Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

Habari Zaidi

 Munishi siyo Mwanasiasa

Munishi Katika Picha

CCM imezeeka
haitufai
Tanzania


Serikali Kenya yatishia kubomoa kanisa la Pastor Muiru Yeye Husema KUNA NURU GIZANI Lakini sasa inaonekana giza nuruni


Mjue mch. Lusekelo


Bishop Mwasumbi


Mrs. Wilfred

Mazuri ya Nyerere?
Bishop

Katiba Mpya

River Road Gospel Tapes


Lenny Aokoka, Asema OGOPA DJ ni waabudu Shetani. Adai ilikuwa atolewe sadaka kwa Shetani ndipo Mungu alipomwita aokoke. Asema wasanii wengi wamekutana na vifo vyao katika mazingara ya kutatanisha Tena asema sasa atamwimbia Mungu badala ya BABY DONT GO!
Habari Zaidi



Rev.JB Masinde Nairobi inamwita BABA Kweli ni baba wa wengi kiroho


Mjue Bishop Arthur Kitonga


Miss Ester Gospel Singer Nairobi


Mrs. Saimon Gospel Singer Dar Er Salaam


Bishop Mark Kariuki Amzika Lianda

Rev. Lianda


Miss Lianda


Bishop Maboya


EV. Mrs. Doro


Mr. Meti

Mrs Meti


Bishop Wanjiru


Makala Tumaini Jema


Mch. Merisheki Kila akiwaza..



Nairobi Katika Picha


Mkuu wa kinamama TAG


Mr. Peter Ni Polisi tena ni Mhubiri Yuko Arusha mjini


Mrs. Lily


New Life Band Singer Arusha


Mhariri Victor wa 'Nyakati' wengi wanaliona gazeti hilo kama CCM ndani ya kivuli cha dini.

Kakobe Anayahonga Magazeti?


Pastor Nduati John Kigoi Afikishwa mahakamani kwa utapeli


Pastor Mwangi Aiaga Dunia Ajalini


Wazo la wiki na Dani Hagaeli


Mr. Dani

Mrs. Dani


Mr. John Mwangi Mwanzilishi wa Kenya Studio akumbukwa

Nyerere Online
Mjue Pastor Egesa
Polisi wampiga mchungaji risasi

gospelcom
CNN
TBN
BBC
Times
Islamtz.org
Winners
Maranatha
Intergrity

 

 



Gazeti la INJILI
Kwenye Internet

http://www.munishi.com

Tel. 254722602445 E-mail: munishi@munishi.com Or
info@munishi.com


Nyerere Aililia CCM akiwa kaburini

Rais wa 4 Tanzania awe raia" Munishi

Rais wa nne wa Tanzania Lazima awe raia" Mwinjilisti Faustin Munishi
"Zaburi 27:1-3 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini. Amen."

Munishi Magazetini

Polisi Nairobi wampiga mchungaji risasi: Ni Rev. David Jesse wa Kwanza

Injili inalinda maslahi ya Mungu duniani

Mwinjilisti na mwimbaji wa nyimbo za Injili Faustin Munishi
Injili inalinda maslahi ya Mungu duniani. Watu dunia na vyote vilivyoko ni mali ya Mungu. Hatuwezi kunyamaza wakati Mkapa na kundi lake wanapowaua waislamu zaidi ya 70 huko Zanzibar kwa sababu za kisiasa. Hata kama waliouawa siyo wakristo, lakini ni watu wa Mungu. Tukilinyamazia kesho itakuwa zamu yetu kuuawa. Hatuna nia kujiunga kwenye siasa, lakini wanasiasa wanapoyaingilia maslahi ya Mungu, chombo pekee kukemea hayo ni INJILI. Tunapowakemea wanasiasa, ndiyo tunaihubiri Injili. Tunaponyamaza ndiyo tumechanganya siasa na dini. Kwa hiyo sisi tunaokemea maovu yatendwayo na Mkapa, ndio tunaoihubiri Injili. Wale wanaowaunga Mkono kina Mkapa na kikosi chake cha mauaji ndio tunaotakiwa kuwaambia waachane na siasa kwani itawatoa katika kweli. Nasikitika kusema kwamba tayari wameshatoka katika kweli. Kwa hiyo siwezi kuacha kuyakemea maovu wanasiasa wayatendeayo jamii. Nikifanya hivyo nitakuwa nimekoma kuihubiri Injili.

