Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com


Askofu Kulola huipigia debe CCM

Nani anamdanganya nani? Askofu Moses Kulola na mkewe wakikumbatiana na aliyekuwa askofu wa TAG Tanzania, Emanuel Lazaro na mkewe. Wanaoangalia ni Askofu Kitonga (wa pili kulia) Pia alikuwepo mlinzi maalum wa Askofu Kulola anayejulikana kwa jina moja tu ALEX. Bila hata kuambiwa, sura yake tu inaonyesha yuko kazini. Wenzake wanacheka, lakini yeye hacheki na watu. Ana sura ya mawe. (Ni wa kwanza kulia.) CCM tangu wakati wa Nyerere, ilimpatia Kulola walinzi wanaolipwa na serikali, ili akipigie debe chama hicho. Kulola alikaidi uongozi wa TAG ikazuka vita kati yake na Askofu Emanuel Lazaro. Serikali ilimpendelea kulola kwani alidai misaada mingi kutoka Marekani ilikuwa na lengo la kupenyeza CIA Tanzania kwa kutumia TAG. Nyerere aliinunua hiyo jumla kwani sera zake za ujamaa zilizoshindwa zilikuwa zikihofu sana Marekani wasijeleta ubepari Tanzania. Kulola alionekana malaika wakati Lazaro serikali ilimuona shetani. Lazaro alikwamishwa mpaka alipoachia ngazi ya uaskofu. Kulola mpaka leo anafaidi uongo wake wa kuidanganya serikali kwamba CIA walimtumia Lazaro. Ukiyasikiliza mahubiri ya kulola kwa makini, utakuta anawalisha waumini siasa za CCM bila wao kujua. Kulola ndiye mhubiri wa DOLA Tanzania. Mikutano yake inalindwa na kikosi maalum, Yeye mwenyewe analindwa kila aendako, Ni kipenzi cha CCM. Tuombe iwe hata mbinguni Mungu atampa heshima anayopewa na CCM. Vinginevyo atakuwa ameshavuna duniani. Nchini Kenya Kitonga aliipamba sana KANU na alikuwa mhubiri wa dola Kenya. Tangu KANU waachie ngazi Kitonga yuko nje ya duara la madaraka.


Mkewe Kulola anasadikiwa kuwa na pea elfu tatu za vitenge na khanga. Kila mkutano washirika hulazimishwa kununua vitenge na zawadi nyingine kwa mama askofu. Inasemekana kwamba kina Mwasota walikosana na Kulola pale na wao walipopewa zawadi za vitenge na ikaonekana mke wa Mwasota anashindana na mama askofu kimavazi na ndipo Mwasota alipotimuliwa. Inasemekana kwamba mke wa kulola hupenda kuonekana amewazidi wote kimavazi. Nchini Kenya Kitonga aliipamba sana KANU na alikuwa mhubiri wa dola Kenya. Tangu KANU waachie ngazi Kitonga yuko nje ya duara la madaraka

Kulola Amtimua Mchungaji Arusha

Na Mwandishi Wetu Arusha

Aliyekuwa Askofu wa jimbo katika kanisa la EAGTkatika mtaa wa Elerai Arusha Mchungaji Jackson Peter, amejiengua kutoka kanisa hilo na kuanzisha kanisa jipya. Sababu? Bado hicho ni kitendawili ambacho wanaoweza kukitegua ni askofu mkuu Moses Kulola na yeye mwenyewe mchungaji J.K.Peter.


Askofu Moses Kulola Uzee unamnyemelea

Askofu Jack ambaye pia alikuwa akisimamia kanisa la Elerai mjini Arusha amelihama kanisa hilo katika mazingara ya kutatanisha. Washirika waliohojiwa na gazeti la mtandao walisema kwamba mchungaji aliamua kuachia ngazi baada ya kutokuelewana na uongozi wa kanisa hilo,huku wengine wakisema kuwa ameachishwa kazi na uongozi wa kanisa hilo kwa sababu zinazojulikana na uongozi wa kanisa hilo la EAGT.

