003

Posted: Nov. 21 2003,20:55   

Kuna wengine wa asili ya kiasia ambao nao hupewa kumiliki maeneo yote muhimu ya kibiashara. Makubaliano ni kwamba mapato wayagawane na wanasiasa. Inasikitisha kuona wananchi ndani ya nchi yao wakiteseka, huku wanasiasa na wageni wachache wakimiliki njia zote kuu za uchumi.


Ndugu Munishi,

Nimesoma hoja zako kwa makini.Soma ulivyoandika hapo juu. Inaonekana ni dhahiri kua kwanza wewe ni mbaguzi mkubwa.
Nasema hivyo kwa sababu unakifua ya kutamka waasia  ambao nao hupewa kumilki maeneo yote muhimu ya kibiashara.
Je unajua kuwa waasia hao ni raia wa Tanzania na wako nchini hata kabla ya wewe kuzaliwa. Kwa hivyo wana haki zote sawa na mzawa au raia mwingine wowote.
Please stop being a RACIST and fingerpointing at a particular tribe.It would be much better for your philosophy and your preaching if you totally stop this attitude of Racism.
Labda nilichoandika itaku udhi sana lakini nimesema ukweli.
Ahsante

 
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 22 2003,12:20   


CCM WENGINE WANAKIITA CHAMA CHA MAJAMBAZI

SIKU YA KUFA NYANI MITI YOTE HUTELEZA

http://www.munishi.com

Siku ya kufa nyani, Miti yote huteleza.
CCM ni sawa na nyani ambaye siku ya kufa kwake imekaribia. Kila mti wanaojaribu kuuparamia unateleza. Ujuzi wa CCM kuparamia miti ni wa miaka mingi. Lakini sasa miti yote inateleza na kufa watakufa.

Utafiti uliofanywa na BBC Tanzania unaonyesha kwamba ukimwi umesambaa Tanzania kwa kiwango cha kutisha. Nchini Tanzania inasadikiwa kwamba wenye madaraka ndio wanaoongoza katika kuusambaza ukimwi. Kwingine wanadai ngono kama hongo, na mara nyingine wanapewa kama zawadi kwa sababu wana pesa nyingi walizojipatia wakiwa madarakani. Usijali kama walipata kwa halali mapesa wanayotumia, lakini ukweli unabaki kwamba wenye madaraka Tanzania ndiyo wanaoongoza katika kuusambaza ukimwi. Nani wamekuwa kwenye madaraka Tanzania kwa zaidi ya miaka arobaini kama siyo CCM?

 Hao ndio nambari wani kwa kila kitu, hata kuusambaza ukimwi ni nambari wani. Hata bila upinzani, ukimwi unatosha kuisambaratisha CCM. Msidanganyike kwamba CCM ni chama imara. Kama kuna chama kisicho na matumaini ni CCM.

Ni ukweli walikuwa wamejiimarisha katika kila kona ya nchi, lakini nguvu zao ndizo zimegeuka kuwa maangamizo yao. Huzuni yetu ni watanzania wasio na hatia ambao itawabidi wapoteze maisha yao.

Nchi nyingi barani Afrika wameutangaza ukimwi kama janga la kitaifa, Lakini Tanzania ndio kama hakuna ukimwi kabisa. Vigogo wanaokufa kwa ugonjwa huo wanatafutiwa majina ya kitaalamu kufunika isieleweke walikufa kwa Gonjwa la Ukimwi.

Utasikia kwamba ilikuwa ni kansa ya damu, wengine watasema kwamba moyo ulishambuliwa, na siyo ajabu ukasikia wakisema kwamba damu za waadhirika zilitengeneza mabonge ya barafu ya damu, na ilipokataa kuyeyuka ndipo kifo kikatokea. Kwamba nchi imekataa kukubali ukweli kwamba ukimwi unaua hata viongozi hilo ndilo linalotisha kuliko Ukimwi wenyewe. Hatulifurahii, kwani hatujui wanaosambaza wamefikia wapi katika zoezi lao. Siyo ajabu miaka kumi ijayo Tanzania ikawa na watu wachache sana.

Kama CCM wanaongoza kueneza ukimwi? KANISA NI SALAMA?
Lakini tusisahau kwamba maaskofu na mapadri wanakufa kwa ugonjwa huo wa UKIMWI.
Kwamba hata hao wanaondoka tena kwa kasi ya ajabu, huo ni ushahidi tosha kwamba wengi katika jamii hawawezi kuachana na UFUKSA. Sasa je tuwaache waende kaburini kichwa kichwa? Wanaohubiri kwamba KONDOMU inakinga kwa asilimia mia  moja wanakosea, na wanaosema kwamba watu wasitumie kondomu kabisa wanakosea zaidi. Mbaya zaidi ikiwa wanaosema hivyo ni kanisa Katoliki ambalo linajulikana kwa mmomonyoko wa maadili kuanzia makadinali maaskofu mapadri na watawa wa kike.