Askofu Kulola huipigia debe CCM


Nani anamdanganya nani? Askofu Moses Kulola na mkewe wakikumbatiana na aliyekuwa askofu wa TAG Tanzania, Emanuel Lazaro na mkewe. Wanaoangalia ni Askofu Kitonga (wa pili kulia) Pia alikuwepo mlinzi maalum wa Askofu Kulola anayejulikana kwa jina moja tu ALEX. Bila hata kuambiwa, sura yake tu inaonyesha yuko kazini. Wenzake wanacheka, lakini yeye hacheki na watu. Ana sura ya mawe. (Ni wa kwanza kulia.) CCM tangu wakati wa Nyerere, ilimpatia Kulola walinzi wanaolipwa na serikali, ili akipigie debe chama hicho. Kulola alikaidi uongozi wa TAG ikazuka vita kati yake na Askofu Emanuel Lazaro. Serikali ilimpendelea kulola kwani alidai misaada mingi kutoka Marekani ilikuwa na lengo la kupenyeza CIA Tanzania kwa kutumia TAG. Nyerere aliinunua hiyo jumla kwani sera zake za ujamaa zilizoshindwa zilikuwa zikihofu sana Marekani wasijeleta ubepari Tanzania. Kulola alionekana malaika wakati Lazaro serikali ilimuona shetani. Lazaro alikwamishwa mpaka alipoachia ngazi ya uaskofu. Kulola mpaka leo anafaidi uongo wake wa kuidanganya serikali kwamba CIA walimtumia Lazaro. Ukiyasikiliza mahubiri ya kulola kwa makini, utakuta anawalisha waumini siasa za CCM bila wao kujua. Kulola ndiye mhubiri wa DOLA Tanzania. Mikutano yake inalindwa na kikosi maalum, Yeye mwenyewe analindwa kila aendako, Ni kipenzi cha CCM. Tuombe iwe hata mbinguni Mungu atampa heshima anayopewa na CCM. Vinginevyo atakuwa ameshavuna duniani. Mkewe Kulola anasadikiwa kuwa na pea elfu tatu za vitenge na khanga. Kila mkutano washirika hulazimishwa kununua vitenge na zawadi nyingine kwa mama askofu. Inasemekana kwamba kina Mwasota walikosana na Kulola pale na wao walipopewa zawadi za vitenge na ikaonekana mke wa Mwasota anashindana na mama askofu kimavazi na ndipo Mwasota alipotimuliwa. Inasemekana kwamba mke wa kulola hupenda kuonekana amewazidi wote kimavazi. Nchini Kenya Kitonga aliipamba sana KANU na alikuwa mhubiri wa dola Kenya. Tangu KANU waachie ngazi Kitonga yuko nje ya duara la madaraka. Habari zaidi


Wapinzani Tanzania wanapinga nini?


Farida asema hakuna kama Yesu

Huko kwenye ulimwengu mwingine alijulikana kama malkia wa chakacha. sasa amezaliwa mara ya pili na anaimba nyimbo za injili. Mwislamu wa kuzaliwa, anasema yeye siyo mwislamu wa kwanza kujiunga na Ukristo. Habari zaidi

Usafiri Nairobi-MATATU

Kila kitu ndani ya Matatu ni haraka. Kuingia haraka, kulipa haraka, na kushuka haraka. Ukifika Nairobi usisahau haraka ya Matatu. Wao husema Haraka ina baraka. Sera mpya za usafiri Kenya zinaonekana kuhamisha tatizo kutoka kwenye MATATU na kulihamishia kwenye Treni. Sijui watakapolihamisha kwenye Treni tatizo sugu la usafiri wataliahamishia wapi? Habari zaidi