Kanisa la EAGT linaongozwa na Askofu mkuu Moses Kulola, ambaye hakuweza kupatikana mara moja kukanusha au kukubaliana na habari hizi.Juhudi za mwandishi wa habari hizi kujaribu kumpata Askofu kulola hazikuweza kufanikiwa kwani kila mara alipopiga simu aliambiwa hawezi kuongea na Mtumishi wa Mungu kwa wakati huo.

Naye mchungaji Jackson Peter hakuweza kupatikana kukanusha au kukubaliana na habari hizi.

Lakini watafiti wa wa habari katika makanisa wanasema kuwa, mambo ndani ya EAGT siyo mazuri kwani kuna baadhi ya wachungaji ambao hawapendezwi na hatua ya kiongozi wa kanisa hiloBishop Kulola kumtawaza mtoto wake Dani Kulola huduma ya uinjilisti, na kuwasahau wengine ambao wanafikiri kuwa wanaweza kuliko huyo anayetawazwa.Kwamba hiyo ndiyo sababu iliyomfanya mchungaji Jackson Peter aachie ngazi, tunasubiri kusikia kutoka kwa Bishop Kulola.


Kutoka kwa Mhariri .
Mhariri wa gazeti la mtandao anaomba kuwasiliana na wahusika wote katika habari hizi hasa Askofu Mkuu Moses Kulola, na Askofu wa jimbo Jackson Peter,ili kuepusha kuandika habari ambazo zinaweza kuonekana kama kuegemea upande mmoja. Ni matumaini yangu kwamba kanisa litatambua umuhimu wa chombo cha habari kama hiki kanisani ili watoe kila msaada unaotakikana badala ya kusingizia kwamba mtumishi wa Mungu anaomba na hawezi kupatikana.
E-Mail fmunishi@hotmail.com

Bado Hatujasikia kutoka Kwa askofu Kulola, Lakini wasomaji wameanza kutoa maoni yao. Yafuatayo ni maoni ya wasomaji kama walivyoyaandika. Gazeti la mtandao halihariri maoni ya wasomaji bali huyatoa kama yalivyoandikwa.

EAGT Dodoma Kunafuka Moshi
Na Mwinjilisti Mwazembe Dar

watu wanahoji uko Dodoma kuhusu kanisa la E.A.G.T kuwa kuna mch. wa uko Dodoma eneo la Makole anatuhumiwa kuzaa nje ya ndoa na kuna vikao vinaendelea kama atengwe au namna gani.

Ambacho watu watu wanahoji ni kwamba kucheleweshwa kwa hukumu kunatokana na sela ya upendeleo ambayo imeligubika kanisa hilo.

Habari tulizopata hapa nikwamba askofu mkuu anamtetea huyo bwana kwa sababu wanahudumu naye. Yeye ndie anaye pambisha pambio za kushusha utukufu. Hofu ni hii kuwa kama askofu atakubari atengwe italeta maswali kuwa kama amekuwa anahudumu kwenye mikutano ya bishop je Bishop hana macho kiroho mpaka huyo mtu amedumu katika dhambi ya kupelekea kuzaa mtoto nje ya ndoa.

Na wangine wanahoji kuwa kama Akina Mwasumbi alitupwa nje na Mwasota kwa nini pia Huyu asishugulikiwe. Ninaendelea kulifuatilia jambo hili ingwaje ni kazi ngumu kidogo kama unavyojua wa EAGT ni wapole kama mzee kulola kila unapohoji jambo wao hunyamaza kimya na kukuambia kwa kweli sijui.