Siyo siri tena kwamba ufuksa kwenye kanisa hilo ni wa hali ya juu, hasa ule unaohusisha watu wa jinsia moja. Kisa na sababu ni sera ya kanisa ya kutowaruhusu watumishi wa kanisa kuoa na kuolewa. Ikiwa wenyewe  ni MAFUKSA YA KUTUPWA, kuna kosa gani mtu akiwapa mipira kujikinga angaa kidogo? Kwa wale waliowahi kupanda ndege, kila siku ni lazima atokee msaidizi katika ndege hiyo ili kuwaelezea jinsi ya kutumia mpira wa kujiokoa wakati wa ajali. Watu wote husikiliza kwa makini sana maneno yake, japo hakuna ukweli ni kwamba inapotokea ajali ya ndege wengi hufa. Na wale wanaopona mara ngingi huwa hawakusaidiwa na mipira hiyo. Japo kuna wachache ambao imewasaidia. Pointi hapa ni kwamba tusikatae kabisa kondomu. Nakataa kwamba kondomu itachochea ufuksa. Kuna majaketi ya kujikinga na risasi, na sioni watu wakiyanunua ili waende mahali polisi na majambazi wanapofyatuliana risasi.

Kwa kuwa ushahidi wa kutosha upo kuonyesha kwamba watu wameshindwa kuacha ufuksa, tusipinge kila juhudi zinazochukuliwa kuwasaidia wale walioshindwa kujizuia. Ukimuona mtu kapanda kwenye jengo ndefu na anataka kujirusha chini, siyo vibaya kutafuta magodoro mawili matatu ili akifika chini asijipigize sana kwenye lami. Nani ajuae? unaweza kuyaokoa maisha yake hata kwa kujaribu kumdaka kama mpira.Ninachotaka kusema hapa , ni kwamba kila juhudi zifanywe kujikinga na janga hili la ukimwi. Niliwahi kuimba na kusema kama polisi wanawashika wauza bangi, kwa nini wasiwakamate wauza miili wanaoeneza ukimwi? Wengine walisema BOLTI  nne zimefunguka kichwani mwangu. Cha ajabu niko hapa, na hakuna aliyejaribu kukaza hizo BOLTI kama alivyosema Bwana Njiraine. Pengine hawana spana saizi ya bolti hizo. Lakini hata PLAYAS inaweza kujaribu kukaza.

Suala siyo nani aliyeleta UKIMWI. Ila kwa kuwa uko nasi, tusizuie kila juhudi zinazofanywa na kila taasisi au watu binafsi kujaribu kupigana na janga hili ukimwi. Unafiki kama unaoonyeshwa na kanisa katoliki hautosaidia chochote. Wale wanaoweza kuachana kabisa na ufuksa hawawezi kushawishiwa na kondomu kujiingiza tena kwenye ufuksa. Wakifanya hivyo, wajilaumu wenyewe na siyo makampuni yanayotengeneza KONDOMU. Tuelezeni nini kitumike  badala ya kondomu  lakini siyo kukazania mambo ambayo hatuna hakika kama kweli mnayaweza mnayosema. Hata kama tuna hakika mia kwa mia kwamba Moshi na Mdada hawajihusishi na ufuksa, hiyo haitufanyi tuache kuwasaidia wale ambao hawakubahatika kushinda mtihani huo.

Kila la kheri na mjichunge jamani!!! Mambo siyo mazuri. kumeharibika. Hizo ndizo ligha za mitaani siku hizi.

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 22 2003,15:41   

.
MIMI SIYO MBAGUZI WA RANGI

http://www.munishi.com

Nisemayo ni ukweli. Kuna wengine wa asili ya kiasia ambao hupewa maeneo muhimu ya kibiashara ili mapato wayatumie kukinufaisha chama tawala. Hiyo ni wazi Tanzania. Kusema hivyo siyo ubaguzi wa rangi. Wahindi ni watu kama wengine. Kuna matapeli wa kihindi, kuna wauza madawa ya kulevya katika jamii ya wahindi, Pia kuna wahindi wasiyojihusisha na yote hayo na ni raia wema, au wageni wema. Kuwataja wale waovu katika jamii ya kihindi siyo ubaguzi wa rangi. Siombi radhi kwa matamshi yangu hayo. Kama kura nitapata kutopka kwa wahindi raia wema. Hizo kura za wahindi maharamia wa CCM sina haja nazo. Zikae.

Mchungaji Faustin Munishi Yeye na CCM mbali-mbali

Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha kisiasa na sitarajii kujiunga na Mtikila wala chama chochote cha kisiasa. Wala sitarajii kuunda chama cha kisiasa. Lakini nataka mimi na Watanzania wengi wasio wanachama wa vyama vya kisiasa tuwe huru kugombea uongozi katika  nchi yetu bila kuzuiwa na chochote kama katiba ya CCM. Tunataka katiba irekebishwe iseme hivyo.

   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 237
Joined: May 2003

Posted: Nov. 22 2003,16:31   

Quote (Munishi @ Nov. 22 2003,12:20)
lakini ukweli unabaki kwamba wenye madaraka Tanzania ndiyo wanaoongoza katika kuusambaza ukimwi. Nani wamekuwa kwenye madaraka Tanzania kwa zaidi ya miaka arobaini kama siyo CCM?