Serikali yatatiza usafiri Kenya
Kufuatia agizo la serikali kwamba MATATU zote ziwekwe vithibiti mwendo pamoja na mikanda, Sekta ya usafiri Kenya imetatizika. Ni tatizo ambalo halitegemewi kuisha karibuni. Barabara ni mbovu, Magari ni machache, kuyaongeza hakuna pa kuyaegesha, Treni haziwezi kukithi mahitaji ya usafiri Abiria ni wengi kuliko vyombo vya usafiri vilivyoko. Badala ya kuwapunguzia matatizo, hatua ya serikali inaonekana kuyaongeza. Maisha ya abiria sasa yako hatarini zaidi kama picha inavyoonyesha.Ni matumaini yetu kwamba hatua za haraka zitachukuliwa kurejesha hali ya kawaida katika sekta ya usafiri Kenya. Kwingineko tume ya kurekebisha katiba ilikumbwa na utata pale serikali ilipojiengua ikidai kwamba matakwa yake yamepingwa kwa wingi wa kura. Inaonekana nia ya serikali ni kuwalazimishia wajumbe matakwa yao. Je watafanikiwa? HABARI ZAIDI

Hotuba Ya Munishi kwa taifa 'Ujamaa ulishindwa'

Mwinjilisti Faustin Munishi Mwimbaji wa nyimbo za injili aliyetia fora Afrika mashariki na kati.Nyimbo zake zenye maonyo zimegusa mioyo ya wengi, na safari hii kanda yake toleo la saba imewagusa pabaya serikali ya Tanzania. Wimbo MPENDE ADUI unasema CCM aliyoanzisha Nyerere, sasa imezeeka na sera za ujamaa ziliharibu Tanzania.Ukiwasikia watumishi wa Mungu wakiteta, Jueni kuna jambo. Mungu atawashughulikia wanaowatesa watanzania. Hakuna linalomshinda. Siyo Mkapa wala CCM. Kwake hao ni mvuke unaopita. Watayeyuka mara.

Nation Lageuka kuwa Gazeti la chama na serikali
Hatutegemei kazi ya gazeti iwe ni kuipinga serikali tu, Sambamba na hilo hatutegemei gazeti liwe linaimba sifa za serikali hata pale serikali inapokosea. Nation wanafanya hivyo bila haya. Tangu serikali mpya waingie madarakani gazeti la Nation limekuwa likiyafumbia macho makosa yao, huku wenzao Standard wakiwa mstari wa mbele kuyakemea. Baada ya Nation kuisoma "Stori" hii, Kiranja wao Wilfred Kiboro alikasirishwa sana. Haraka aliamuru sera za gazeti hilo zibadilishwe na kuanza kuikemea serikali. Sasa kama hawaikemei serikali kwa sera mbovu za usafiri, Kiboro mwenyewe anakuwa habari, kama siyo habari kuwa Kiboro. Walianza na Kibaki mwenyewe pale waliporipoti kwamba aliporomoka kwenye ngazi za Ikulu na kutonesha majeraha ambayo tayari alikuwa nayo. Serikali iliwapuuza kwani ilikuwa na kazi ya kuwanyamazisha Standard waliokuwa wamezidi na kelele zao. Ni ukweli usiopingika kwamba Nation ya Kiboro inaboronga na inaporomoka, huku Standard wakijigamba kwamba wameshika usukani. Sijui kama wasomaji watarudisha imani yao kwa Nation tena. Tunasubiri tuone. Serikali ni kama inafanikiwa. Kwani Standard nao wanaonekana kwamba mdomo waliokuwa wakiupanua sana kupiga kelele, umewekwa kitu, na sasa sauti haitoki sawasawa. Kwamba wanaopinga ndio wanaozawadiwa, inaonekana kuwaumiza Nation na CITIZEN. Sasa wameanza kupinga. Lakini wakiwa wamechelewa. Nani aliwadanganya wanasiasa watakumbuka fadhila? Wanajidai kuwasaidia Kana kwamba wanajitetea, Nation waliandika kuhusu mhariri wa gazeti hili na kujaribu kuichambua web site hii. Lengo ni kuonyesha kwamba mkuki kwa Nguruwe ni sawa, lakini kwao ni wa uchungu. Habari zaidi