Lakini hizo ni habari ambazo tumepata nje ya kanisa hilo ila kutoka kwa watu wa karibu sana na huyo Mch. kama unavyojua wachungaji hupenda kushirikisha watu wanao waamini juu ya majaribu yao ili wawaombee wanasahau kwamba wale wanowaamini nao wana watu wao ambao ndio sisi.
Mwandishi wetu Mwazembe

 

Ndugu Lemomo Amlaumu Mhariri wa Gazeti la INJILI

Name: Joseph lemomo
Hometown: Arusha
Sent: 16.12 - 26/9
Habari zako hazina ushahidi wa kutosha. Unaweza kuwaingiza matatani wale wanaokupenda na kuanza kuyatangaza mawazo yako kama ni habari kamili. natumaini ingekuwa vizuri ungeanzisha chama cha siasa.

Mwinjilisti Mwazembe Amtetea Rev.Kulola

Name: Leonard S. Mwazembe
Hometown:
Dar
Sent:
12.41 - 27/9

Namshukuru Mungu sana kwa kunipa nafasi hii ili kutoa maoni yangu.Ingawaje hii ni mala yangu ya pili Kujitokeza katika safu hii ya maoni.

Nimepitia habari kadha katika gazeti la mtandao la injili ila napenda kutoa maoni yangu kuhusu kufukuzwa kwa mch arusha. Ni kweli inawezekana kutofautiana maono lakini zipo njia nzuri za kiblia za kuachana zenye kumpa Mungu utukufu.

Mf.wa Paulo na Banaba pia Rutu na Ibrahimu hawa waliachana kwa utukufu wa Mungu na wengi ne wengi. Ningependa pia kusema kama sio kutofautina maono ila ni kwa sababu tu za kibinadamu basi hatari.

Ninasema za kibinadamu kwa sababu tayari nasikia wengine hawaridhiki na kuteuliwa kwa mtoto wa askofu kuwa mwinjilisti Tufahamu kua uinjilisti sio cheo wala sio biashara ni wito wa kuwafikia wenye dhambi ambapo kibiblia wote tuliookoka tumeitwa kuufikia ulimwengu wa wenye dhambi.

Sasa sioni shida mtoto wa askofu kuchukua nafasi ya kutangaza injili ya ufalme na kama watu wanaokoka na wewe unampinga hiyo ni roho ya dini.

Mwaka huu nilikuwepo kwenye mkutano wao wa pasaka alihubiri mtoto wa askofu na watu wengi waliokoka na wengi kufunguliwa kutoka katika nguvu za giza je hiyo sio baraka? Na unapo pinga hiyo kazi tukuite nani?

Inakupasa ujifunze kwa wanafunzi ambao walitumwa na Bwana Yesu wakakuta mtu mwingine anafanya kazi ile ile ambayo wao walijiona wanafaa kuifanya wakamzuia Bwana akawambi msimkataze asiye kinyume chenu yuko upande wenu.

Mimi nasema hivi huyo mtoto wa askofu yuko upande wao na kama wakimpinga basi wanitumikia dini au shetani maana dini na shetani ni mke na mume kazi yao kubwa ni kupinga injili ya wokovu na nguvu za Mungu.
Na watu kama hao ukiwapa muda si muda mlefu wataanza kuwasha mishumaa badara ya Roho wa Mungu.

Pili injili sio mashindano kuwa nani zaidi sio simba na yanga. namtia moyo mtumishi wa Mungu Dan Pamoja askofu Kulola asitishwe na mawazo ya kidini.

Hata Musa wa biblia alitumwa na ndugu zake wa tumbo moja Miriamu pamoja na Haruni Kut 7:7. Sasa hiyo sio sababu ya mtu kuhama kama ni moja wapo.

Kubwa ya kibiblia iwe ni kutofautiana maono ambapo lengo liwe ni lile lile la kumtwanga shetani. Mungu awabariki sana popote ambapo maoni haya yatawafikia.

Mwinjilisti Mwazembe Dar

Bwana Mwakipesile Ampinga Mwazembe

Name: Mwakipesile
Hometown: Mbeya
Sent: 12.31 - 29/9

Ndugu Mwazembe!! Pengine wewe ni mgeni hapa Tanzania na hulijui vizuri kanisa la EAGT. Kulola ndiyo EAGT na EAGT ni Kulola. Naweza kuliita kanisa linalojihusisha na kulinda maslahi ya mtu mmoja.