Nchi nyingi barani Afrika wameutangaza ukimwi kama janga la kitaifa, Lakini Tanzania ndio kama hakuna ukimwi kabisa. Kama CCM wanaongoza kueneza ukimwi? KANISA NI SALAMA?
Lakini tusisahau kwamba maaskofu na mapadri wanakufa kwa ugonjwa huo wa UKIMWI.
Kwamba hata hao wanaondoka tena kwa kasi ya ajabu, huo ni ushahidi tosha kwamba wengi katika jamii hawawezi kuachana na UFUKSA. Sasa je tuwaache waende kaburini kichwa kichwa? Wanaohubiri kwamba KONDOMU inakinga kwa asilimia mia  moja wanakosea, na wanaosema kwamba watu wasitumie kondomu kabisa wanakosea zaidi. Mbaya zaidi ikiwa wanaosema hivyo ni kanisa Katoliki ambalo linajulikana kwa mmomonyoko wa maadili kuanzia makadinali maaskofu mapadri na watawa wa kike.

Pointi hapa ni kwamba tusikatae kabisa kondomu. Nakataa kwamba kondomu itachochea ufuksa.

Wengine walisema BOLTI  nne zimefunguka kichwani mwangu. Cha ajabu niko hapa, na hakuna aliyejaribu kukaza hizo BOLTI kama alivyosema Bwana Njiraine. Pengine hawana spana saizi ya bolti hizo. Lakini hata PLAYAS inaweza kujaribu kukaza.

Ndugu Munishi, Kama ni mwisho wa Dunia naona ni sasa. Yesu mwenyewe alisema kuwa siku ile ya kurudi kwake (YESU) hakuna ajuaye  "watajitokeza manabii wengi wa Uongo wakihubiri kwa jina langu, Msiwasikilize hao".

wewe ni mmoja kati ya manabii wa Uongo  waliotabiriwa na YESU. Tena ni IBIRISI mkubwa wewe. Nina hofu hata huo Uchungaji wewe ulijiita kama wafanyavyo Waganga wa Jadi kujiita "DR" wakati ukiuliza Chuo kipi walichosomea wanashindwa kujibu eti wamerithi kwa Babu. Nawe ni Mchungaji ambaye hana sifa, sidhani kama unaweza kusimama Kanisani na kuhubiri waumini wakakuelewa, umejaa nguvu za giza katika Moyo wako.
Kama ilivyokuwa kwa SAULI ndivyo itakavyotokea kwako, Bwana atakutokea siku moja jiandae. Usilitumie jina la kanisa kwa manufaa ya KISIASA.

SIASA ni biashara. YESU alisema "Msifanye nyumba ya baba yangu kuwa sehemu ya biashara" Je, wewe huwa unahubiri nini pale kwa Waumini wako zaidi ya siasa Kanisani.

Bahati yako upo mbali huko NAIROBI lakini ningependa siku moja nije kuhudhuria Ibada katika Kanisa lako nisikie mahubiri yako.

Sijapata kuona Mchungaji anahubiri na kuhalalisha Ufuska, wewe ni kiongozi wa NGONO, ndiyo maana unaitetea sana.

YESU alisema "Usihukumu ili usije hukumiwa, toa Bolt iliyo katika jicho lako kisha mwambie mwenzio mbona wewe una Banzi"

Huijui BIBLIA nini wewe nikufundishe!!!!!!!!! Alahhhhhhh!!!

Wewe moyo wako umejaa mawazo ya ushetani mtupu, unatumia Kanisa na Uchungaji kuficha madhambi yako mbele ya Binadamu lakini elewa huwezi kumficha Mungu.

Wewe ni dhahiri umeshindwa kuongoza Kanisa lako sasa sijui utawezaje kuongoza Nchi. Kama unataka uongozi kwa nini usigombee huko KENYA ulipo. Hatutaki MKIMBIZI kuwa kiongozi hufai hata kuongoza "TEN CELLS" Itakuwaje kwa nchi??????

Kweli kuna BOLT zimeregea katika kichwa chako, au huo UKIMWI unaouhubiri unakaribia kukupeleka, tafadhari nenda peke yako hapa humpati mtu. NENDA PEKE YAKO KAWASALIMIE WOTE WALIOTANGULIA KUZIMU.

Umeona mahubiri ya upotofu unayotoa Kanisani kwako hayatoshi sasa unaamua kuleta katika ICONBOARD ili uturubuni.

INANIUMA SANA!!!!!
Jina Kubwa

   
Munishi



Group: Members
Posts: 77
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 22 2003,18:03   



NAJUA CCM WATACHENSHA SANA

http://www.munishi.com


Najua CCM watachemsha sana. Lakini nina maji tayari endapo watayahitaji.Watatumia maandiko ya biblia ambayo hawaijui, Yote hayo kumzuia Munishi. Watafunga njia hata zile ambazo Munishi hatarajii kupitia. Mambo bado. Hiyo ni miti inateleza. Ujanja wa CCM kuparamia miti sasa basi. Kila lililo na mwanzo halikosi mwisho wake. Mwisho wa CCM ni sasa na siyo baadaye.
2 Next Page

Page1

Break in News