Rev.Wachira asema magazeti yanapaswa kuikosoa serikali, kwani hata kama serikali ingeundwa na malaika, bado inahitaji chombo cha kuikosoa isiende mrama. Ni makosa kufikiri kwamba serikali mpya haijafanya makosa. Kwangu tayari wamefanya makosa mengi kwa mwaka mmoja madarakani. Mwaka wa pili utakuwa kuvunja rekodi ya makosa yaliyofanywa na serikali za awali.Tusubiri hadi wavunje rekodi ndipo tuikosoe?



Toa Maoni yako hapa na hakuna atakaeyahariri


Mzee Mbise ameiaga dunia lakini....

Mchungaji Edward Mbise Atakumbukwa daima kwa misimamo katika yale aliyoyaamini. Misingi aliyoijenga kwa watoto wake matunda yanaonekana wazi. Ni shujaa ambaye hakuogopa kuutetea ukweli. Tukitaka kumuenzi lazima tuige mfano wake.Watoto wake wanakiri kwamba sasa wametambua kwamba ukali wa mzee umekuwa na faida kubwa kwao. Wanajitegemea kimaisha, na hali yao ni bora kuliko ya marehemu baba yao. Mtu hapimwi kwa mali alizoacha, bali mifano ya kuigwa aliyoiacha. Mzee Mbise ameacha mifano mingi ya kuigwa. Alikuwa mchungaji aliyezaliwa mara yapili, Lakini pia alikuwa mwanachama wa CCM. Wakati wote wa kuugua na kulazwa katika hospitali ya KCMC Moshi, CCM hawakuwepo kumjulia hali. Kwenye mazishi yake ambayo yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu, CCM walijikomba kuweka bendera ya chama chao kwenye Jeneza la Marehemu. Huo ulikuwa unafiki au kulia machozi ya mamba. Mzee Mbise mkazi wa Ngarenaro Arusha, alizikwa kwenye shamba lake SOKON ONE Mjini Arusha. Cha ajabu ni kwamba CCM hawakuruhusu bendera ya chama chao izikwe pamoja na marehemu. Mwili wa marehemu ulipoanza kuwekwa kaburini, Haraka waliiondoa bendera yao. CCM inaogopa kuwekwa kaburini lakini wanaelekea hapo. Tangulia Mzee. CCM chama chako watakufuata haraka.
Tangaza Biashara yako Bure
Tuma picha na maelezo kwa munishifaustin@yahoo.com

http://munishi.com FREE!
Send photo and information to
munishifaustin@yahoo.com
Upako Unaotimua mapepo


Mch. Faustin Panga wa JESUS TOUCH THE WORLD MINISTRY akiwaombea wenye mahitaji maishani. Hapana hajazimia. Ni baada ya kuombewa, nguvu za kusimama zikamwishia na akajikuta chini. Mama huyu ambaye hatukuweza kupata jina lake ni mmoja wa wale wanaohudhuria ibada katika kanisa la JESUS TOUCH THE WORLD MINISTRY Huko Mombasa Kenya. Kwa sasa kanisa hilo ndilo linalokua kwa kasi ya kutisha Mombasa. Linakaribia kuyapita makanisa kama JCC linaloongozwa na Lai, Pamoja na lile la Neno linaloongozwa na aliyekuwa mfungwa zamani Mchungaji James Maina Ng'ang'a.