Waangalie wachungaji hasa wa Mbeya.Hali yao kimaisha inatisha. Lakini mwangalie Kulola. Michango yote ya kanisa nchi nzima ni yake.Akija kwenye mkutano atazikandia pesa na kusema kuwa hazipendi. Baada ya mkutano, sadaka yote anakabidhiwa yeye. Bila kusahau vitenge wanavyonunua walala hoi kumpa mke wa Kulola.


Mwinjilist Mwasumbi

Kwa ujumla hali ya washirika wa kanisa la EAGT haiwezi kufananishwa na hali ya maisha ya askofu wao. Hatusemi wafanane kabisa, lakini ionekane kidogo wanajaribu kuinuka kimaisha.Miaka nenda miaka rudi washirika wanalipishwa michango ya kuufanya mkutano wa kulola ufanikiwe kuwakusanya watu ambao watakuja kutoa michango mingine.

Siyo vibaya kufanya mikutano ya Injili,lakini mikutano ya Kulola haiwalengi wenye dhambi, bali wale ambao tayari wamekwisha amini tayari. Nasikitika kusema kwamba hata wanaojifanya kulia pale mbele ili kuleta hisia kwamba mapepo yanawatoka, ni waumini wa kanisa hilo ambao wengi wao huwa wanazililia shida na matatizo ya maisha na siyo mapepo.


Kulola akiwa na vijana wa INJILI

Hakuna maana ya kuwakusanya watu na kuwafanya walie,halafu uwachangishe pesa na kuwaacha katika hali ile nile ya umasikini wa kutupwa.

Safari zote za Kulola hutumia ndege kutoka mkoa huu kwenda mwingine na inasadikiwa kuwa kanisa hilo lina uhusiano wa karibu sana na chama kinachotawala CCM.Linatumiwa na serikali kulinda maslahi ya serikali.

Moses Kulola mwenyewe ni CCM Damu.Anawakemea wote wanaoikosoa serikali na kusema wanachanganya siasa na dini.Ukweli ni kwamba WANAOKUBALIANA NA MAOVU YA SERIKALI NDIO WANAOCHANGANYA SIASA NA DINI.

Ndugu Mwazembe fanya utafiti kuhusu EAGT na utagundua kuwa ni kanisa la kikabila na Wasukuma ndio wanaoliona kama ni kanisa lao.Pamoja na kwamba sisi Wanyakyusa tupo,lakini hatusikiki.Mtu wetu akijaribu kuinuka kidogo Wasukuma wanamwambia Kulola amtupe nje ya Kanisa.


Mwinjilisti Emmanuel Mwasota

Mfano ulio Hai ni Mchungaji Emanueli Mwasota ambaye pamoja na kwamba alimsaidia Kulola sana wakati wa mwanzo, sasa Kulola amemsahau na kumtupa nje.Mwingine ni Mwasumbi. Naye yuko nje.Cha ajabu ni kwamba Kulola bado anawakandia kwa nguvu zote ili hata huko waliko waonekane kama wenye dhambi na Kulola aonekane Mtakatifu kuliko wote Tanzania

Mwakipesile Mbeya

Mwazembe Ajibu Mashambulizi

Name: Rev Mwazembe L.
Homepage:
Hometown: Dar
Sent: 15.46 - 1/10
"Siyo nia yangu kumpinga Kulola ili nisikike, Lakini ugumu ninaokumbana nao kwenye kazi hii ya kuhubiri hasa kwenye mikoa ya Tanzania, kwa sehemu Kulola amechangia kuwaaminisha Watanzania kuwa yeye peke yake ndiye mtumishi wa kweli na wengine ni wababaishaji tu. Huo ndio uongo kutoka kuzimu ambao ninaupinga kwa nguvu zangu zote." Ev. Mwazembe.


