Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Sikiliza waongo


Ukimwi unaua: Asema Kenedy Ochieng


Gazeti INJILI
Kwenye Internet
-


http://www.munishi.com

Tel. 254-722-602445 E-mail:
munishi@munishi.com


Waki ametibua maji. Sioni yakitulia karibuni.Kibaki atakuwa wa kwanza kwenye ndege inayoelekea kwenye mahakama ya kimataifa.Katika kipindi cha uongozi wake alichochea cheche za kikabila zilizopelekea hali ya kisiasa Kenya kuzidi kuegemea misingi ya kikabila.Mbaya kuliko yote ni kukiuka MoU ambayo alikubaliana na viongozi wenzake. Alipoingia madarakani siyo tu alikiuka MoU, bali aliwatimua serikalini wale walioonekana kuuliza kulikoni. Yote hayo ndiyo yaliyozaa upinzani uliojulikana kama ODM. Uchaguzi ulifanyika huku kura za maoni zikionesha ODM ni maarufu na watashinda uchaguzi kwa kishindo. Kibaki anajua alifanyaje ikawa ilivyokuwa. Wakenya walihisi kuibiwa haki yao ya kupiga kura. Hasira yao na ya wale waliotaka kubaki madarakani kwa gharama yeyote, ilipelekea watu zaidi ya 2000 kupoteza maisha yao.Jamii ya kimataifa iliingilia kati na kumlazimisha Kibaki kugawa madaraka kati kati. Kichwa upande akakubali. Asijue ameingia kwenye mtego wa Amerika. Ofisi ya waziri mkuu ililazimishiwa kwenye katiba ya Kenya. Japo wanaoigharamia ni Amerika, sasa wanataka mapendekezo ya tume ya Waki kutekelezwa. Walioorodheshwa kwenye bahasha ya siri aliyokabithiwa Kofi Annan, lazima washitakiwe kwenye mahakama ya kimataifa. Hayo ni kwa mujibu wa Amerika, japo baadhi ya wabunge Kenya wameanza kuimwagia maji baridi ripoti hiyo. Je itapoa? Hilo ndilo swali la wengi. Inaonekana Marekani wamepania kuwachukulia hatua wote waliohusika kusababisha ghasia za kisiasa Kenya.Haishangazi kuona watu wa kabila fulani Kenya hawafurahii sana Obama kushinda uchaguzi wa Amerika. Wanauona huo kama mwisho wao.Mungu ibariki Kenya.Je Marekani wana haki gani kumkamata KIBAKI na kumfurusha kwenye mahakama ya kimataifa? Wanadai wao ni wanademokrasia halisi. Mbona na wao walikuwa wakiunga mkono ODM na inadaiwa walikuwa wakiwamwagia pesa za kampeni? Hilo siyo kosa kwani PNU nao walikuwa wakiungwa mkono na kupewa pesa nyingi kutoka CHINA.Hata hilo siyo kosa kwa mtizamo wa wengi. Kwangu hayo ni makosa makubwa. Na kama tume ya waki haikuyaangalia hayo, basi wanaopaswa kushitakiwa watabaki na wanyonge watasulubiwa badala yao. Haki na uhuru wa uchaguzi ni pale wananchi wanaporuhusiwa kuchagua bila kushawishiwa kipesa wala kutapeliwa na MEDIA zilizonunuliwa. Huwezi kutumia nafasi yako kama rais wa Jamhuri ya Kenya kuvuruga uchaguzi, Halafu utumie nafasi hiyo kuunda tume ya kuchunguza yaliyojiri baada ya uchaguzi kutoa matokeo yenye utata, kisha utegemee matokeo ya tume yatakupendelea na kuyafunika makosa yako. Kwamba tume ya waki ilimtaja KIBAKI kama kiongozi aliyevuruga siasa za Kenya na kupelekea wakenya kuuana kwa misingi ya kikabila, hilo ndilo ambalo wengi tunalipongeza. Kazi ya rais ni kulinda katiba ambayo ndiyo mhimili wa nchi. Haki za kisiasa hupatikana wakati sheria kulingana na katiba zinapofuatwa.Rais akiikiuka katiba, atumie vyombo vya dola kubaki madarakani kwa gharama yeyote, Anategemea nani afuate katiba? Kila mtu itakuwa mguu niponye, wengine itakuwa pesa niponye, na kwa wanasiasa itakuwa majeshi binafsi niponye.Ilikuwa hivyo Kenya wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi.Mbaya zaidi hata vyombo vya dola ambavyo hupaswa kuwalinda wananchi wote, navyo vilijikuta vikiegemea upande wa amiri jeshi mkuu ambaye alikuwa KIBAKI kwa wakati huo. Ndiyo maana tunasema kwa ujasiri kwamba, kama kweli haki itaonekana kutendeka, basi bahasha nyingine yenye majina ya KIBAKI, WAHARIRI WA MEDIA KARIBU ZOTE KENYA lazima apewe Annan. Vinginevyo jamii ya kimataifa ijitayarishe tena, kwani Kenya inaweza kurudi ilipokuwa na mambo yakawa mabaya zaidi.Mungu apishe mbali. Hayo ni maombi yetu.Tena bahasha ya tatu lazima iwe na majina ya AMERIKA na CHINA kwa kosa la kuvipatia vyama vya kisiasa pesa za kufanya kampeni za uchaguzi.Watakaoshitakiwa lazima wawe wengi ndipo haki ionekane kutendeka. Kama mtumishi wa Mungu, kusameheana ndiyo njia muafaka kwa Kenya.Pendekezo langu ni katiba ibadilishwe iwaruhusu wananchi wote kugombea uongozi bila kuwa wanachama wa vyama vya kisiasa. Pia katiba iwazuie watu kutumia pesa zao binafsi kufanyia kampeni.Halafu katiba ishurutishe Media kuwaangazia wagombea wote sawa.Kama kulipwa, vyombo vya habari vilipwe kiwango sawa na serikali.Katiba tena ipige marufuku AMERIKA na CHINA kuvipa vyama vya kisiasa au watu binafsi pesa kwa lengo la kufanyia kampeni.Hayo yakifanyika, Mzee au kijana wa KIBERA au KILELESHWA, atagombea kiti chochote popote Kenya na atachaguliwa kwa misingi ya uwezo wake kuongoza na siyo vinginevyo.Wanahabari watakuwa na matumbo makubwa siyo kwa sababu wamehongwa na wanasiasa, bali wamelipwa kulingana na ujuzi wa kufanya kazi zao sawa na maadili ya taaluma yao.Waimbaji wa INJILI wataacha kutunga nyimbo za kuwasifu wanasiasa na watatunga nyimbo za kumsifu Mungu na kueneza injili. Naona nilikuwa nasahau bahasha ya nne. Hii inatakiwa iwe na majina ya wasanii pamoja na wanariadha wote waliotumiwa na wanasiasa kuwagawa wakenya katika misingi ya kikabila.Sasa si mnaona? kama kushitakiana, kila mtu atashitakiwa Kenya. Jela zote zitajaa waandishi wa habari, Polisi, maofisa wa tume ya uchaguzi, Rais Kibaki na rais mstaafu MOI, Wanasiasa karibu wote,Waimbaji wa nyimbo za injili pamoja na wanariadha. Je tuna magereza yenye uwezo wa kubeba watu wote hawa? Msururu bado ni mrefu. Hata balozi wa AMERIKA Kenya atakuwemo.Je mtampeleka KAMITI au SHIMO la TEWA? Kwao jela ni sawa na hoteli ya kifahari. Kuna jamaa nimemsahau. Nafikiri hata WAKI alisahau kumweka kwenye bahasha.RAILA AMOLLO ODINGA. Hivi kweli hakuchangia kwa lolote kuifikisha Kenya ilipokuwa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi? RUTO je? UHURU KENYATTA? Niache nisije nikataja mhariri wa KBC na NTV waache kucheza nyimbo zangu.Lakini CITIZEN na KAMEME hawakuwatetea wakikuyu kwa hali na mali? Je K24? KTN siogopi kuwataja maana hata hawachezagi nyimbo zangu. Hawa walikuwa ODM damu.Jeff Koinange sijui awekwe bahasha gani. Kelele zake zilikuwa zikiishia Nairobi pekee. Kama K24 ingekuwa nchi nzima, Basi JEFF KOINANGE alipaswa kuwa kwenye ile bahasha ya kwanza ya WAKI. Mnaona? majina ni mengi. Na bado mtasikia mengi.Basi tuache tusameheane yaishe. Lakini nani mwenye uwezo wa kunyamazisha ripoti ya WAKI? Ni Kibaki? Ama RAILA? Au ni BUNGE? Pengine MAHAKAMA? Au tuseme maandamano ya halaiki. Yanaweza kweli kusimamisha ripoti ya waki isitekelezwe? Au ni Amerika? Pengine CHINA. Nani hasa mwenye uwezo wa kuzima pima joto hii??? Hicho ndicho kitendawili kigumu. Mwandishi ni mwimbaji wa nyimbo za injili Faustin Munishi.Sijui naye atakuwa kwenye bahasha gani?
Video Nyingine Hizi hapa
VIDEO 2/3/4/5/6/7/8/9/10/11/12/13/14/15/