Pastor Maina Ng'ang'a wa kwanza kushoto, Mchungaji Faustin Panga katikati, Na Wilfred Lai. Hawa ndio wanaoitikisa Mombasa kwa Injili. Karata ya ukabila bado ndiyo inayotawala Mombasa. Kanisa la Ng'ang'a linafadhiliwa zaidi na jamii ya Wakikuyu, wakati lile la Lai nalo linasimamishwa na Wakamba. Mchungaji Panga naye anategemea makabila yote kwani yeye anatoka Jamhuri ya Kongo ambao ni wachache Mombasa. Akiongea na gazeti hili, Mchungaji Panga alisema anapanga kumtegemea Mungu zaidi kuliko kuwategemea watu wa kabila lake.


EV. Jeff Waciama atinga Dar


Mwinjilisti na Mwimbaji wa nyimbo za Injili Jeff Macharia.
Kwa sasa yuko Dar nchini Tanzania, Anadai Mungu amemwita kuihubiri Injili huko.Atakumbukwa kwa wimbo wake uliovuma sana Kenya JESU NIWACIAMA. Ni wimbo aliouimba kwa lugha ya Kikuyu ukiwa na maana Yesu ni wa miujiza. Kwenye huduma yake amekumbana na milima na mabonde, Lakini bado yuko. Mengine anadai amesingiziwa, Lakini mengine anakiri ni udhaifu wake kama mwanadamu. Msikie asemavyo."Siyo kwamba sijaona mengi ya kunitenga na Mungu, Nimeyaona. Lakini nimeamua kusimama imara nikiyasahau yaliyopita na kuyaendea yaliyo mbele." Huyo ni Jeff Waciama

RHM Walaumiwa kuwanyanyasa wasanii

Mkurugenzi wa Redio Habari Maalum Bwana DD Digulla

Wasanii walioingia mikataba nao wanadai asilimia kumi wanayolipwa kwa kila kanda inayouzwa na RHM Tanzania haitoshi. Tena hawana namna ya kujua wameuza kanda ngapi. Isitoshe wamegundua kwamba kanda zao zinauzwa nje ya Tanzania na hawalipwi chochote. Wasanii wanasema sasa basi. Inatosha. Wanataka walipwe haki zao au wachukue hatua za kisheria.
. Msomaji una maoni gani kuhusu tuhuma hizi?

Naye msanii wa nyimbo za Injili Bwana Shari Martin ameliambia gazeti hili kwamba Digulla anayeingia mikataba na wahindi ili kughoshi kanda zake Tanzania, siyo Bwana DD Digulla ambaye ni mkurugenzi wa RHM bali ni majina tu yanayofanana. Aliongeza kwamba huyo tapeli hata picha yake anayo, na yuko mbioni kumchukulia hatua za kisheria. Ila habari nyingine zinadai kwamba Digulla tapeli ni ndugu wa damu wa DD Digulla mkurugezi RHM. Ikifikia hapo, kila mtu ataubeba msalaba wake. Mungu atusaidie nyakati hizi za mwisho.
KASIWUKIRA KILLING THE MUSIC

Apart from RHM from Tanzania, There is also KASIWUKIRA LTD from Kampala Uganda. This company pirates music like hell. Ask them why? The answer is "Every body is doing it, why not KASIWUKIRA LTD?" WHAT DO YUO SAY?