Ndugu Mwakipesille. Elewa kwamba kimaisha watu hawezi kufanana na miaka pia aliotumika mzee Kulola ni mingi huwezi ukamlinganisha na mtu alienza juzi pia mambo anayofanya sio wote wamepakwa kwa kiwango kile. Na hizo sadaka zinakuja kwa wingi kutokana na upako mkuu katika maisha yake. Pia ni haki yake kuchukua sadaka kutokana na neno la Mungu. Asnte sana.

Mwinjilisti Mwazembe

 

Naye Mchungaji Peter Mattimba Mchungaji Msaidizi Kanisa la Full Salvation Church Amuunga mkono Mwazembe na kusema:

Mahubiri ya Moses Kulola ni kikwazo kwa waumini wa Bwana wetu Yesu Kristu Hili ni jibu kwa Moses Kulola baada ya kusoma mahubiri yake kwenye gazeti la Nipashe Jumapili Aprili 23,2000 Uk.1 na 2.

Wafuasi wa Yesu walio waaminifu tuna mashaka sasa kadri tunavyoendelea kusikia mahubiri ya wale wanaoitwa watumishi wa Mungu, kwani wanakoelekea wameacha agizo walilopewa na kiongozi wetu Mkuu wa Imani yetu YESU KRISTO (Waebrania 12:2) Moses Kulola ni mmoja kati ya viongozi waliopo hapa nchini ambao huongoza na kusikilizwa na wafuasi wengi, naye hufanya mihadhara mbalimbali.

Hivyo chakusikitisha ni pale tunapoona baadhi ya mahubiri yake hayafundishi Imani ya YESU KRISTO badala yake huwakwaza. Labda uaskofu wake hakuwepa na Yesu Kristo bali ni kutoka kwa wanadamu tu ambao hawajui mapenzi ya Mungu yaliyo halisi. Kitendo alichofanya mhubiri huyo hapo Kidongo Chekundu (labda na sehemu nyingine pia) cha kufundisha watu kuwa Mwenyezi Mungu amewaweka wauguzi na madaktari ili kuwasaidia wagonjwa ni kitendo kinachomfanya asiwe mmoja wapo wa wafuasi wa Bwana wetu Yesu Kristo. kwani watumishi aliowaweka Yesu Kristo hapa duniani wawe mawakili wa siri za mbinguni ni hawa, Waefeso 4:11-16 'Naye alitoa wengine kuwa Wachungaji na Waalimu kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa kristo ujengwe..."

Biblia inatuonyesha wazi Bwana Yesu ndiye aliyewachagua kazi yake na amewapa kielelezo jinsi ya kufanya kazi. katika kitabu cha Mathayo 9:37 -38 na 10:1,7-8..Basi mwombeni Bwana na Mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili akawapa AMRI juu ya pepo wachafu, wawatoe, na KUPOZA MAGONJWA YOTE na udhaifu wa kila aina. Na katika kuenenda kwenu hubirini mkisema Ufalme wa Mungu umekaribia. Pezoni wagonjwa fufueni wafu, tukaseni wenye ukoma toeni pepo,mmepewa bure toeni bure".

Hii ndio maana hata Moses Kulola hukiri na kusema" wagonjwa na wenye shida mbalimbali wataombewa, karibuni wote" kwanini asiache wagonjwa waende hospitali, bali anawaita kuwaombea? Madaktari na wauguzi wamesomea na kupasishwa na wanadamu, Moses Kulola naye labda uaskofu wake amesomea; lakini wanafunzi wa Yesu Kristo au Mitume wake sio wa kusomea na kupewa shahada ya utumishi bali ni vipawa vya Roho Mtakatifu apewavyo muumini Je Moses Kulola (na kila mwenye imani hiyo) ni mfuasi mwenzetu wa Yesu Kristo? Mbona matunda yako (mahubiri) uliyonayo hayatokani na shina ambalo ni Yesu? Ikiwa wewe unamtilia mashaka Yesu kuwa hawezi au hatawaponya ukimwi eti kwa sababu umeingia kwa uzinzi je kama ni hivyo dhambi yenyewe ya uzinzi, Bwana Yesu atashindwa kuisamehe na kuifuta kabisa? Kama dhambi ambayo ni kazi ya shetani itamshinda je shetani mwenyewe hatapiga goti kwa Yesu? Sasa utueleze anamtumikia nani kama si imani haba!.

