Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

Gazeti la INJILI
Kwenye Internet

http://www.munishi.com

Tel. 254722602445 E-mail:fmunishi@hotmail.com Or
munishifaustin@yahoo.com

Askofu Deya Matatani


Bwana Deya
Eti Wanauza Watoto?

Ach Bishop Deya akihubiri Mombasa mwaka 2002.Wachungaji Mombasa waliususia mkutano wake, isipokuwa Apostel James Maina Nganga aliyeungana naye kwenye mkutano huo. Inasemekana kwamba baada ya mkutano huo Deya alirudi London, na hapo ikawa ndio mwanzo wa Nganga kuonekana KBC. Inasemekana kwamba malipo ya kwanza ya AIR time Deya alimlipia Nganga. Hatujui mambo yaliendaje, lakini tunasikia kwamba kwa sasa Nganga anajilipia mwenyewe. Na uhusiano kati ya wahubiri hawa wawili siyo wa karibu kama mwanzo.

Mchungaji Apolo Joo Ambaye ni marehemu, ndiye aliyemuuzia Deya usajili wa kanisa. Alisajili kanisa lake enzi za Kenyatta, na likamshinda kuendesha na alikuwa tu na cheti cha usajili. Inasemekana alimuuzia deya kanisa hilo kwa bei ya KSHs. 40,000. Naye Deya bila kupoteza wakati alienda kwa msajili wa vyama na kubadili majina ya Apollo joo na kubandika ya kwake. Wakati Apolo joo alikuwa askofu wa kanisa hilo, Deya aliona abadili na akajibandika ARCH BISHOP DEYA. Wakati unaponunua kanisa, unaweza kujiita chochote. Nashangaa kwa nini hakujiita POPE.

Sasa kuna sakata la watoto wa kimiujiza. Gazeti la injili kwa sasa halisemi chochote mpaka tuwasiliane na Deya. Kila juhudi zinafanywa ili tuweze kumpata Deya kwa mahojiano.


Achbishop Deya Gilbert

Je watu wanamsakama bure? Kwa nini? Je kweli Mungu hufanya miujiza? Kazi ya Mungu kutenda miujiza itahadhiriwa vipi na sakata hili la Deya? Tuseme kweli ni miujiza ya Mungu. Kanisani kwa Deya miujiza pekee ni ya watoto? au kuna miujiza mingine? Mbona hatusikii kashfa za miujiza aina nyingine isipokuwa ya watoto? Haya na mengine mengi ndiyo maswali yanayoumiza vichwa vya wengi. Ukweli utajulikana umuweke Bishop Deya huru.
Contact us/ tuandikie

Your full Names
Your E-mail
Subject
Message
   
 

NAME: Wilson . P. Balihagati
E-MAIL: wilson_enos@hotmail.com
SUBJECT: Deya

Ukweli watu wengi tumechanganyikiwa na hilo suala. Mungu anatenda miujiza mikubwa kuliko hii ambayo leo Deya anashambuliwa nayo. Yesu alifufua wafu, aliponya viwete, wakoma, na magonjwa mbalimbali. Siwezi kuona ajabu hata kidogo kama Deya naye kwa kutumia jina la Yesu ameweza kufanya hivyo. Nimefika kanisani kwa Deya hapa London na kuona maajabu mengi yakitokea madhabahuni kama kuponya watu fibroid, magonjwa ya ngozi, mapepo nk. Hili la watoto kama mnataka kuamini njooni kanisani kwa Deya kuna mama ana miaka 54 na katika muda wake wote alikuwa hajapata kizazi na baada ya maombi sasa hivi ana mimba, sasa mtasemaje na hilo?. Kuna watu walikuwa na HIV/ AIDS na sasa wamepona kabisa baada ya maombi mtasemaje kwa hilo tena? Jamani muacheni Deya kweli mungu anamtumia kwani hata Yesu aliwaambia wanafunzi wake enendeni mkahubiri injili na mtatenda memngi kuliko niliyotenda.

Hayo ni maoni yake Bwana Wilson.P.Balihagati. Wewe unasemaje? Tuandikie kuhusiana na sakata hili la watoto wa kimiujiza nasi tutachapisha maoni yako hapa. Ikiwezekana taja mahali ulipo.

NAME:Brian Kithuku
E-MAIL:bkithuku@yahoo.com
SUBJECT:Deya
Mimi ni Mkristo ninayeishi Arusha. Sina shaka kuhusu miujiza inayoweza kufanywa katika jina la Yesu, lakini natambua pia kwamba udanganyifu na utapeli vyawezekana pia. Utabiri kuhusu manabii wa uongo umetajwa mara nyingi katika Biblia. Twawezaje kuzitambua roho za aina mbalimbali zitumikazo hata katika miujiza? Tukilikabidhi swala hili kwa Roho Mtakatifu katika maombi ukweli wote utawekwa wazi mbele yetu kuhusu Deya.


NAME:Peter. M. Mwangi
E-MAIL:
pitamuryumwangi@yahoo.com
SUBJECT:Deya and the miracle babies
Well,there are times when just a mere comment on deeds regarding God's miracles need not be a major debate any longer. God is the author and perfector of everything. You can not case for him. He has power to do anything to defend his name for its a great one and cannot just seat back and watch it being tanished by simple human beings out in search of "quick wealth". Gilbert Deya is a man of God as he claims to be. We cannot start scrutinizing his secret ways with God. One thing is real : - The wicked will not go far in their wickedness. It will soon (wickedness) fight them back and we shall know the wheat and the chaff. Just as Eli said about his wicked children - Phinehas and Hophni - that May God deal with them , I also say them May the Lord God Deal with the Ministers of the Gospel who tarnish his great name. Thank you.

 
| http://munishi.com |