Censorship turning systematic in Tanzania

Mr.&Mrs. Faustin S. Munishi His Gospel tape was banned by Tanzanian goverment

Apollo Joo Akumbukwa

Mtume Joe Kayo, Mwinjilisti na mwimbaji Munishi, Na Marehemu Apollo Joo

Habari Katika Picha

Kiraeli Carol 1989, Munishi 1974, Sister to Kiraeli 1989, Salelo, Mojashi 1995

Wakenya wasema ni Kibaki

Wakenya wamesema ni Kibaki. Tuheshimu sauti ya wengi, Na viongozi wajue kwamba mwajiri wao ni wananchi. Ni mwanzo mpya kwa Kenya, na itakuwa mwanzo mpya kwa Afrika mashariki. Yaliyotokea Kenya lazima yatokee Tanzania. Wembe ulioinyoa KANU, Utainyoa CCM na Mkapa. Tunaiombea serikali mpya Kenya, Tunamuombea Rais Emilio Kibaki. Mungu awasaidie washindie mtihani wa kwanza unaotishia kuuvunja muungano wao. Wananchi waliuchagua umoja wao ni siyo mtu binafsi. Yeyote asijisahau ajione bora kuliko wengine. Kilichoshinda ni umoja na mshikamano. Ni matumaini yetu kwamba ushindi huo utadumishwa kwa kila hali. Mungu ibariki Kenya, Na utusaidie kuikomboa Tanzania.


Kibaki akila kiapo cha kuiongoza Kenya katika ENZI MPYA. Pongezi mheshimiwa. Majeshi yote saluti ni kwako. Waandishi wote kalamu zetu ziko tayari. Siyo tu kukusifia, ikibidi tutakosoa. Wembe uliomnyoa MOI, sasa utaelekezwa kwako. Ichunge KBC, lakini usiitumie kama fimbo. "NATION" wape masafa, watangaze nchi nzima. Usituogope wanamedia, ila tuheshimiane. Kusudi letu ni moja, umma kuhudumia. Habari msitunyime, tuziandike sahihi. Tukiwaita kwenye simu, acheni kupuuzia. Matarajio ni mengi, na yote ni ya muhimu. HABARI ZAIDI

Mkapa Anatuibia Kiutandawizi

Yaliyotokea Kenya lazima yatokee Tanzania. Wembe ulioinyoa KANU, Utainyoa CCM na Mkapa. Watanzania tumechoka na matesom ya CCM. Majuzi Mkapa aliwaua waislamu zaidi ya 70 huko Zanzibar. Kosa lao ilikuwa kusema kwamba CCM imezeeka hawaitaki.
Nyani ni hodari kuparamia miti, lakini siku yake ikifika miti yote huteleza. CCM mwisho wao umefika. Kila wanaloparamia linateleza na watabamiza chini kwa kishindo.

"Too appalling this letdown, Ndugu Mkapa"

Mr Philip Ochieng. Mwandishi wa habari wa siku nyingi afrika mashariki. Kwenye miaka ya sabini waliwahi kufanya kazi kwenye gazeti la DAILY NEWS pamoja na Mkapa. Wote walitumika kama kinywa cha Nyerere kusambaza sera zake za ujamaa. Ochieng aliona mbali, Akauona ujamaa ukielekea kushindwa, na akaanza kusema hivyo. Nyerere alimfuta kazi na kumtimua Tanzania. Alirudi kwao Kenya na mpaka leo ni mwandishi wa makala katika gazeti linaloheshimiwa sana afrika mashariki NATION. Anamshangaa mwandishi mwenzake Mkapa jinsi alivyolewa madaraka mpaka kufikia kiwango cha kuwatesa waandishi wa habari wenzake. Anamsema sana Mkapa kwamba anaiaibisha taaluma ya uandishi. Habari Zaidi

Serikali yabomoa Makanisa Arusha

Mchungaji Emanuel Nnko wa kanisa la Beroya EAGT Arusha. Kanisa lake ni moja ya makanisa yaliyokumbwa na bomoa bomoa ya makanisa mjini Arusha. Kwa sasa anapanga kuishitaki serikali kwa Mungu, Halafu mahakama kuu ya Tanzania. Suala lake amelifikisha kwa wanaohusika lakini bila mafanikio ya kurudishiwa hata vyombo vya kanisa walivyobeba. "Je Tanzania kuna uhuru wa kuabudu kama katiba yetu inavyosema?" Aliuliza Mchungaji Nnko alipolitembelea gazeti la Injili Nairobi Kenya.