Sisi wanafunzi wa Yesu tulimpinga Kakobe pia aliposema ameanzisha operesheni ya kuwaombea na kuwaponya wagonjwa wa ukimwi huku akiwataka waende na vyeti toka kwa daktari, Sivyo bwana Yesu amesema 'Pozeni magonjwa yote nakila aina ya udhaifu' tena ana uwezo wa kusamehe dhambi zote kwani dawa ni maungamo tu. Hivyo natoa wito kwa watu wate kuwa wasibabaike kusikia jina la Askofu wa Kimataifa au Askofu Mkuu mwenye vyeti kutoka kwenye vyuo vya kidunia; kwani hao hawakutumwa na Bwana wetu Yesu Kristo bali ni wasomi tu wasio na Imani ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Hao wanaokiri kuwa wanamjua Yesu 'wenye mfano wa utumwa lakini wakikanga nguvu zake hao nao ujiepushe nao' 2Timotheo 3:5. Katika Biblia Musa alitumwa na Mungu kuwa aweke Nyoka wa Shaba juu ya mti pindi mtu aking'atwa na nyoka mwenye sumu, amtazamapo Nyoka wa Shaba apate uponyaji. huo ndio uwezo wa Mungu wa uponyaji tangu zamani. Kadhalika hata leo wagonjwa wa kila aina na wenye dhambi wote waende kwa Yesu (aliyewafia msalabani) kwa njia ya Imani wataokoka ndio kupona Bwana Yesu hasemi kama Moses Kulola au mmojawapo wa hao wasioamini kuwa ukipata Ukimwi kwa njia ya zinaa hata ukiombewa hutapona. NI UONGO MTUPU HUO labda ni agizo la chuo chao na na sio agizo la Bwana Yesu kamwe wala sio Injili ya kweli kwani hakuna ugonjwa usiotii mbele za Yesu.

Magonjwa ni kazi za shetani na waliopewa amri juu ya shetani hapa duniani sio madaktari na wauguzi bali ni wanafunzi wa Yesu tu. Bwana Yesu ameyachukua magonjwa yetu yote tena yeye ndiye Bwana atuponyae kwani ameweka wahudumu kanisani ili mtu akiugua awaite wazee (wahudumu) wamwombee wampake mafuta kwa Jina la Bwana Yesu (Yakobo 5:13-15), wazee wa kanisa sio madaktari. Wafuasi wa Yesu hapo sio kwamba hatutaki kwenda hospitali bali ipo njia ya waaminio ambayo hutoa uzima bure kwa njia ya imani ya Yesu. Tena ukiamini hatakuwa na haja ya madawa, kwani unao uzima wa mwili na roho katika Kristo. Mnaotegemea madawa ni wazi kuwa mmeshindwa katika imani (kiroho) na kuenenda kimwili, basi ni kweli na wazi Yesu ni yeye yule jana na leo nahata milele tena ana uwezo wa kusamehe dhambi kuponya magonjwa yote na kufufua wafu pia. Mwamini Yesu leo utaokoka Ameni Mchungaji Peter Mattimba Mchungaji Msaidizi Kanisa la Full Salvation Church. Kwa habari zaidi kuhusu KULOLA bonyeza hapa utoe maoni yako: http://amazingforums.com/forum/MUNISHI/forum.html

 

Ev.And Gospel Singer Faustin Munishi

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>