VIDEO 2/3/4/5/6/7/8/9/10/11/12/13/14/15/

Tangaza Biashara yako Hapa

Kwamba uko hapa, maelfu ya wengine duniani wako hapa. Tatizo siyo kuwa na Web Site, ila swali ni wangapi wanaoifahamu na kuitembelea? www.munishi.com sasa inatembelewa na watu zaidi ya elfu mia nane kwa mwezi, na wengi wao wakiwa kutoka Afrika mashariki na kati. Ni kweli Internet haijafanyika kuwa njia kuu ya mawasiliano kwa wengi, lakini tunaelekea hapo. Tofauti na kutangaza kwenye gazeti ambalo kesho litafungia nyama, Bora uigundue njia hii ya kuweka tangazo lako hapa na litakaa kwa muda mrefu mpaka lisomwe na kila mtu. Bei zetu ni sawa na bure. Tuma picha na maelezo kwa munishi@munishi.com

http://munishi.com
Send photo and information to munishi@munishi.com


Delmonte Thika Kenya


NAKUMATT Kenya. Mabingwa wa kuuza kila kitu. Ukitaka kanda za nyimbo za injili, utazipata NAKUMATT


 


Kasanga Music Store

Click the picture for www.coexistkenya.org

Video Nyingine Hizi hapa
VIDEO 2/3/4/5/6/7/8/9/10/11/12/13/14/15/
 
biashara| http://munishi.com |