Nyerere aliiharibu Tanzania

Mwalimu Nyerere: Sera za ujamaa zilishindwa kabisa Tanzania
Aliyegundua umeme ni binadamu kama aliyeanzisha siasa ya ujamaa Tanzania. Wote wamekufa na yale waliyoyafanya duniani ndiyo yanayotufanya tuwasifu au tuwaite wapumbavu. Nyerere ni MPUMBAVU kwa sababu yote aliyoanzisha hayapo kumtetea. Yako wapi maduka ya Ushirika? Viko wapi vijiji vya ujamaa? Iko wapi RTC? Na mashirika ya umma je yako wapi? Mashamba aliyotaifisha au tusema aliyowanyanganya wazungu yako wapi? HUO NDIO ULIOKUWA UPUMBAVU WA NYERERE. Nchimbi atembee kwa miguu kutoka Dar mpaka Musoma haibadilishi chochote. Nyerere atabaki MPUMBAVU. Mkapa ajaribu kila hali kuzitetea sara zake mbovu haisaidii. Nyerere atabaki MPUMBAVU aliyewahi kuishi Tanzania. Mwisho nikimalizia , viko wapi vibali ambavyo kila aliyetaka kununua sukari kwenye maduka ya ushirika alipaswa kuwa navyo. Utawala wa Nyerere ulikuwa mbaya kiasi kwamba kilo mbili za sukari ungezipata baada ya kuonyesha kibali kutoka kwa mkuu wa wilaya. Tulioishi nyakati hizo, ilikuwa sawa na kuishi Jehanamu. Hoteli kubwa zilikuwa zinauza chai na mihogo badala ya mikate. Cha yenyewe ilikuwa ni ya sukari guru. Ilikuwa ukiwa na pesa na asiyekuwa nazo nyote sawa. Huo ndio uliokuwa wendawazimu wa Julias Kambarage Nyerere.

Nilipata Mateso Makali jela

Samwel Kariuki adai kupata mateso mengi jela.

Serikali Kenya Darubini kwa Ng'ang'a

Kushoto ni Pastor James Maina Ng'ang'a, wakiwa na kiongozi wa kundi la MUNGIKI.
Mchungaji Maina Nganga alianzia Mombasa na sasa yuko Nairobi. Kanisa la Mombasa limefifia huku washirika wakihamia makanisa mengine. Aliyefaidi sana Mombasa ni mchungaji Panga ambaye washirika wengi wa Nganga wamehamia kwake. MTAKA YOTE HUKOSA YOTE ndivyo wanavyosema Mombasa. Wengine wanasema TAMAA ILIMPONZA FISI. Naye mchungaji Nganga anasema sasa Mungu amemwita Nairobi, na Mombasa ikae. Nayo serikali ya Kenya imekuwa ikimfuatilia kwa karibu mchungaji Ng'ang'a baada ya kiongozi wa kundi la Mungiki kudai ameokoka na kujiunga na kanisa la Ng'ang'a. Wanaiona hiyo kama mbinu ya MUNGIKI kuja na sura mpya ya kanisa la Neno Evangelism.

Injili inalinda maslahi ya Mungu duniani

Mwinjilisti na mwimbaji wa nyimbo za Injili Faustin Munishi
Injili inalinda maslahi ya Mungu duniani. Watu dunia na vyote vilivyoko ni mali ya Mungu. Hatuwezi kunyamaza wakati Mkapa na kundi lake wanapowaua waislamu zaidi ya 70 huko Zanzibar kwa sababu za kisiasa. Hata kama waliouawa siyo wakristo, lakini ni watu wa Mungu. Tukilinyamazia kesho itakuwa zamu yetu kuuawa. Hatuna nia kujiunga kwenye siasa, lakini wanasiasa wanapoyaingilia maslahi ya Mungu, chombo pekee kukemea hayo ni INJILI. Tunapowakemea wanasiasa, ndiyo tunaihubiri Injili. Tunaponyamaza ndiyo tumechanganya siasa na dini. Kwa hiyo sisi tunaokemea maovu yatendwayo na Mkapa, ndio tunaoihubiri Injili. Wale wanaowaunga Mkono kina Mkapa na kikosi chake cha mauaji ndio tunaotakiwa kuwaambia waachane na siasa kwani itawatoa katika kweli. Nasikitika kusema kwamba tayari wameshatoka katika kweli. Kwa hiyo siwezi kuacha kuyakemea maovu wanasiasa wayatendeayo jamii. Nikifanya hivyo nitakuwa nimekoma kuihubiri Injili.



Rais wa 4 Tanzania awe raia" Munishi
Rais wa nne wa Tanzania Lazima awe raia" Mwinjilisti Faustin Munishi
"Zaburi 27:1-3 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini. Amen."


Kenedy Ochieng na Apollo Joo waaga dunia Bonyeza Picha usome Story

Biblia Inasemaje? Polisi ampiga mchungaji risasi Ukimwi Unaua Jiadhari- KENEDY ... Askofu Kulola Alaumiwa Mjue Pastor Ekesa ... Mwinyi Aliibadili Tanzania ... Nation TV Yakosa Mwelekeo ... Siasa na Dini Zitenganishwe? Kweli serikali haina dini? ... Waislam Wampora Mkisto Nyumba ... Nyerere Msingi aloujenga Haufai Tuubomoe? ... Mjue Kaka Paul ... "Nisaidieni Nioe" Asema Jeff WACIAMA... Mkapa Hatoki Muda Ukiisha ... Marandu T.L Ajitoa Kwenye "FORUM"Kisha Akarudi Tena...MUNISHI AZINDUA HERALD ... Majira Wajaribu Kumzima Munishi? ...Professor Oloo Amlaumu Mwinyi ... Taliban Wamefanya Kiungu, Amerika walifanya kishetani ... Philip Ochieng attacks Mkapa- ...Moi Aombewa Amalize Vizuri ...Rodnat Mwenda Amshambulia Munishi...SIKU TATU BAADAYE Majambazi Wamvamia Munishi Nyumbani... NYERERE ALISHINDWA MENGI... Leila Asema Alikuwa Shujaa... Wengi Wampinga Leila... EAGT Dodoma kunafuka Moshi ... ASKOFU KULOLA AMTIMUA MCHUNGAJI ARUSHA ...Mwazembe Amtetea Kulola NAYE MWAKIPESILE ASEMA EAGT IMEOZA...Kwa Nini Waislamu Wanalalamika? KITABU HIKI MARUFUKU TANZANIA... Hofu ya Mabomu Imetanda Dar es Salaam SERIKALI YALAUMIWA KUWANYANYASA WAISLAMU ... Amerika Siyo Mungu WENGI WASEMA IJILAUMU YENYEWE. ISIPOBADILI SERA MAMBO BADO Gazeti la Nation Lasema Kenya Ilikosea Kutangaza Msimamo Haraka....NALO GAZETI LA An-Nuur Lamwita Osama Shujaa Na Mpigania Haki...YESU NI MUNGU?... Haki za Wanaume... POLISI TANZANIA WALIUA ZAIDI YA70 HUKO ZANZIBAR Serikali Ilihusika Na Mauaji Ya Raia Wasio Na Hatia...CCM ILIWAITA WALIOUAWA MAGHAIDI... Serikali Inayoua Raia Haifai WENGI WANAOMBA MUNGU AIANGUSHE CCM ...Mkapa Asema Nguvu Za Dola Zitamshinda Mungu... Waziri wa Viwanda TZ Amejiuzulu ... WorldSpace Hawajui Wamlenge Nani ... Dani Hagael Amsaga Askofu Habari Katika Picha ... Mrema Awapongeza Afghanistan ... CUF Kujitoa katika muafaka-... Gospel tape banned by Dar officials ... Tembelea Web Site zetu mpya kwa habari zaidi: http://ktn2.netfirms.com http://nipashe.netfirms.com munishifaustin.netfirms.com

Contact us/ Tuandikie

Full Name
E-mail
Subject
Message
   
   



 
| http://munishi.com |